Tahiya Aachia Ngazi Kwa Mwanaume wa Hamisa Mobetto

Video vixen maarufu kama Tahiya John ambaye Hivi karibuni aliingia kwenye headlines Baada ya kuchukuliana mwanaume na Msanii Hamisa Mobetto.

Tahiya na Hamisa waliingia katika mgogoro kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya Hamisa kumnyakua Mpenzi wa Tahiya anayejulikana Kama Alex hadi kupelekea kuwafumania wawili hao Zanzibar.

Lakini Hivi karibuni Hamisa na Alex walionekana wakiwa katika Penzi zito Baada ya kuongozana pamoja katika tuzo za SZIFF zilizofanyika Wiki iliyopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Tahiya aliulizwa kama ameachana na mwanaume huyo ndipo alipoweka wazi kuwa amemsusia mwanaume huyo kwa Hamisa:

Siwezi kusema nimeachana Alex  au sijaachana naye. Bwana ee kama wameongozana watajijua wenyewe mimi sitaki kuwazu-ngumzia kabisa”.

Juzikati bwana huyo alionekana akiwa ameongozana na Hamisa kwenye Tuzo ndipo watu mitandaoni wakaibuka tena na kuanika kuwa wapenzi hao hawakuachana baada ya kufumaniwa na sasa mambo yapo hadharani. Hamisa aliposakwa kumzungumzia mpenzi wake huyo mpya alipokea simu na baada ya kuelezwa madai hayo alikata bila kusema chochote.

Hamisa Mobetto na Lulu Wazika Bifu Lao

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wameonyesha kuwa hawana Bifu na kila mtu hana kinyongo na mwenzake.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi Februari 23, 2019 katika utoaji wa tuzo za  Filamu Zetu International Festival Film (SZIFF) mwaka 2019  ambapo Lulu alimuita kwa mbwembwe jukwaani Hamisa Mobeto.

Lulu ambaye alikuwa Mshehereshaji (MC) kwenye Shughuli hiyo aliyofanya katika ukumbini wa Mlimani City, alimuita kwa mbwembwe na kusababisha kuibuka kwa shangwe kwa watu waliokuwa ukumbini hapo.

Ninamleta kwenu mrembo, model, mama wa Watoto wawili jukwaani na si mwingine bali ni Hamisa Mobetto”.

Baada ya kupanda stejini Hamisa alienda kukabidhi tuzo kwa moja ya washindi na kurejea kukaaa katika siri yake.

Siku za nyuma Hamisa na Lulu walishawahi kuingia kwenye Bifu zito Baada ya Hamisa kumtuhumu Lulu kwa kumuibia aliyekuwa Mpenzi Wake Majizzo lakini Hamisa alitangaza kuwa hana kinyongo na Lulu Baada ya kufungwa gerezani.

“Sijazaa na Diamond Pamoja Majizzo Kwa Ajili Ya Pesa”-Hamisa

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hajazaa na Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na CEO wa EFM kisa pesa kwani ana pesa zake binafsi.

Hamisa amesema watu wengi wakisikia amezaa na wanaume wenye uwezo kama hao basi moja kwa moja wanafikiri kuwa amefuata pesa Lakini hawajui kuwa pesa zake anatafuta mwenyewe kwa jasho lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Hamisa amekana stori za kuwa amegeuza watoto wake mtaji kwa kuishi kutegemea matunzo atakayopewa kwa ajili ya Watoto Wake na Diamond pamoja na Majizzo.

Mimi ni mtu ambaye nilikuwa najiweza vizuri tu kabla ya kuzaa na ninataka wasichana wadogo wanaoniangalia wajue kuwa kuzaa ndio kutoka kimaisha hapana sio hivyo, Nataka watu wajue kuwa sio kwamba kwa sababu nimezaa na wanaume wenye pesa basi ndio nimejirahisishia maisha hapana kila kitu nilichokuwa nacho ni jasho langu mwenyewe na nguvu zangu nimetumia kuvipata”.

