Florah Afunguka Baada Ya H.Baba Kukiri Kumiss Uwoya

Msanii wa filamu za Bongo movie, Florah Mvungj amefunguka Baada ya mume Wake ambaye ni Msanii wa Bongo fleva H. Baba kukiri kumiss Ex Wake Irene Uwoya.

Siku chache zilizopita H-Baba kupitia  ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya Irene Uwoya kisha kuandika kuwa amemmisi, jambo lililowashangaza wengi kwani siku za nyuma kidogo aliwahi kumponda na kusema haoni ndani kwa mke Wake Flora.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Florah Mvungi amedai haoni tatizo kwa Mume Wake kumkumbuka Aliyekuwa Mpenzi Wake isitoshe amedai yeye hana wivu.

Watu wanakuza mambo sana, mbona ni hali ya kawaida sana, ni kumbukumbu tu ambazo mtu zinamrudia, anafanya anachojisikia, ameona ni vyema kushea kumbukumbu zake na watu kwenye mitandao, sijaona shida yoyote na wala sijahisi wivu“.

 

Mtoto Wa H.Baba na Flora Mvungi Apata Dili Nono

Muigizaji wa Bongo movie, Florah Mvungi na mume wake muimbaji wa bongo fleva wamejikuta wakichekelea baada ya binti yao Tanzanite kukwaa dili nono na kampuni ya Vodacom.

Florah na H.Baba wamezidi kupata umaarufu baada ya kuamua kuwapa watoto wao wawili majina ya kizalendo kupitiliza kwani mtoto wao wa kike anaitwa Tanzanite na mtoto wao wa kiume wamemuita Africa. Inavyoelekea majina hayo ya kizalendo yamekuja na baraka kwani binti yao Tanzanite mwenye miaka mitano amefanikwa kulamba dili nono la kampuni ya simu za mikononi Vodacm ambapo hivi karibuni ataanza kuonekana katika matangazo ya Vodacom.

Florah alipofanya mahojiano na global tv alifunguka yafuatayo kuhusiana na dili hilo nono kabisa:

Tanzanite kiukweli yupo shule kwa sasa hapo mwanzo alikuwa anahitajika kwenye matangazo mengi mengi kama uliona alikuwa balozi wa EBM Signature ambaye yupo Marekani lakini baadae nikaona aende kwanza shule nikasitisha kazi zote alizokuwa nazo lakini hivi karibuni nilipigiwa simu na Vodacom kuwa wanamhitaji kwaajili ya matangazo yao wakaomba picha zake na video clips za majaribio basi wakampenda kwaiyo hivi karibuni ataanza kuonekana kwenye matangazo ya vodacom. kampuni ambazo amewahi kufanya nazo kazi pamoja na EBM Signature, Kids fashion,pia amefanya matangazo ya biskuti na nyinginezo na sasa hili la Vodacom. Kuhusu malipo ni kwamba hawezi akafanya kazi ya chini ya milioni tatu yaani kiasi cha chini wanachomlipaga ni milioni tatu, unajua Tanzanite tangu mdogo tumemtengeneza kama brand kwaiyo hatuwezi kuchukua matangazo yoyote yanayokuja huwa tunaangalia na umaarufu wa kampuni ili aweze kufika mbali sana”.

Florah pia alikiri kuwa wanajitahidi kumuacha mtoto akue kama watoto wengine ndio maana kwa sasa wamempunguzia kazi na wanamuacha asome shule kwanza.