“Chaz Baba Ni Wangu Hata Kama Amefunga Ndoa”- Husna Sajent

Msanii wa Bongo movie Husna Sajent ambaye amezaa na msanii wa dansi nchini Charles GabrielChaz Baba‘ ameibuka na kudai bado anampenda baba watoto wake.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa ikiwa  wiki moja imepita baada ya kufungwa kwa ndoa kisha kufuatiwa na sherehe kabambe kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, ndoa ya Msanii wa Bendi ya The African Stars Twanga Pepeta Chaz Baba na mke wake Mariam tayari visa vimeanza.

Chaz Baba alifunga ndoa kwa mara nyingine na mwanamke aitwaye Mariam. Katika ndoa hiyo visa vimeanza baada ya mzazi mwenza wa Chaz Baba ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Husna Idd ‘Sajenti’ kujitokeza na kusema kuwa anachojua jamaa huyo ataoa sana, lakini mke halali aliyepangiwa na Mungu ni yeye.

Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa, Sajenti alisema kuwa, Chaz Baba ni baba wa mtoto wake wa kwanza na anaamini kuwa hawezi kudumu na Mariam kwani atakuja kuwa mumewe kabisa baadaye. Sajenti alisema hata kama Chaz Baba amefunga ndoa hiyo haimpi shida kwani anajua tu atarudi kwake ili wamlee mtoto wao.

Najua Chaz ni wangu, kwani unajua zimepita ndoa ngapi kwake? Ndoa itakayodumu ni ile atakayofunga na mimi, hicho ndicho ninachokijua hadi ninaingia kaburini, asijidanganye, hawezi kudumu na huyo mwanamke (Mariam)“.

Husna Sajent Adai Mwili Wake Unaruhusu Kupiga Vimini

Muigizaji wa Bongo movie Husna Sajent amefunguka na kudai anavaa vinguo vifupi na vya kutega kwa sababu mwili wake unamruhusu kufanya hivyo.

Husna amedai kuwa hata kama akivaa vivazi vya mitego haisumbui kwa mtu yeyote kwa sababu mwili wake unamruhusu kufanya hivyo na ndio maana hafikirii mara mbili anapoamua kuzivaa.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Husna Sajent amedai kwamba watu wengi kwenye mtandao walikuwa wakimnanga kwa kuvaa mavazi ya kujiachia mwili lakini ni kwa sababau anajiamiani na sio kwamba ana kasoro yoyote kwenye mwili au makovu yanayomfanya avae nguo fupi za kumfunika miguu.

Sinaga kujibana kwenye mwili lakini pia wanaosema navaa nguo fupi sana ndivyo nilivyozoea kwa sababu sina tatizo lolote kwenye mwili wangu wala kovu hivyo nguo kama hizo ni kama zote na siwezi kuacha hata siku moja”.

Wasanii ambao wamekuwa na tabia ya kujiachia kwenye mitandao ya kijamii kwa kuvaa vijinguo vifupi wamekuwa wakikosolewa sana na mashabiki zao.

Dulla Makabila Kamuacha Husna Sajent na Kutembea na Rafiki Yake

Mkali wa muziki wa Singeli Abdallah Mohamed maarufu kama Dulla Makabila amedaiwa kufanya mazito kwani imedaiwa baada ya kumbwaga aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajent hivi sasa anatembea na rafiki yake kipenzi Tiko.

Muigizai wa Bongo movie Husna Sajent na Dulla Makabila walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu hadi kuna muda walitangaza kufunga ndoa lakini baadae wakaachana baada ya familia ya Dulla kumkataa Husna.

Habari za kimbea zinadai hivi sasa Dulla Makabila amewachanganya vibaya mno waigizaji hawa wa Bongo movie ambao ni Husna Sajent na Tiko Hassan ambao walikuwa marafiki wakubwa lakini sasa inasemekana ni maadui wakubwa baada ya kuibiwa bwana.

Tiko

Baada ya habari hizi kusambaa gazeti la Ijumaa Wikienda lilimsaka Husna na kumuuliza kuhusu tuhuma hizo:

Ni kweli kabisa Dulla aliniacha na yuko na Tiko kwa hivi sasa lakini mimi nimeshaanza kusahau hayo mambo nipo na ninaendelea na maisha yangu kwa hivi sasa”.

