Madee Asumbuliwa na Ndoto ya Kumiliki Ndege

Msanii wa muziki bongo, Madee amefunguka na kuweka wazi kuwa amekuwa na ndoto nyingi nazingine zimekuwa zikitimia kwa haraka sasa lakini kwa sasa hivi ndoto kubwa aliyonayo na inayomsumbua ni ile ya kutaka kumiliki ndege yake mwenyewe.

Msanii huyo wa muda mrefu kutoka katika kundi la tip-top connection amekuwa moja ya wasanii waliwhi kujitoa sana kwa ajili ya kufanukisha ndoto za vijana wengi akiwepo Dogo Janja amabe kwa sasa amekuwa msanii mkubwa huku akitokea katika mikono ya msanii huyo.

Madee amebainisha hayo katika ukurasa wake wa instagram, baada ya kuweka picha ikimuonyesha yuko mbele ya ndege na kuandika kuwa hiyo ndio ndoto inayomsumbua sana kwa sasa maishani.

Kila mtu amekuwa na ndoto katika  maisha yake na swala la kuifanikisha kwa ndoto hiyo utegemea na vile unavyofanya kazi ili kufaniskisha hilo, mashabiki wa madee wamepa moyo Madee na kumtaka ajitume kufanikisha hilo , ingawa pia wapo waliompuuza na kuona kama hatoweza kufanikiwa katika hilo.

 

Alichosema Madee Kuhusu Ongezeko la Nyimbo Mbaya.

Madee ni moankatia ya wasanii waliotoka mbali sana na kupitia mengi katika muziki na kwa sababu hiyo basi anatupa uzoefu wake wa kipindi yeye anaanza muziki na vile ilivyo sasa hivi,.

Madee anasema kuwa hapo awali ilikuwa ngumu sana kutoa nyimbo tu kama sasa hivi kwa sababu walikuwa wanaanda nyimbo hapo zamani walikuwa wakifanya kwa kuangalia nyimbo nzuri na ipi mbaya , kama mbaya basi haitatengenezwa lakini sasa hivi hakuna kitu kama icho.

Madee anasema kuna nyimbo sasa hivi ni mbaya sana na ziko nyingi, hii ni kwa sababu ma-producer wa sasa hivi hawaichunguzi nyimbo kabla ya kuitoa.Lakini pia hii inasababisha kuwepo kwa nyimbo nyingi sana na kufanya baadhi ya hizo kutosikika kabisa.

zamani ulikuwa mpaka utoe ngoma inabisi iw inafanya vizuri kwa sababu ulikuwa ukienda kwa producer anakwambia kabisa kuwa hii ngoma wala sio nzuri,lakini maproducer wa sasa hivi naona wako tofauti sana inabidi ifike sehemu producer amwambie msanii kuwa ngoma hii sio nzuri na wala hasitoe.Kwa namna hiyo naona ndo tutapata ngoma nzuri na ambazo zitakuwa zinasikika  kwa sababu kwa mtindo wa wasanii kutoa ngoma kila siku unafanya ngoma zingine zisisikike kabisa.

Madee Hana Mpango wa Kufanya Kazi na Warembo.

Msanii wa bongo fleva nchini madee, amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kusimamia wasanii wa bongo fleva wa kike kama wanavyofdanya watu wengine  katika lebvel yake.Madee amesema sababu ya kufanya hivyo ni ili kuepukana na usumbufu ambao anaweza kuupata.

Hapana, sipendi tu mambo hayo namwachia Daxo Chali, ndio anayaweza. Siwezi tu kukaa na watoto wa kike kwa sababu jinsia tofauti tutapishana maneno ataona nimemuonea,” Madee ameiambia Clouds FM.

Madee ameongeza kuwa kila siku hupokea simu zaidi ya 20 za wasanii wakitaka usimamizi chini ya MMB lakini kutokana hawezi kuwasaidia wote huishia kuwashauri. MMB kwa sasa ina wasanii wawili ambao ni Dogo Janja na Gaza

Juhudi za Madee Katika Kumuandaa Mtoto Wake Kimuziki.

