Madee Amshauri Dogo Janja Kuhusu Maisha Yake Ya Ndoa.

Bado katika mitandao kunafuka moto kwa zile habari za msanii wa bongo fleva Dogo Janja kufunga ndoa na msanii wa bongo movies  Irene Uwoya, kwa tukio ili kila mtu amekuwa na maoni tofauti tofauti kwa wasanii hao huku wengine bado wakionekana kutokubaliana na habari hizo.

Akithibitisha uwepo wa harusi hiyo mama mzazi wa Dogo Janja alisema kuwa Dogo Janja amefunga ndoa na Irene  Uwoya akiwa anajua kabisa na alitoa baraka zake zote kuhusu ndoa hiyo huku akisema kuwa yeye kutokuwepo katika ndoa hakubalishi chochote kwa sababu alikabidhi majuku yote yanayopaswa kufanywa na wazazi kwa msanii Madee.

Madee ni moja ya wasanii wakubwa na wakongwe  ambae aliamua kumchukua Jogo Janja na kuamua kumkuza na kumsaidia kimuziki,hata hivyo akiwa kama baba Madee amefunguka na kusema kuwa yeye kama baba wa Dogo Janja ameamshauri Dogo Janja kutokaa na kusikiliza maneno ya watu katika mitandao kwa sababu watu wengi wa kwenye mitandao wamekuwa na tabia ya kuwapangia wasanii nini cha kufanya.

Madee  anasema kuwa mara ya kwanza alishtushwa na taarifa hizo za kuoa kwa DogJ janja lakini kama mtu wa karibu ni lazima atoe sapoti , anamwambia Dogo Janja kuwa yeye na mwanamke aliemuoa wote ni wasanii na ni maarufu kwaio majina yao yanaweza kuwa midomoni kwa watu mara kwa mara lakini hii isiwafanye wakaanza kuishi tofauti na vile walivyo.

Irene Uwoya na Dogo Janja walifunga ndoa Oktoba 28, huku wakiacha midomo ya watu wengi wazi kutokana na uwazi wa umri uliokuwepo kati ya wawili hao, huku baadhi ya wasanii na mashabiki wakiamini kuwa hiyo ni kiki au kuna kitu kinatengeza katika kazi zao.Hata hivyo wawili hao wamethibitisha ndoa yao na wanasema wanapendana.Tunawatakia kila la kheri wawil hao.

Ushauri wa Madee unakuja baada ya kuona kuwa kumekuwa na wasanii wengi  wakilalamika kupokea mashambulizi kutoka kwa mashabiki zao  na hata kutaka kuwapangia jinsi ya kuishi.