Dr. Cheni Baba Yangu Wa Sanaa- Lulu

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuongelea uhusiano wake  na muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni.

Kwa miaka mingi sasa Lulu ameonekana kuwa karibu sana na Dr. Cheni na sasa anafunguka na kuweka wazi kuwa ni mtu wa muhimu kwenye maisha yake.

Katika mahojiano aliyofanya na Kituo cha Times Fm, Lulu amefunguka na kusema kuwa watu wengi hawajui uhusiano Wake na Dr. Cheni Lakini yeye amemtaja kama baba yake katika Sanaa.

Watu wengi hawajui Lakini Dr. Cheni ni baba yangu wa Sanaa, tangu alipogundua kipaji changu Nikiwa na miaka mitano, amezidi kuwa mtu wa muhimu kwangu katika kuikuza na kuiendeleza Sanaa yangu”.

Lakini pia Dr. Cheni ameonekana na Lulu katika wakati ambao alikuwa anapitia kipindi kigumu ikiwemo wakati ambao aliwahi kupelekwa jela.

Dr Cheni Aiomba Serikali Kuruhusu Mavazi ya Jeshi Kufanyia Filamu

Msanii dr cheni amefunguka na kusema kuwa katika vitu ambavyo bongo movies inakwama ni pamoja na sehemu za kufanyia movies zao kwa sababu Tanzania ina sehemu nyingi lakini kuna zingine hazifikiki wala kuruhusiwa kufanyiwa hivyo.

Akiongea wanahabari kutoka Clouds Media, Dr cheni anasema kuwa katika kikao walichokaa na kutaja mambo yanayowakumba katika kazi zao za sanaa, walitaja kuwa ifike sehemu serikali iruhusu kufanya filamu katika vituo vya polisi, madaraja makubwa ili pia kutangaza nchi na pia hata sare za jeshi na polisi kutumia ili kuleta uhalisia wa movies.

…..tukianza na upande wa serikali tunaiomba itusaidie kupata maeneo kwa ajili ya kufanyia kazi zetu, kwa mfano kwenye madaraja makubwa kwa ajiliya kuitangaza nchi, mbuga za wanyama pia, tumekuwa tukizuiliwa kwenye vituo vya polisi lakini hata sare a jeshi nazo turuhusiwe kuzitumia , kwenye viwanja vya ndege napo tunaomba serikali itufikirie.

Hata hivo bado msanii huyo amekuwa akisisitiza kuwa kwa sasa bongo movies imepoteza kabisa uboara wake na ndio maana hata yeye amekuwa sio mpenzi tena wa filamu za bongo kwa sababu ni mbovu.

Dr. Cheni Amefunguka Mazito Kuhusu Maisha Ya Lulu Gerezani

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni  amefunguka mazito juu ya maisha ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ gerezani.

Ni miezi kadhaa tangu Lulu aende jela baada ya kuhukumiwa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Wiki iliyopita tuliona jinsi Dr. Cheni alivyomuwakilisha Lulu kwa kutoa msaada kwenye kampenzi ya Namthamini ya EATV. Dr. Cheni ni mtu ambaye siku zote amekuwa na ukaribu sana na Lulu hadi Lulu humuita Baba yake.

Kwa mara nyingine Tena Dr. Cheni amefunguka kuhusu maisha ya Lulu gerezani ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv amefunguka haya:

Kusema ukweli Lulu ni binti jasiri sana yaani sisi tuliokuwa nje tuna majonzi kuliko yeye mwenyewe yaani ukienda unamkuta ana furaha mtacheka naye mtafurahi kikubwa anasema tu niombeeni basi na kitu kikubwa Lulu huko jela anatizama sana mabinti anasema anawapenda sana mabinti wa Kitanzania”.

Lakini pia Dr. Cheni amesema kuwa Lulu  ana kawaida sana ya kutoa misaada ingawa hapendi kujitangaza Kwenye mitandao ya kijamii pia amedai Miezi michache kabla hajahukumiwa alienda kutoa msaada segerea.

 

Lulu Michael Atoa Msaada Kutokea Jela

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameguswa na kampeni ya kuchangia pedi kwa watoto wa kike na kutokea gerezani alipo kwa sasa ametoa msaada wake kupitia kwa mtu wake wa karibu Dr. Cheni.