Siku za nyuma Hamisa ameshawahi kusemekana kupangishiwa jumba la kifahari na baba wa Mtoto Wake Diamond Platnumz na kabla ya kuhamia hapo anadaiwa kuwa alipangishiwa nyumba na Majizzo.

Msanii Adai Hamisa Anastahili Kuolewa Kwa Mahari Ya Mil. 300

Msanii anayejulikana Kama Joto Dar Es Salaam ameibuka na kudai kuwa msanii mwenzake Hamisa Mobetto anastahili kuolewa kwa mahari ya milioni 300 kutokana na urembo Wake.

Muimbaji huyo ameyasema hayo siku ya jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa wimbo wake mpya “Amber Tuma” akiwa amemshirikisha Papii Kocha.

Mimi tayari ni mume wa mtu Lakini ningekuwa sijaoa kwa hapa Tanzania ningependa kumuoa msichana mmoja ambaye ni mrembo kati ya warembo wote ni Hamisa Mobetto.

Yaani mimi ningemuoa Hamisa Mobetto kwa gharama yoyote ile yaani hata wangesema milioni 300 ningetoa kumuoa kwa sababu kwanza ni mzuri sana lakini pia naona ana tabia nzuri sana”.

 

“Muacheni Hamisa Aishi Vile Atakavyo”- Mama Mobetto

Mama mzazi wa Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto, Shufaa Lutiginga maarufu kama Mama mobetto ameibuka na kumkingia kifua binti yake kutokana na skendo zinazomuandama.

Siku za Hivi karibuni Hamisa amekumbwa tena na skendo Mpya ya kumchukulia bwana msichana mmoj anayeitwa Tahiya.

Tahiya amemtuhumu Mobetto kwa kumchukulia Mpenzi Wake aliyetambulika kwa jina la Alex ambapo alifikia hatua ya kwenda Mpaka Zanzibar kwa ajili ya kwenda kumfumania.

Baadae Mobetto alianika picha akiwa na mwanaume huyo na kuonyesha kuwa hajamuiba bali alikuwa naye na kuwa yupo naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Baada ya sakata hilo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Mama Mobetto ili kupata maoni yake juu ya skendo hizo ambako zimemuandama Mtoto Wake ambaye mara moja alimwaga Povu zito na kusema mwanaye aachwe aishi anavyopenda mwenyewe.

Jamani nilishawaambia muacheni Hamisa aishi vile ambavyo yeye anapenda, msimfuatilie siku akihitaji kuongea na nyie atawatafuta yeye mwenyewe lakini siyo kila kukicha kumfuatilia”.

 

 

Hamisa Mobetto Afungukia Skendo Ya Kuiba Bwana Wa Mtu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto ambaye Wiki iliyopita aliingia kwenye headlines Baada ya kudaiwa kuiba bwana wa mrembo aitwaye Tahiya.

Tahiya ambaye ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond, alimtuhumu Mobetto kwa kumchukulia bwana ake anayeitwa Alex ambaye anatajwa kuwa mtoto wa Kigogo mmmoja hapa nchini.

Kushoto: Hamisa Akiwa na Alex Kulia: Tahiya Akiwa na Alex

Tahiya  aliposti picha ya Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya; “Hamisa Mobeto achana na wanaume za watu.”

Baada ya muda mwanadada huyo akaposti tena meseji zao zote alizokuwa wakijibizana na mwanamitindo huyo kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo Tahiya alionekana akimsihi Mobeto aachane na mpenzi wake lakini haikusaidia kwani mwisho wa waliishia kujibizana maneno mabaya huku kila mmoja akijiona anaweza zaidi ya mwenzake.

Baada ya skendo hiyo kutawala mitandao ya kijamii Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Hamisa Mobetto ili kupata Ukweli kwa upande Wake ambapo alifunguka na kusema:

Mnataka niwaambie nini, mlichokiona ndiyo hichohicho isitoshe mimi siyo mtoto mdogo kwa hiyo naelewa ninachokifanya, sijaiba mwanaume wa mtu ila alikuja mwenyewe na nampenda nifanyeje sasa”.

