Diamond Amkana Irene Adai Yupo Naye Kikazi Tu

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amekana kabisa kuwa Kwenye Mahusiano na video vixen maarufu kama Irene Godfrey maarufu kama Lynn.

Tetesi za wawili hao kuwa Kwenye Mahusiano zilipamba moto wiki iliyopita baada ya picha zilizowaonyesha wako pamoja kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Tetesi hizo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Staa huyo ili kupata ukweli kuhusu taarifa ambapo alimkana binti huyo na kufunguka:

Kwa nini kila mwanamke nahusishwa naye? Tatizo kila mrembo ninayekuwa naye karibu kikazi watu wanasema natembea naye. Hakuna chochote kati yangu na huyo Lynn zaidi ya kufahamiana naye kikazi.

Kuna wakati napata ugumu sana maana kila mwanamke ninahusishwa naye wakati hata sijawahi kumtamkia neno la mapenzi zaidi ya kazi tu.

Unajua kazi yangu ni muziki so (hivyo) kukutana au kuwa karibu na warembo ni sehemu ya kazi yangu, sasa watu wakiniona nao wanajua tayari niko nao kimapenzi

Lakini pia, gazeti la Ijumaa lilimtafuta mwanadada huyo na kumbana ili kupata undani wake na Diamond kama wapo kwenye uhusiano au walikwenda kwa ishu ya kikazi, lakini aliishia kutoa povu kwa mwandishi wetu.

Nini? Bwana? Mi’ sijui, mniache na maisha yangu, tena mniache”.

Diamond Platnumz na Irene Waonekana Pamoja Zanzibar (+picha)

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz amedaiwa kuonekana kwenye visiwa vya Zanzibar akiwa na video queen Irene Hillary.

Diamond ambaye alitangaza kuwa yupo Single wiki iliyopita baada ya kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi na mama  watoto wake Hamisa Mobetto, ameonekana kupata mpenzi mwingine.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Diamond ana Mahusiano ya Kimapenzi na Irene mpaka kuna muda ilisemekana kuwa aliwahi kubeba ujauzito wake.

Diamond ambaye kwa sasa yupo visiwani  Zanzibar kwa ajili ya kazi zake za sanaa anadaiwa kuonekana na Mrembo Irene wakiwa bega kwa bega kuonyesha kuwa wako pamoja.

Picha ambayo inasambaa Kwenye mitandao ya kijamii inawaonyesha wawili hao wakiwa pamoja na crew nzima ya WCB:

 

Irene Amtupia Dongo Zito Wema Inadaiwa Kisa ni Diamond

Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

 

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.

Official Lynn- Diamond Namjua Vizuri Sana

Video queen maarufu anayejulikana kama Irene amefunguka na kukiri kumfahamu vizuri mwanamuziki wa bongo fleva Diamond Platnumz anayetamba zaidi kwa skendo zake na watoto wazuri.

Wiki iliyopita Irene alizua gumzo zito baada ya kueleza kuwa msanii Diamond alimpa ujauzito mapema mwaka huu lakini kwa bahati mbaya ujauzito huo uliharibika.

Tetesi za Diamond kuchepuka na Irene zilianza kupamba moto baada ya Irene kurusha picha za Diamond kwenye mitandao yake ya kijamii na zilizidi baad ya kitokea kwenye video ya kwetu ya Rayvannny baada ya Tayvanny kuanza kutoka na Fahyma ambaye rafiki wa karibu wa Irene watu walidai kiwa wawili hao wamegawana.

Hivi karibuni Irene alifanya mahojiano na LilOmmy ambapo alifunguka mengi kuhusiana na uhusiano wake na Diamond:

Kusema ukweli nilipitia kipindi kigumu sana kwa sababu mashabiki wa Zari au Team Zari walikuwa wananishambulia sana  hadi kunisababishia kujisikia vibaya lakini ikotokea nikapata nafasi ya kidate naye siwezi nikakataa kwa sabanu ni mtu wangu ambaye namjua vizuri sana”.