Msanii wa muziki wa bongo fleva  Madee  amekuwa mstari wa mbele katika kumuandaa mtoto wake mdogo wa kike kuwa msanii wa baadae huku akifuata nyayo za baba yake  ili kufikia hatua aliyoifikia yeye.

Katika ukurasa wake wa instagram, madee ameweka pich aya mtoto wake huyo wa kike akiwa studio akitaka kuikaribia mic na chini ya picha hiyo madee aliandika”ipo siku utaifikia mwanangu wala huna haja ya kuharakisha”

Maneno hayo yanaonyesha ni jinsi gani Madee ameshatambua kipaji cha mwanae na amekuwa akifurahi kumuona mtoto huyo akiwa na kipaji kama chake   na amekuwa akitamani sana mtoto huyo kufikia alipofikia yeye.

Madee Atofautiana na Diamond Kuhusu Malezi ya Watoto.

Msanii wa muziki Bongo kutoka Tip Top Connection, Madee amesema iwapo wanae wa kike, Aimal Hamad  atachagua kuwa msanii kama yeye hatokataa kwa sababu na yeye pia amefuata nyayo za baba yake.
Mtazamo wa Madee unatofautinaa na ule wa Diamond Platnumz pale alipoulizwa kuhusu mwanae Tiffah kuja kufanya muziki. Katika mahojiano na KTN, May 2017 alisema anaogopa iwapo Tiffah ataingia katika muziki ataweza atembea kimapenzi na wanaume wengi.
Madee katika mahojiano na Bongo5 hivi karibuni alisema licha ya mara nyingi kuwa na wanae hata studio hajui iwapo atapenda muziki lakini yeye kama mzazi hawezi kumuwekea mipaka.

Tunashauriwa tuwaangalie watoto wafanye kile ambacho wanapenda kwa sababu anaweza kuwa anapenda mpira mimi nikamzuia nikamwambia afanye kitu kingine na asifanikiwe, nitakuwa nimepata lawama,” amesema.

“So akielekea huko mimi sina tatizo kwa sababu hata mimi mwenyewe nimemfuata baba yangu alikuwa ni mwanamuziki wa Western Tabora Jahazi Band wala hakutegemea nitakuwa mwanamuziki, so sitaona maajabu sana kwa sababu Waswahili wanasema maji hufuata mkondo,” Madee ameiambia Bongo5.
Mtoto wa Madee, Aimal Hamad ni miongoni mwa watoto wa wasanii ambapo pia wanapatikana katika mtandao wa Instagram.

Madee :Sifungi Ndoa kwa Kufuata Mkumbo.

Mkurugenzi wa Manzese Music Baby  Hamad Ally  amefunguka na kusema kuwa kamwe hatakaa afunge ndo kwa kufuata mkumbo kwa sababu kuna wasanii wamefunga ndoa ila  anataka kufunga ndoa kwa sapaizi ili kuwashangaza wengi kwa sababu hatatotangaza.

Madee ambae  kwa sasa anataka kufanikisha kusimama kwa kazi zake za muziki kwa kuimarisha wasanii katika lebo yake ambapo mpaka sasa ameweza kuwatoa Gaza na Dogo Janja.

unajua swala la kufunga ndoa sio swala la kukurupuka tu,ndoa ni kitu binafsi labisa na ni swala , ndoa ni kitu binafsi na ni maamuzi ambayo yanafanywa mara moja tu  uwezi kuwa na maamuzi tena pale ukishaamua.kwaio mimi kama mimi swala la kufunga ndoa  hiyo ni mipango nitakayoifanya mimi na familia yangu ambayo siwezi kuiweka wazi muda wote kuanzia sasa hivi ninaweza kufunga ndoa.

