Nitafurahi Kama Diamond Atamuoa Wema: Esma Platnumz

Dada wa supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan amefunguka na kudai kuwa atafurahi endapo kaka yake atamuoa Wema Sepetu.

Tangu Diamond atangaze kufunga ndia mwaka huu baada ya kuachana na mama watoto wake na mpenzi wake wa miaka mingi Zarinah Hassan ‘Zari’ swali pekee lililopo midomoni ni mwanamke gani ambaye Diamond anaweza kumuoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na ‘Over the weekend’ alifunguka kuwa kwa upande wake hawezi kumchagulia mke kaka yake lakini Kama moyon wake ukiamua kurudi kwa Wema basi yeye moyoni mwake furaha zaidi.

Unajua Naseeb ndio anajua zaidi mke anayemfaa, lakini kama pia ataamua kurudi kwa Wema, mimi nitafurahi zaidi kwa sababu ni mtu ambaye tunapatana sana na ninampenda pia”.

Tangu Diamond atangaze ndoa kabla mwaka huu haujaisha kuna wanaodai atakayeolewa ni Wema wengine wanasema ni Zari na pia kuna wanaodai ni Hamisa.

Irene Amtupia Dongo Zito Wema Inadaiwa Kisa ni Diamond

Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

 

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.

“Hakuna Mwanamke Aliyeniliza Kama Wema”- Diamond

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz anazidi kutengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii Ikiwa albamu yake ya ‘A boy From Tandale’ Ikiwa sokoni kwa hivi sasa.

Diamond amefunguka na kueleza ya moyoni mwake ambapo amekiri kuwa hakuna mwanamke ambaye alikuwa kumliza kwenye mapenzi kama Wema.

Diamond amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya nchini Kenya na Citizen Radio na Willy .M. Tuva, ambapo amedai Wema ni mwanamke ambaye alimtambulisha sana machozi.

Mara ya mwisho kulia kwa sababu ya mapenzi ni nilivyokuwa na uhusiano na Wema Sepetu dah yule mwanamke ameniliza sana hadi nakumbuka kuna siku nilikuwa pale home nipo gym babu Tale akawa ameona kuna maambo mabaya mabaya mtandaoni akaniambia mdogo wangu si uachane naye? Mi nakumbuka nikamwambia yaani sikudanyi bosi yule mwanamke nikiwa naye najisikia kama niko peponi  kwaiyo hata tulivoachana alikuwa haamini”.

Lakini pia Diamond amesisitiza kuwa ni kweli amemwaga na Zari na wala sio kiki kama watu wengi wanavyodai ila amesema kwa sasa hataki kumuongelea Zari kwani ameelekeza nguvu zake kwenye kuitangaza albamu yake iliyotoka siku chache zilizopita.

 

Wema: Zari Alimuacha Diamond Kwa Mambo Aliyomfanyia Huko Nyuma Sio Kisa Mimi

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema anaamini Zari alimuacha Diamond kwa mambo yao waliyotofautiana kipindi cha nyuma lakini sio kisa yeye alimkumbatia.

Baada ya Zari kutangaza kumuacha Diamond alifanya Interview na BBC Swahili na aliweka wazi kuwa amemuacha aliyekuwa mpenzi wake supastaa wa Bongo fleva Diamond kwa sababu ya yeye kukumbatiana na Wema kwenye party.

Wema na Diamond walikuwa pamoja kwa miaka kadhaa huko nyuma na wamekuwa na tabia ya kuachana na kurudiana hata Diamond amedaiwa kuchepuka kwa wapenzi wake wapya na Wema hivyo alivyoonekana tu Wema wanakumbatiana ikaonekana tayari.

