Wolper Alizwa na Vifo Vya Watoto Njombe

Mastaa mbali mbali wamejitokeza kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya Watoto ambayo yanaendelea mkoani Njombe Hivi sasa.

Kwa Wiki karibuni chache sasa kumekuwa na mauaji makubwa ambayo yanafanyika katika vijiji vya mkoa wa Njombe ambapo Watoto wamekuwa wakiuliwa kikatili kwa kuchinjwa.

Msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo hivyo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno haya:

Jesus eti Nini kina endelea sijaelewa ? Hii ni Tanzania Then why ?‍♀️How? Coment This kwa wanaojua Na poleni Wote“.

Lakini pia Haji Manara amekemea pia kitendo gaucho ambapo ameandika:

Tupaze sauti zetu wote kukemea dhulma hii!! Watoto wanayo haki ya kuishi,haki ya kusoma na wanayo haki ya kucheza na kufurahi! Why wauawawe ? Ndugu zangu hili ni jukumu letu sote kuwalinda watoto wetu,kulilinda Taifa letu la baadae,tusikubali udhalimu huu,na tuseme NO!! Inaumiza sana kuona yupo Mtanzania anafanya ukatili huu kisa ni imani potofu za kishirikina!!
Khofu ya Mungu ipo wapi? Ohhh Watoto wetu nn kosa lao? Au kuzaliwa watanzania? ! Mwenyezi Mungu kwako tunakukabidhi wauaji hawa waliolaanika
.”

 

Nampenda Sana Jokate, Mtu Akimsema Naumia-Haji Manara

Mkuu wa utohaji habari katika club ya Simba Haji Manara amefunguka na kusema kuwa anampeda sana Jokate Mwegelo kwa sababu ni msaichana anasikia, kujali na kutoa ushauri kwa wengine.Haji manara anasema kuwa katika wanawake maarufu wa bongo anavutiwa zaidi na Jokate kuliko haa Wema sepetu.

mimi ni shabiki sana wa Jokate, nampenda sana lakini sio kimapenzi niweke wazi , ni rafiki yangu na katika wasichana maarufu bongo nampenda sana Jokate , naumia sana wakimsema Jokate alafu ni mwanamke ambae anasikiliza hata ukimshauri unakuwa unasikia raha.

Kuhusu kauli yake ya kumuoa wema sepetu haji mamanra ansema kuwa huo ulikuwa ni utani katika mpira ili kusisitiza kubadilishwa kwa ratiba ya Ligi kuu Tanzania Bara.Na hiyo yote kwa sababu Wema sepeyu ni msichana mrembo na mwenye nguvu kubwa ya ushawishi anweza kutumika katika matukio makubwa nchini.