Dulla Makabila Amuanika Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa singeli nchini Abdallah Ahmed maarufu kama Dulla Makabila amemuanika hadharani kwa mara ya kwanza mpenzi wake aliyemtambulisha kwa Jina la Maiya Abdul.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wawili hawa walinaswa ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo msanii wa filamu za maigizo nchini, Yvone Cherry ‘Monalisa’ alikuwa akizindua mpango wa kuwasaidia wasichana kufikia malengo yao kwenye tasnia ya filamu uitwao, Mona ACT.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Dulla alibanwa kuhusu Mrembo huyo ambapo alifunguka na kusema yule ndio mchumba wake na wanategemea kufunga ndoa siku za mbeleni.

Huyu ni mchumba wangu anaitwa Maiya na hapa nimefika kwani tuna malengo mengi ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa Mungu akipenda”.

Huyu ni mwanamke wa kwanza ambaye ameonekana hadharani na Dulla Makabila tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake Msanii wa Bongo movie Husna Sajent.

Penzi la Sajent na Dulah Makabila Laota Mbawa.

Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dullah Makabila na aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajent wadaiwa kumwagana na sasa hivi ni maadui wakubwa huku kila mmoja akikaa kimya na kukana tuhuma hizo ili kukwpa aibu ya kushangazwa na watu kwa kuwa kipindi cha mahusuiano yao walikuwa wameonekana kushibana sana.

Wawili hao ambao walikuwa wakionekana kupendana sana na kusemekana kuwa hawawezi kuachana kwa madai kuwa wanatagemea kufunga ndoa hivi karibuni lakini kwa habari za kunyapia ni kwamba wawili hao sasa ni maadui na penzi halipo tena.

Sajent ndie alikuwa meneja wa msanii huyo wa singeli huku akiwa na wasanii wengine wa singeli kama kina Sholo Mwamba lakini kutokana na wawili hao kujiingiza katika mapenzi ilimfanya meneja huyo(Sajent) kushibdwa kufanya menejiment kwa wasanii wengine na kujikuta akigombana na wasanii wengien kwa sababu ya kuwa na mapenzi na Dullah Makabila.

Akiulizwa kuhusu kuachana huko, husna sajent alionekana kuchukizwa na thuma hizo na kusema”hivi hakuna wasanii wengine wenye mahusiano ambao mnaweza kuwahoji , basi naomba muwaulize hao mimi nipo busy kwa sasa”

Kipindi  cha mapenz ya wawili hao yanavyoanza , Dullah makabila alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine alikuwa akijulikana kama Asali ambae alitoa hata mimba baada ya kupokonywa  bwana huyo na husnasajent.

Ni kawaida kwa wasanii na watu maarufu kushindwa kumudu katika mapenzi tena kwa Sajent na Dullah Makabila inakuwa ngumu zaidi kwa sababu wawili hao walikuwa ni mtu na bosi wake hivyo upande wa kazi pia unakuwa umeharibika.