Lakini Wema amekataa tuhuma za Zari kuwa amemuacha kisa yeye Kwenye Interview aliyofanya wikiendi iliyopita na Bongo 5 Wema Alitalia maneno haya juu ya suala hilo:

Zari alikuwa ana sababu nyingi sana za kupanick za nyuma za Diamond za mambo yao wenyewe lakini sio hiyo ya juzi ya mimi kumkumbatia Diamond kama rafiki atakuwa ana jingine”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa pamoja na yeye na Diamond wameachana kipindi kirefu kilichopita lakini bado wana chemistry ambayo haiwezi kuisha.

Wema alipotakiwa kumshauri kitu chochote Zari alifunguka na kusema kuwa hawezi kuwa mshauri wa Zari kuhusu Mahusiano yake na Diamond.

“Mimi na Diamond ni Marafiki Hakuna Kingine Kinachoendelea”- Wema

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amesisitiza na kusema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Diamond zaidi ya urafiki na ukaribu wa kawaida.

Tetesi za wawili hawa kurudiana ziliibuka mwezi uliopita baada ya Wema kuibuka kwenye moja ya party za WCB na kuanza kukumbatiana na Diamond kimahaba kabisa na ishu hii ilizidi kupamba moto baada ya Zari kukiri kumuacha Diamond kisa kumkumbatia Wema.

Diamond na Wema Enzi za mapenzi yao

Tangu sakata hilo Diamond ameshakataa tuhuma hizo na kusema yeye na Wema ni marafiki tu hawana uhusiano mwingine wowote na Wema pia ameibuka na kuthibitisha hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Wema alifunguka na kusisitiza kuwa yeye na Diamond wamebaki kuwa marafiki wa karibu tu:

Mimi na Diamond ni marafiki ni marafiki wazuri, nadhani kinachowafanya wengi washangae ni kwa sababu mimi na yeye tulikuwa hatuongei kwa muda mrefu tangia tulivyoachana lakini sahivi tumeamua kukua na we decided to just put all those things behind us na maisha yaendelee kwaiyo hakuna cha kushangaza mimi kuongea naye au akinikaribisha kwenye party za WCB lakini kilichowashangaza ni mimi kuenda kwenye partu akaja kunisalimia mimi and Diamond we did not kiss nilimhug I hug my friends”.

Wema ameendelea kusisitiza kuwa yeye na Diamond ni marafiki tu hakuna cha zaidi na mambo aliyofanya na Diamond pale anaweza kufanya na mtu mwingine yoyote ambaye ni rafiki wa kawaida.

Martin Kadinda Ajikanyaga Kuhusu Penzi La Wema na Diamond

Mbunifu wa mavazi na mwanamitindo maarufu nchini Martin Kadinda ambaye pia anajulikana hasa kwa kuwa Meneja wa Muigiaji wa Bongo movie Wema Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu na kujikanyaga alipoulizwa kuhusu hali ya penzi la Wema Sepetu na Diamond Platnumz.

Wiki iliyopita aliyekuwa Staa Diamond Platnumz aliachana rasmi na mpenzi wake Zari na hivyo kuacha nafasi ya watu kujaza nani atakuwa na Diamond kwa hivi sasa na moja kwa moja kila mmoja alielekeza macho yake kwa Wema.

Wema na Diamond wamekuwa wakitawala headlines mbalimbali kwenye social media wakidaiwa kuwa wamerudiana huku kitu kikubwa kilichosababisha hiyo yote ni baada ya Wema kuonekana akikumbatiana na Diamond hadharani.

 

Diamond na Wema wiki chache zilizopita

Martin sio tu alikuwa meneja wa Wema bali pia ni rafiki wa karibu kwaiyo kutokana na ukaribu alionao na Wema gazeti la Amani lilimtafuta na kumuuliza endapo hizi tetesi zinasombaa kuwa Diamond na Wema kurudiana zina ukweli wowote m? Cha ajabu Martin alijikanyaga sana kujibu swali hili mwishowe alisema;

Jamani mimi siwezi kuzungumzia lolote kuhusu hilo na hata sijui nianzie wapi kuzungumza lakini kama ishu nyingine yoyote nitazungumza kwa mapana yote lakini sio suala hilo hata kidogo kwa kweli”.