Wasanii wengi sasa wamekuwa wakijiingiza katika ndoa , na kuacha ukapera .Msanii kama AY, Shiloleh na wengine wengi wamefunga ndoa na wengine wanatarajia kufunga ndoa.

Madee Amshauri Dogo Janja Kuhusu Maisha Yake Ya Ndoa.

Bado katika mitandao kunafuka moto kwa zile habari za msanii wa bongo fleva Dogo Janja kufunga ndoa na msanii wa bongo movies  Irene Uwoya, kwa tukio ili kila mtu amekuwa na maoni tofauti tofauti kwa wasanii hao huku wengine bado wakionekana kutokubaliana na habari hizo.

Akithibitisha uwepo wa harusi hiyo mama mzazi wa Dogo Janja alisema kuwa Dogo Janja amefunga ndoa na Irene  Uwoya akiwa anajua kabisa na alitoa baraka zake zote kuhusu ndoa hiyo huku akisema kuwa yeye kutokuwepo katika ndoa hakubalishi chochote kwa sababu alikabidhi majuku yote yanayopaswa kufanywa na wazazi kwa msanii Madee.

Madee ni moja ya wasanii wakubwa na wakongwe  ambae aliamua kumchukua Jogo Janja na kuamua kumkuza na kumsaidia kimuziki,hata hivyo akiwa kama baba Madee amefunguka na kusema kuwa yeye kama baba wa Dogo Janja ameamshauri Dogo Janja kutokaa na kusikiliza maneno ya watu katika mitandao kwa sababu watu wengi wa kwenye mitandao wamekuwa na tabia ya kuwapangia wasanii nini cha kufanya.

Madee  anasema kuwa mara ya kwanza alishtushwa na taarifa hizo za kuoa kwa DogJ janja lakini kama mtu wa karibu ni lazima atoe sapoti , anamwambia Dogo Janja kuwa yeye na mwanamke aliemuoa wote ni wasanii na ni maarufu kwaio majina yao yanaweza kuwa midomoni kwa watu mara kwa mara lakini hii isiwafanye wakaanza kuishi tofauti na vile walivyo.

Irene Uwoya na Dogo Janja walifunga ndoa Oktoba 28, huku wakiacha midomo ya watu wengi wazi kutokana na uwazi wa umri uliokuwepo kati ya wawili hao, huku baadhi ya wasanii na mashabiki wakiamini kuwa hiyo ni kiki au kuna kitu kinatengeza katika kazi zao.Hata hivyo wawili hao wamethibitisha ndoa yao na wanasema wanapendana.Tunawatakia kila la kheri wawil hao.

Ushauri wa Madee unakuja baada ya kuona kuwa kumekuwa na wasanii wengi  wakilalamika kupokea mashambulizi kutoka kwa mashabiki zao  na hata kutaka kuwapangia jinsi ya kuishi.

 

Wolper amrarua Madee kwa kutumia katuni yake

Jacqueline Wolper amekerwa na hatua ya Madee kutumia katuni ya picha yake bila idhini yake kwenye video ya wimbo wake ‘Sikila’ aliyomshirikisha msanii Tekno kutoko Nigeria.

Mrembo huyo alidhihirisha kuwa hakufurahia alichofanya Madee kwa mtandao wa Instagram ambapo aliweka picha ya katuni yake na kuiambatanisha na ujumbe mrefu:

Picha ya katuni ya Wolper aliyotumia Madee kwenye video yake

“Hebu ona jamani, macho yanatia huruma kama nina upwiro kilo 200. Hii mikaka yetu ya Kibongo kuna muda inaboa, kuna muda inakuwa poa. Sasa Madee, Rais wa Manzese nikuulize swali, ulishindwa nini kunyanyua ka simu kako na kunipigia hata kinafiki na kuniambia unani-video queen katuni, sijui sanamu?

