“Si mtegemia mtu mimi” Diamond Platnumz awaambia wandiishi wa habari wanaomharibia sifa

Inaonekana kuwa Mwimbaji Diamond Platnumz amechoshwa na wanatangazali na waandishi ambao wamekuwa wakimsema vibaya. Kupitia interview aliyoifanya na Kings FM Diamond alisema kuwa wanajiharibia wakati.

Diamond Platnumz aliendelea kusemakuwa hapo alipofika, hategemei Redio wala TV kumpa push anapotoa nyimbo zake. Hivi sasa yeye ni big fish na anaamini kuwa mashabiki wake wapo kumsaidia kupromote projects zake.

“Unajua kwamba kuna kiwango unapofikia,unapokuwa na mashabiki wengi,lazima uongeze ufanisi wako wa usambazaji wa kazi zako.Tuna redio tuna TV, lakini pia lazima tuongeze namna zingine za kupromote kazi zako,” amesema Diamond.

Akizungumza exclusively na Prince Ramalove kupitia Kings FM, Diamond aliendelea kusema kuwa waandishi na wanahabari hupenda kutengeza controversy kupitia wanachoandika kumfanya mtu kukakaa vibaya mbele ya watu.

“Wasanii wanatakiwa wajiongeze, sasa naona kuna watu wameichukua tofauti na kuipindua kumtengenezea mtu baya,lakini wanapoteza muda.”

Hata hivyo, Diamond Platnumz aliongeza kusema anaheshimu media ata wanapomchomea picha, bado yeye anaamini kuwa hiyo ni part of their wrok.