Baada ya hapo gazeti hilo lilimtafuta Dulla Makabila ili kupata ukweli wake kuhusu ushindani hiyo na alifunguka:

Kwa hivi sasa niko na Tiko ndiye mpenzi wangu lakini kuna vitu vilinifanya nifanye hivyo kuhusu suala la kuwachanganya mimi nilianza kumjua Tiko kabla ya Husna ni mwanamke aliyekuwa akilini mwangu na hata hivyo sioni kama kuna shida hata kama walikuwa wanajua na ilimradi nimeshuacha mmoja nipo na mwingine”.

 

Penzi la Sajent na Dulah Makabila Laota Mbawa.

Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dullah Makabila na aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajent wadaiwa kumwagana na sasa hivi ni maadui wakubwa huku kila mmoja akikaa kimya na kukana tuhuma hizo ili kukwpa aibu ya kushangazwa na watu kwa kuwa kipindi cha mahusuiano yao walikuwa wameonekana kushibana sana.

Wawili hao ambao walikuwa wakionekana kupendana sana na kusemekana kuwa hawawezi kuachana kwa madai kuwa wanatagemea kufunga ndoa hivi karibuni lakini kwa habari za kunyapia ni kwamba wawili hao sasa ni maadui na penzi halipo tena.

Sajent ndie alikuwa meneja wa msanii huyo wa singeli huku akiwa na wasanii wengine wa singeli kama kina Sholo Mwamba lakini kutokana na wawili hao kujiingiza katika mapenzi ilimfanya meneja huyo(Sajent) kushibdwa kufanya menejiment kwa wasanii wengine na kujikuta akigombana na wasanii wengien kwa sababu ya kuwa na mapenzi na Dullah Makabila.

Akiulizwa kuhusu kuachana huko, husna sajent alionekana kuchukizwa na thuma hizo na kusema”hivi hakuna wasanii wengine wenye mahusiano ambao mnaweza kuwahoji , basi naomba muwaulize hao mimi nipo busy kwa sasa”

Kipindi  cha mapenz ya wawili hao yanavyoanza , Dullah makabila alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine alikuwa akijulikana kama Asali ambae alitoa hata mimba baada ya kupokonywa  bwana huyo na husnasajent.

Ni kawaida kwa wasanii na watu maarufu kushindwa kumudu katika mapenzi tena kwa Sajent na Dullah Makabila inakuwa ngumu zaidi kwa sababu wawili hao walikuwa ni mtu na bosi wake hivyo upande wa kazi pia unakuwa umeharibika.

Husna Sajent Na Wolper Mambo Safi.

Wanadada wawili waliokuwa mahasimu wakubwa kutokana na kutembea na bwana mmoja kwa sasa wameamua kuweka mambo yao sawa na kuwa marafiki kama zamani kwa sababu yule aliyekuwa akiwafanya wagombane hayupo tena.

Kitendo hichi kimejidhihirisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwanadada Jackline Wolper ambapo alimuhalika mwanadada huyo na alihudhuria .Husna Sajenti na Jackline Wolper walikuwa kuwa maadui wakubwa baada ya Husna Sajent kutoka kiapenzi na aliyekuwa mpenzi wake na Jackline ambapo wawili hao waligombana kwa ajili ya mwanaume huyo.

Msanii  jackline wolper

mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la  Mwami Radjabu  inaesemekana ni mkongo alifikia hatua ya kumvalisha pete husna sajent lakini hawakubahatika kufunga ndoa na mwanadada huyo.

Hata hivyo moja ya watu wa karibu wa Husna Sajenti alisema kuwa wawili hao waliamua kuacha kugombana kwa sabau husna tayari alishaachana na mwanaume huyo na wameona kuwa hakuna haja ya wao kugombana ukizingatia wao wote ni wanawake.

Tulishamaliza tofauti zetu,sian tofauti  wala bifu na  Jackline, maana aliyekuwa anatugombanisha ni mwanaume na hayupo tena na sisi ni wanawake  na tujifunze kuwa wanaume ni watu wa kupita. Aliongea Husna Sajent

Hii itakuwa funzo pia kwa wasanii wngine hasa wa kike ambao wamekuwa wakiingia katika mabifu hovyo hovyo kwa sababu ya wanaume bila kujali maslahi ya urafiki wao kwanza.wasani wengi wa kike wamekuwa wakiingia katika migogoro kwa sababu ya kuibiana wanaume.