Martin aliulizwa swali hilo kwa sababu siku ya tukio la Diamond na Wema kukumbatiana na kupeana busu wiki chache zilizopita Martin naye alikuwepo na alionekana kuongea na Diamond Pamoja na Wema.

Diamond Atokwa na Povu Zito Baada ya Tetesi za Kurudiana na Wema Kutapakaa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amewatolea povu zito watu wote ambao wamemtemea cheche siku ya jana baada ya tetesi za yeye kurudiana na Wema Sepetu kutapakaa kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema miaka minne iliyopita lakini baada ya kuachana urafiki uliisha na waligeuka maadui wakubwa sana kwa kipindi kirefu lakini baadae wawili hao walisema wamemaliza tofauti zao na wamekuwa marafiki.

Siku ya jana mitandao ya kijamii yote ilitawaliwa na skendo za Diamond na Wema ambapo picha na video zilizosambaa mtandaoni ziliwaonyesha wawili hao wakiwa wamekumbatiana na kupapasana na hata kuna muda Wema alitaka kumpiga busu Diamond.

Baada ya kuongelewa sana na watu kumponda Diamom kwa kuanzisha ukaribu ule na Wema wakati anajua wazi kuwa ana familia yake anayoiumiza hasa mpenzi wake Zari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliwatolea povu Kali wote waliomtolea cheche baada ya habari za yeye na Wema kutapakaa:

Wengi hupenda kuona watu wakiwa kwenye vita au uhasama usio na kichwa wala mguu eti utamsikia mtu anasema “Dogo mimi shabiki yako Mkubwa na ninaukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema ‘umeniuzi’ kwa iyo wewe unataka mimi niendelee kuwa na vita na Wema ili iweje? Yaani nikiwa na vita na Wema wewe unafaidika nini? ama itasaidia vipi kwenye sanaa yetu? Huwezi kuwa shabiki yangu alafu unafurahia mimi kuwa na vita na mtu tena vita ambayo imeshaisha…Nina familia yangu naipenda naiheshimu…ila hiyo sio sababu ya kuwa na vita na watu na huu mfano mwingine unafuata…shukrani sana madam kwa kuja usiku wa Jana”.

 

Diamond na Wema Wabambwa Ndani ya Mahaba Mazito hadharani (picha na video)

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezua gumzo siku ya Jana baada ya kuonekana hadharani na aliyekuwa mpenzi wake muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu huku wakionekana wakiwa wanashikana shikana .

Diamond na Wema waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka kadhaa iliyopita lakini waliachana mwaka 2014 ambapo Diamond aliendelea na kuanzisha mahusiano na mzazi mwenzake Zari na Wema aliendelea na wanaume wengine.

Siku ya Jana label ya Diamond WCB iliandaa hafla kwa ajili ya kumtambulisha msanii wao mpya Marombosso au maarufu kama Mbosso aliyekuwa kwenye kundi la Yamoto Band.

Tafrija hiyo ilifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Hotel ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Wema Sepetu, ambaye alionekana akiwa beneti na rafiki yake Aunty Ezekiel.

Lakini baada ya muda macho yote yalikuwa kwa Wema na Diamond kwani katika hali iliyowashangaza wengi ukumbini hapo Diamond alianza kukumbatiana na Wema na kushikana shikana nywele na kupapasana migongo.

Baada ya picha hizo na video kusambaa na kila mmoja kuongea lake Mange Kimambi alifunguka na kusema kuwa Wema na Diamond wamerudiana na inavyosemekana hivi sasa ni kuwa Wema ana ujauzito wa Diamond na ndio maana Wema anamchukia sana Hamisa hiyo yote ni kwa sababu ya kuzaa na Diamond.

Mpaka sasa haijajulikana Zari na Diamond wanasimama wapi kama Wema na Diamond wamerudiana kati ingawa hakuna aliyethibitisha taarifa hizo mpaka hivi sasa ingawa Zari aliposti video akiwa kanisani siku ya jana.