Hii ndio sababu Barnaba hataki kufanishwa na mtu yeyote

Msanii wa Bongo Fleva, Barnaba amesema kuwa hakuna msanii yeyote Bongo anayeweza kufananishwa naye kwa sababu yeye anauelewa muziki ambao anaoufanya.

Akizungumza na Mikito Nusunusu , Barnaba alisema kuwa kipaji chake amekitoa kwa mungu na anamshukuru Mungu kwa kumjalia kipaji cha kipekee kwenye muziki na kwamba ataendelea kukitendea haki. Alisema;

“Mimi ni mwanamuziki na si msanii, lazima kwanza utofautishe mambo hayo mawili, ndiyo maana ninaweza kutunga na kuimba na hata kutumia vyombo vyote vya muziki, hiyo ndiyo maana halisi ya mwanamuziki. Naomba sana nisifananishwe na mtu kwenye eneo hilo. Nilizaliwa kuburudisha watu na ninafanya muziki kama sehemu ya maisha yangu, siangalii fedha na masilahi, muziki uko kwenye damu,”