“Unajua wewe, acha dharau, wewe pumbavu, piga simu, omba kwanza, hata kama humlipi mtu, sisi tunasaidiana, wote wasanii, leo kwangu, kesho kwako na kunishika kimahaba, umenishika, una dhambi wewe kaka na suti umenivalia kama unaenda kutoa posa kwa Masawe.

Madee

“Sasa onyo, siku nyingine omba utapewa, acha kuparamia kama vile unaomba raundi kwa kimada wako, kwanza unitafute utoe hata faini ya kuniweka macho kama nimevuta ugoro.

“Ila nyimbo kali, nisiwe mchoyo na nimependa idea ila mwambie alinichonga na kunipa hiyo shepu nitampasua,” Wolper aliandika.

 

“Kuna kipindi nilikosa hata nguo za kuvaa” Rayvanny asimulia safari yake kimuziki baada ya kushinda tuzo la BET

Rayvanny alifunguka kuhusu maisha yake ya awali kabla ya yeye kuwa mtu mashuhuri na kupata hela. Staa huyo wa Wasafi aliamua kuongea kuhusu maisha yake ya awali baada ya kushinda tuzo la BET.

Ray alimshukuru sana Madee ambaye alisema alimsaidia sana wakati bado alikua fukara, staa huyo aliishi na Madee alipokuja Dar kutafuta riziki.

“Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Unaemuona mbele yangu.kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu @madeeali Alisimama namimi Kila Alipokua Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada yakuniona mnyonge Nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua akinipeleka studio nakunishauri Vitu vingi sana vyakimaisha na mziki pia nakusisitiza kua Nisikate tamaa.

Rayvanny na Madee

 

“Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi la watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari,nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari.Akaniambia mdogo wangu Unakitu Ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua Pia Nikawa mjanja wavitu vingi na kujiamini kisa yeye.Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA @madeeali” Rayvanny aliandika.

Picha 10 za Dogo Janja ambazo ni dhibitisho kuwa anang’ara kimavazi kushinda Diamond Platnumz

Muonekana wa Dogo Janja dhibitisho kuwa mwanamuziki huyo amewekeza pesa na muda katika mavazi. Dogo Janja sasa anashindana na Diamond kung’ara.

Msanii Madee alisema kuwa Dogo Janja amefanikiwa katika uvaaji kwa asilimia 92, alifunguka na kusema kuwa alikaa na Dogo chini na kumshauri

“Hicho ndio kitu tulijaribu kumshauri Janja na tukakaa naye vizuri na kumueleza na ndio kitu amefanya na amefanikiwa kwa asimilimia 92 na baada ya siku kadhaa naamini tutafika kule ambapo tunataka Janja awe na ule muuonekano,” Madee aliambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

Picha hizo hapo chini ni dhibitisho kuwa anang’ara kimavazi kushinda Diamond Platnumz:

Jibu Madee alilolitoa baada ya kuulizwa kuhusu mwanawe na msichana mwingine akiwa kwenye uhusiano

Leo kwenye kipindi cha Uheard cha Soudy Brown leo moto ulikuwa umewaka na ni baada ya  mkali wa muziki wa Bongofleva kutoka Mazense Madee kuulizwa kuhusu mtoto aliye naye msichana anayejulikana kama Minah.

Mtoto huyu alizaliwa wakati Madee alikuwa kwenye uhusiano mwingine na jambo hili liifanya penzi lao kuyoyoma.

Kulingana na Madee, wakati haukua kamilifu kuongelea jambo hilo aliambia Soudy Brown.

”Sasa kama nina mtoto mpya Soudy wewe ni nani mpaka nikuambie..? Taarifa zikiwa rasmi nitakuambia.” Alieleza kikamilifu

Minah yeye alikuwa tayari kuongea na hili ndilo jambo alilolisema:

”Asante mtoto mpya ana miezi minne, halafu sina rafiki anayeitwa Soudy na mbona Madee hajanitambulisha kama wewe ni rafiki yake. Kama Madee ni rafiki yako mbona hajakuambia jina la mtoto?”