Ujumbe wa Gabo kwa Diamond na Wasanii Kuelekea Wasafi Festival

Msanii wa bongo movies, gabo zigamba amefunguka na kuandika ujumbe kwa wasanii wanaoenda kufanya show katika tamasha la Wasafi festival kuwa tamasha hilo linaonekana kuwa la kisasa sana hivyo na wao pia inawabidi kufanya mazoezi kwa muda mrefu na umakini ili kuweza kuwahudumia vizuri mashabiki wao.

Gabo pia anasema kuwa Diamond ni mkombozi wa wasanii na muda wa kufanikisha hayo ndio sasa ingawa wapo watu watakaofanya figisu ili kuweza kudidimiza jitihada zake lakini hapaswi kujali hayo zaidi ya kuangalia kile anachotaka kukifanikisha.

binafsi ninajua kuwa wazo lako ni zuri kulio wazo lenyewe, lakini pia ninaamini kuwa upande wa bongo fleva’ Freedom is coming tommorrow‘, ila wapo watwana watakaovijika uungwana  ili wanyanganye kidogo chetu twana na kusema kuwa lengo halisafishi njia…hao ni wapuuzi tena wakupuuzwa na kushindwa zao dhamiri,  wasiweze kusimama.pasi na shaka stage ni ya kisasa  basi pls wasanii mfanye mazoezi ya kukonga nyogo za mashabiki  zenu maana kuimba ni swala jingine na show ni swala jingine.

Tamsha hilo linatarajiwa kuanza november 24 mwaka huu na kuanzia mkoa wa mtwara ambapo wasanii wa WCB pamoaja na wasanii wengine watapata nafasi ya kukutana na kufurahia pamoja na mashabiki wao.

Vanessa Mdee na Gabo Waunga Mkono Harakati Za BASATA

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa Vanessa Mdee na Muigizaji bora wa Kiume wa Bongo movie Gabo Zigamba wameonekana kuunga mkono harakati za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Wiki iliyopita BASATA ilitangaza sheria mpya kwa wasanii wote Tanzania kuwa wanaenda kujisajili BASATA mara tu wanaenda Safari za nje ya nchi Kwenye shoo mbali mbali.

Vanessa Mdee na Gabo wameonekana kuwa mstari wa mbele kuinga mkono na kutoonekana sheria hiyo kwani wameenda kuomba kibali kw ajili ya kusafiri nje ya nchi kwa kazi zao za sanaa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Onesmo Kayanda amesema Vanessa Mdee ameshapatiwa kibali kaenda Afrika Kusini huku Gabo akipata kibali cha kwenda nchini Ireland.

Wii iliyopita Diamond Platnumz alizuiliwa kusafiri akiwa uwanja wa ndege baada ya kukiuka sheria hiyo na kutaka kusafiri bila kibali.

Gabo Amefanikiwa Kuziba Pengo La Kanumba- Mama Kanumba

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amemtaja msanii ambaye anaamini ameziba pengo la Kanumba Kwenye tasnia ya Bongo movie.

Mama Kanumba ambaye naye aliingia Kwenye Bongo Movie mara baada ya mwanaye kufa amemtaja Gabo Zigamba kama Msanii ambaye ameziba pengo la Kanumba.

Kwenye mahojiano  na Wasafi TV, Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.

Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi.”

Lakini pia Mama Kanumba amelinganisha uwezo wa Kanumba na Gabo:

Ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza”.

Gabo Ashinda Tuzo Nyingine Zanzibar

Muigizaji wa Bongo movie Gabo Zigamba  ametunukiwa tuzo ya ushindi katika kipengele cha muigizaji bora wa kiume kupitia filamu aliyoigiza ya ‘SUMU’ kwenye tamasha la ZIFF lililofanyika visiwani Zanzibar.

Kwenye mahojiano na tovuti ya East Africa Gabo ameweka wazi juu ya hatua zinazofanyika mpaka yeye kushinda tuzo hiyo licha ya filamu kuwa haijaangaliwa na watazamaji wengi na kusema hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa majaji duniani kote kupitisha filamu ambayo haijatazamwa na mashabiki.

Tuzo zilivyo duniani zipo za aina mbili, zile za ‘Choice Awards’ kwa maana ya tuzo zinazopatikana kwa Kura za mashabiki kwa filamu walizoziona, na kuna tuzo zinazotolewa kwa kufanyiwa ‘judgement’ na watengenezaji filamu ambazo huchujwa hata kabla watazamaji hawajaziona kwa mara ya kwanza kwenye ‘Movie Premiers’. Mfumo huo hutumika duniani kote na ndio tuzo yenye hela sana na kubwa duniani ukiachana na tuzo zinazopatikana kwa kura za mashabiki, sababu kura wanazopiga mashabiki ni kipimo cha kujua watu wanakupenda kias gani”.

Gabo amezidi kuibuka kidedea baada ya kushinda tuzo ya Muigizaji bora wa kiume mapema mwaka huu.