Kituo cha televisheni cha EATV kinaendesha kampeni inayoitwa Namthamini ambayo inakusanya na kupokea michango ya pedi kwa ajili ya kuwapelekea watoto wa kike wa shule mbali mbali ambao hawana uwezo wa kununua pedi.

Mchango huo kutoka kwa Lulu umewasilishwa na Muigizaji wa Bongo movie Dr. Cheni ambaye pia ni mtu wa karibu wa Lulu ambaye amesema Lulu ameguswa sana na kampeni ile na ameamua kutoa kidogo alichoweza kuwa nacho.

Kwenye mahojiano na East Africa Tv, Dr. Cheni alizidi kufunguka haya kuhusu mchango huo:

Kwanza niwapongeze kwa hii program nimekuwa mfuaatiliaji na naamini itakuwa na ‘Impact’ kubwa kwenye jamii.

Kikubwa mimi Mahsein @drchenitz ni Muwakilishi, nimeleta ‘pic kadhaa za Pads ambazo zitakuwa msaada kwa Wasichana wakitanzania.

Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU), Ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo, yupo (jela)

Zaidi amesema niwaambie ANAWAPENDA saana na anawataka mabint wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia”.

Lakini Dr. Cheni alisema tetesi zito zilizokuwa zikisambaa kwa muda sasa kuwa eti Lulu hayupo jela bali alishatoka na kafichwa nchini Uganda jambo ambalo amesema ni tetesi tu mitandaoni.

Dr.Cheni Awashangaa Wanaosema Hukumu Ya Lulu Haitoshi

Msanii mkonwe wa filamu za bongo ambae pia kwa muda wote amekuwa mlezi wa msanii lulu michael na amekuwa bega kwa bega  na lulu pamoja na familia yake katika kufatilia kesi ya msanii huyo Dr.Cheni amefunguka na kuwashangaa wanaosema kuwa hukuma aliyopewa   lulu ilikuwa haitoshi na  haikulingana na kile alichokifanya.

Dr.Cheni amefunguka hayo baada ya kuona watu wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa hukumu ya msanii huyo haiendani na mauaji aliyoyafanya  na wengine wakifikia hadi hatua ya kupendekeza kuwa ilitakiwa apewe kifungo cha kuanzia miaka mitano, sita na kuendelea.Hata hivy o mmoja wa watuwaliotoa maoni ya hukumu ya lulu alikuwa   baba mzazi wa Kanumba ambae alisema kuwa adhabu aliyopewa msanii huyo ni kama adhabu ya kuua kuku tu.

Dr. Cheni amesema kuwa watu hao wamekuwa hawamtakii mema lulu na kusema kuwa jambo baya lolote linaweza kumpata mtu yeyote  maana hakuna anaejua kesho yake, lakini pia amewashukuru wale wote waliomia na kutuma ujumbe wa pole kwa lulu pamoja na familia yake kwa ujumla.

Katika ukurasa wake wa instagram Dr.Cheni aliandika kuwa

Linapokukuta jambo wapo watakao kuonea huruma  na wapo watakaokuwa na furaha ila  niwakumbushe  jambo hakuana anaejua kesho yake kubwa kila mapito mwambie mungu  asante.watanzania tulio wengi  wanakuombea yaliyo meme na tunakuhaidi tupo nyuma yako  kukushika mkono  kwa kila hatua  maombi yao mungu atayasikia  hata kama hukumu imepita  tupo na wewe  na mungu yuko na wewe.-aliandika Dr.Cheni

Lulu alipata hukuma yake tarehe 13 november mwaka huu baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia , maujia yalitokea April 2012 baada ya kugombana na mpenzi wake ambae pia alikuwa msanii wa bongo movie Steven Kanumba.

Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kuumia na hukumu hiyo lakini wapo walikuwa wakilalamika na kusema kuwa hukumu hiyo haiendani na maujia hayo.Baada ya hukumu ya lulu mengi yamesemwa kuhusu msanii huyo.

Maoni ya Dr.Cheni katika ukurasa wake wa Instagram