 

 

Mange Kimambi Amtolea Povu Zito Hamisa Mobetto

Mange Kimambi ameibuka na kumtolea Povu zito Msanii Hamisa Mobetto ambaye pia ni mdogo Wake wa hiyari Baada ya kuweka picha mtandaoni akiwa na mpenzi Wake Mpya.

Siku ya jana Mobetto aliingia kwenye vita ya mtandaoni na mrembo mwingine anayeitwa Tahiya Baada ya kumtuhumu Mobetto kwa kumchukulia mwanaume wake anayeitwa Alex.

Hamisa na Mpenzi Wake Alex

Ili kudhihirisha kuwa Mobetto hajamuiba mwanaume bali ni Mpenzi Wake na sio wa Tahiya Hamisa aliposti picha Kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na bwana huyo huku akimrushia vijembe Tahiya.

Baada ya sakata Hilo Mange alimjia Mobetto na kumtaka aache kujianika na wanaume tofauti katika mitandao ya kijamii ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuandikia ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/Bs1kmnTAnLN/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=4sk802wnincs

Esma Akiri Kumkumbuka Hamisa Mobetto

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kudai kuwa amemiss sasa Mzazi mwenzake na Kaka yake Hamisa Mobetto.

Esma ambaye amewahi kuwa na urafiki na Mobetto ameweza wazi kuwa mbali ya kuwa wifi yake Lakini aliwahi kuwa rafiki mzuri sana kwake hivyo anakuwa anamkumbuka sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Esma  alisema kati ya watu ambao huwa akikaa anawamisi, mmojawapo ni Mobeto kwa kuwa alikuwa ni rafiki mzuri kwake ingawa watu wengi hawalijui hilo.

Sijasema hivi kwa kutafuta kiki jamani ila nimeongea ukweli kutoka moyoni. Misa (Mobeto) alikuwa ni rafiki mzuri sana kwangu ingawa siku hizi kuna watu kwenye mitandao wanamuaribu na amekuwa tofauti na mwanzo”.

Urafiki wa Esma na Mobetto ulifikia kikomo mara Baada ya Diamond kumkataa Mtoto wa Mobetto na kusababisha ugomvi kati ya panda hizo mbili.

Idris Sultan Afungukia Tetesi Za Kujisogeza Kwa Mobetto

Staa wa filamu aina ya Komedi, Idris Sultan amefungukia tetesi zinazomkabili za kujisogeza kwa mwanadada anayetrend Hivi sasa kwenye Mitandao ya kijamii Hamisa Mobetto.

Tetesi hizo zilianza kusambaa Baada ya Idris kuonekana akikomenti sana kwenye picha za mrembo huyo mara tu Hamisa anapoposti picha zake basi Idris anekuwa akimuachia makopa tu.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa, Idris kwa sasa ameamua kujipooza kwa Mobeto.

Wamekuwa wakiongozana kila kona kama kumbikumbi, ndiyo kwanza mapenzi yao yanachipukia“.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, Gazeti hilo lilimsaka Idris ili kuupata Ukweli wa mambo kutoka kwake ambapo moja kwa moja alikana kabisa tetesi hizo na kumwaga povu:

Hebu acheni mambo yenu ya ajabu bwana kwa hiyo kila msichana nitakayeongozana naye basi ni mpenzi wangu? Halafu mmesahau kwamba mimi na Hamisa ni washkaji kitambo tu? Sasa kwa nini leo muanze kusema natoka naye? Muda mwingine watu wakikosa kazi ya kufanya huwa wanatunga tu vitu vyao”.

 

“Marafiki Wanamuharibu Hamisa”- Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameibuka na kudai Hamisa ni rafiki mzuri sema watu wanatajwa kama marafiki zake ndio  wamemuharibu.

Esma amefunguka hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo aliomba mashabiki zake wamuulie maswali yoyote na yeye angejibu na moja kati ya maswali aliyoulizwa yalimuhusu Hamisa.

