Ruby afunguka baada ya kudaiwa kuwa ujauzito wake ni wa Alikiba

Mwanamziki wa bongo Ruby anadaiwa kuwa na mimba ya Alikiba, hata hivyo hakuna aliye na uhakika wala dhibitisho tosha kuhusu uvumi huu.

Akizungumza na Bongo 5 hivi karibuni Ruby alikiri kuwa amesikia maneno Hata, lakini kulingana na yeye huu ni uvumi usio na ukweli wowote.

Ruby aonyesha mimba yake

Ruby aliendelea kuongeza kwa Sasa amezoea kusikia watu wakidai kuwa yeye ni mpenzi wa Kiba, lakini hana la kusema kwa sababu uhusiano wake na Kiba ni wa urafiki tu.

Tazama mahojiano yake na Bongo 5 hapa;

Ruby amuonyesha mpenzi wake ambaye ni baba ya mtoto anayemtarajia (Picha)

Mrembo na Msanii wa nyimbo za bongo Ruby anamtarajia mtoto wake wa kwanza kulingana na picha ambazo zinaenea mitandaoni.

Ruby aonyesha ujauzito wake

Ruby anaonekana kuwa yuko mjamzito na baada ya kuachia nyimbo kadhaa, mrembo huyu ameamua kuanza familia yake na mpenzi wake aliyemuonyesha kupitia mtandao wake Wa Instagram.

Staa huyo aliamuanika kwa kuiweka picha yake huku akimwandikia ujumbe uliodhibitisha kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wao atakaye zaliwa hivi karibuni. Ruby aliandika kusema;

“My prince charm, my smile maker, Baba princess Ruby”

Tazama picha hapa chini;

Mpenzi wa Ruby