Kama utakumbuka siku za nyuma Esma alishawahi kuwa na urafiki wa karibu na Hamisa Mobetto tena inasemekana alikuwa na urafiki na familia ya Diamond kwa miaka mingi.

Lakini urafiki huo uliingia shubiri baada ya Hamisa kuzaa na Diamond na kupelekea Bifu kubwa kati ya Hamisa na Familia nzima ya Diamond iliyopelekea urafiki wa Esma na Hamisa kuisha kabisa.

Swali la Kwanza:

Umemiss nini kutoka kwa Hamisa Mobetto alikuwa rafiki Yako sana?

Esma Akajibu:

Hamisa ni rafiki mzuri ila watu wanamuharibu tu”.

Swali la Pili:

Kwa nini hupendi Hamisa aolewe na Diamond?

Esma Akajibu:

Sijawahi kusema hivyo”.

Sakata la Hamisa na Esma lilichukua sura mpya Baada ya kumrushia tuhuma za uchawi dhidi ya kaka yake Diamond.

 

“Hamisa Ndio Kiboko Ya Zari”- Maimartha

Mtangazaji mkongwe nchini Maimartha Wa Jesse amerudi tena kwenye headlines za mitandao ya kijamii Baada ya kutoa kauli tata ya Hamisa Mobetto dhidi ya Zarinah Hassan.

Siku mbili zilizopita mlimbwende Hamisa Mobetto alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa na mmoja kati ya watu waliojitokeza kumtakia Birthday njema n Maimartha.

Maimartha Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuandikia ujumbe ambao ulizua maswali kwani alimuhusisha Mobetto na adui yake namba moja Zari ambapo aliandika maneno haya:

Happy Birthday Hamisa Kiboko ya Zari, ulijua kuwaparaganisha na Chibu…Zari alitamani akumeze ishi maisha dill yenye mafanikio”.

 

Nandy Kupanda Steji Moja na Hamisa Mobetto

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ametangaza habari njema kwa mashabiki Wake wanaokaa nje ya nchi kwani anatarajiwa kupanda steji moja na Hamisa Mobetto.

Nandy ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Aibu’ ameweka wazi kuwa mwezi huu baadae anatarajia kuungana na Hamisa Mobetto kwa ajili ya your yake ya nchini Marekani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Nandy ameweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Aslay wanatarajia kuungana na Hamisa Mobetto nchini Marekani.

Natarajia kusafiri siku ya tarehe 25 mwezi huu kuelekea Marekani kwa ajili yakufanya ziara nikiwa na msanii mwenzangu Aslay na Hamisa kisha nitarudi Bongo tarehe 10, Desemba tukiwa wote watatu, pia hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kufika huko kwa sababu sijawahi kwenda kabisa”.

Hamisa Mobetto amekuwepo nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi sasa ambapo ameonekana akiwa anafanya matamasha katika majimbo mbali mbali katik nchi hiyo.

“Nilijua Hamisa Atakuwa Staa Tangu Zamani”-Mama Mobetto

Mama mzazi wa mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa alijua mwanaye atakuwa maarufu tangu akiwa mdogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya Global Publishers, Mama Mobetto amesema kuwa mwanaye alionesha mapema atakuwa mtu fulani kutokana na jinsi alivyokuwa akijiweka na watu wengi walimwambia kuwa atakuwa mlimbwende.

Unajua Mobeto alikuwa akijipenda tangu mdogo na alikuwa na mambo f’lani ambayo niliamini akikua atakuwa mtu f’lani mwenye jina mjini”.

Lakini pia Mama huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona umaarufu wa mwanaye alijitahidi kumpa malezi mazuri na makini kwani alimlea peke yake bila kuwa na baba.

Mama huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya kuona umaarufu wa mwanaye alijitahidi kumpa malezi mazuri na makini kwani alimlea peke yake bila kuwa na baba”.

Mobetto anaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki kwani wimbo wake wa ‘Tunaendana umeendelea kukamata chati.

 

Hamisa Mobetto Awataka Mashabiki Zake Wake Wavumilivu

Mwanamitindo na msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuwataka mashabiki zake kumvumilia katika kipindi hiko ambacho yupo katika Mahaba mazito.

Hamisa Amezidi kukamata headlines kwenye mitandao ya kijamii tangu aliposafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki na kupata Mpenzi mpya anayejulikana Kama Josh Adeyeye.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Hamisa alisema kuwa anajua watu wengi wangependa kumuoana anarudi nyumbani sasa hivi wajue ni kitu gani kinaendelea lakini amewaomba watulie kila kitu ambacho wananakitarajia kutoka kwake watakiona.

Najua watu wengi mnataka kujua nikija nyumbani inakuwaje au mambo yangu yatakuaje mimi nimewaomba mtulie tuli mambo yataenda kama mnavyoniombea na yameshakuwa kabisa”.

Hamisa amezidi kufanya Vizuri Baada ya kuachia wimbo wake siku ya jana unaoitwa ‘Tunaendana’ ambao umeshika namba moja kwenye mtandao wa YouTube.

Mama Mobetto Atoa Masharti Mazito Kwa Mkwe Wake

Mama mzazi wa Msanii wa Bongo fleva na mwanamitindo Hamisa Mobetto, Shufaa Rutiginga maarufu kama Mama Mobetto ameibuka na kutoa masharti kwa Mpenzi wa mwanaye.

Mama Mobetto amefunguka hayo Baada ya picha kusambaa kwenye mitandaoni ya kijamii zilizomuonyesha Hamisa na Mpenzi Wake Josh Adeyeye nchini Marekani.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mama Mobetto alipoulizwa kuhusu picha hizo alisema, msimamo wake ni kwamba, hata kama picha hizo zinaonekana na yeye kuziona kwenye mitandao lakini bado anamtambua tu kama hawara.

Mama Mobeto alisema, kama kweli jamaa huyo anamhitaji mwanaye basi masharti anayompa ni kufika nyumbani kwanza nyumbani kwake kujitambulisha ili amjue vizuri yeye pamoja na ndugu zake.

Hivi jamani umeona wapi mzazi ambaye anajua maadili amuongelee hawara wa mtoto wake ambaye hajatambulika rasmi? Aje nyumbani, ajitambulishe, hapo sasa nitakuwa free kumuongelea, lakini habari za kwenye mitandao siwezi kuzizungumzia”.

Mobetto alimuanika Mpenzi Wake huyo siku chache zilizopita baada ya kuisha kwa mahusiano na aliyekuwa Mpenzi na baba mtoto Wake Diamond Platnumz.

Sister Fey Amfungukia Mazito Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kwenye mitandao ya kijamii Kama Sister Fey ameibuka na kumpa maneno mazito Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Sister Fey amemuibukia Hamisa na Kumpongeza kwa mambo mazuri anayofanya hivi sasa nchini Marekani ambapo anafanya shoo mbali mbali katika nini mbali mbali.

Sista Fey amemtaka kuwa jasiri na kutoangalia nyuma sasa kwani alipotoka ni mbali lakini alipofika hivi sasa ni mbali zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sista Fey ameandika maneno haya:

Uanawza ukatukanwa Sana na ukadhalilishwa sana ukapitia magunu mpaka ukajiuliza kwanini Mimi? ILA siku ni moja tu kila mmoja atashangaa hata maadui zako watajificha kukuangalia kimya kimya wakati wa Mungu ni wakati sahihi but Hamisa nakuomba na kukuombea usirudi nyuma ikiwezekana kweli chukua uraia huko na ikishindikana piga kazi haswa hakikisha unapata madili mengi ili uzidi kuwanyamazisha wabaya wako Misa dunia dura mama na sitamani kusikia utoto umekurudisha nyuma kwa uliyopitia jione una miaka 40 wewe ni mrembo”.

 

Hamisa tangu ameachana na Diamond na kuelekeza nguvu zake kwenye kupiga kazi ameonekana kufanya vizuri na kufika mbali zaidi.