Wolper Afunguka Kuwaingilia Harmonize na Sarah Tena

Mbunifu wa Mavazi na Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper ameibuka na kujibu Tuhuma Za kuingilia tena mahusiano ya aliyekuwa Mpenzi Wake Harmonize na Mpenzi Wake Mpya Sarah.

Sakata hilo lilijitokeza siku chache zilizopita baada ya Wolper alionekana kuuimba katika akaunti yake ya instagram wa mapensi mabaya akimaanisha ‘mapenzi mabaya’ na yeye kubadilisha na kuimba kinyume.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wolper alisema kuwa amejisikia tu kuimba kinyume kuwa mapensi mazuri.

Lakini watu wanazungumza vingine kwamba namchokoza lakini isivyo hivyo. Nimejisikia tu kuimba haijalishi yeye ndiye ameanza kuimba lakini mimi nikaona niimbe kinyume na yeye alivyoimba ni vile nimejisikia tu kufanya hivyo”.

Baada ya video ile kusambaa watu wengi walichukulia kuwa Wolper amefanya vile ili kumsanifu Sarah hasa kwa sababu wawili hao hawaivi kabisa.

 

Wolper Afanya Maamuzi Magumu Ya Kuuza Gari Lake

Mbunifu wa mavazi na Muigizaji wa Bongo movie  Jacqueline Massawe maarufu kama Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa Hivi karibuni alifikia uamuzi wa kuuza gari lake.

Wolper ambaye alikuwa anamiliki gari aina ya Toyota Brevis, ameweka wazi kuwa ameamua kuuza gari lake hilo ambalo lilikuwa ndio Usafiri wake pekee ili anunue matirio za kutengenezea magauni.

Katika mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Global Publishers, Wolper ameweka wazi kuwa aliamua kuchukua uamuzi wake huo baada ya kupendezwa na matirio hayo alipokuwa nchini Dubai hivi karibuni.

Unajua mimi ni fundi cherehani hivyo  nilivyofika nchini Dubai na kuwaona wadada wakipendeza kwa kuvaa magauni kama haya na nilipowaangalia niliona kabisa kuwa nayamudu kuyadizaini.

Nilichoamua kufanya ni kuuza gari yangu na kwenda kununua matirio haya na kutengeneza magauni kadhaa ambayo kama hili na mengine nayauza. Kwa sasa natumia usafiri wa kukodi na hilo kwangu sioni shida”.

 

Wolper Alizwa na Vifo Vya Watoto Njombe

Mastaa mbali mbali wamejitokeza kukemea vitendo vya mauaji dhidi ya Watoto ambayo yanaendelea mkoani Njombe Hivi sasa.

Kwa Wiki karibuni chache sasa kumekuwa na mauaji makubwa ambayo yanafanyika katika vijiji vya mkoa wa Njombe ambapo Watoto wamekuwa wakiuliwa kikatili kwa kuchinjwa.

Msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo hivyo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno haya:

Jesus eti Nini kina endelea sijaelewa ? Hii ni Tanzania Then why ?‍♀️How? Coment This kwa wanaojua Na poleni Wote“.

Lakini pia Haji Manara amekemea pia kitendo gaucho ambapo ameandika:

Tupaze sauti zetu wote kukemea dhulma hii!! Watoto wanayo haki ya kuishi,haki ya kusoma na wanayo haki ya kucheza na kufurahi! Why wauawawe ? Ndugu zangu hili ni jukumu letu sote kuwalinda watoto wetu,kulilinda Taifa letu la baadae,tusikubali udhalimu huu,na tuseme NO!! Inaumiza sana kuona yupo Mtanzania anafanya ukatili huu kisa ni imani potofu za kishirikina!!
Khofu ya Mungu ipo wapi? Ohhh Watoto wetu nn kosa lao? Au kuzaliwa watanzania? ! Mwenyezi Mungu kwako tunakukabidhi wauaji hawa waliolaanika
.”

 

Wolper Adaiwa Kumkuwadia Dogo Janja Kwa Demu Mpya

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper ameibuka na kukana kabisa taarifa zinazodai kuwa amemsaliti rafiki yake Irene Uwoya kwa kumkuwadia shoga yake kwa Dogo Janja.

Dogo Janja ana ‘kifaa’ kingine kipya ambaye ni mtoto mkali, mkazi wa jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Linna. Baada ya kusambaa kwa video na picha za Dogo Janja ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Linna wakiwa kwenye mahaba mazito ndipo baadhi ya watu wakaibuka na kila mmoja kuanza kusema lake.

Dogo Janja na Mpenzi Wake Linah

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa kwa sasa uhusiano wa Uwoya na Wolper hauko sawa. Kufuatia bango hilo kuwa na madai mazito ya Uwoya kupaniki huku Wolper akitajwatajwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wolper alifunguka na kusema haya:

Kikubwa ninafurahi kwa sababu baada ya kupelekewa hiyo ishu, Irene (Uwoya) hakutaka kuamini kwani ananijua jinsi ninavyompenda na kumchukulia. Anajua siwezi kuwa snichi kwake kwani ninamchukulia kama ndugu yangu. “So hata alivyoambiwa alikuwa ndiye mtu wa kwanza kukataa mimi kufanya hivyo.

Anajua mimi siwezi unafiki ndiyo maana hujawahi kuona nikimposti Dogo Janja (kwenye ukurasa wake wa Instagram) na huyo demu ambaye ni mdogo wangu (Linna) maana nitakuwa mchawi. Yaani mchawi kabisa.

Na mimi ninamlaumu Dogo Janja maana Dogo Janja hajui undugu wangu na Linna kwa hiyo ninahisi alitumia uanaume wake kuni-block (mtandaoni). “Mpaka hapa ninakuambia huyo mdogo wangu, Linna siyo mteja wangu tena na hana tena ukaribu na mimi tangu awe na Dogo Janja.

Sasa nikisema Dogo Janja mchawi nitakuwa mwongo? Mchawi ni mtu mharibifu. “Nilishangaa sana kusikia eti mimi ndiye nimemkuwadia wakati Dogo Janja nilikuwa ninamchukulia kama mwanangu na alikuwa shemeji yangu (kwa Uwoya). “Hiyo skendo ndiyo imenifanya niwakalie kimya Linna na Dogo Janja maana Dogo Janja alikuwa rafiki yangu kabla hata ya kuwa na Irene (Uwoya) na huyo aliyenaye ambaye ni mdogo wangu kabisa.

Kinachoniuma sana ni huo uvumi ulivyotokea maana nilimuuliza huyo mdogo wangu (Linna) na Dogo Janja wakakataa katakata na meseji zao ninazo alafu eti leo hii ninaonekana…. (tusi) wakati Irene (Uwoya) ni rafiki yangu na ni mfanyakazi mwenzangu“.

 

 

Jacqueline Wolper- Natamani Kupata Mtoto

Staa katika tasnia ya Bongo movie na mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper ameibuka na kusema katika vitu anatamani mwaka huu ni kupata mtoto  wake  wa kwanza.

Wolper ambaye amethibitisha kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye amesisitiza kuwa  hataweza kumuweka hadharani Lakini amesema huu mwaka anatamani kupata mtoto bila kujali kama itakuwa ndani ya ndoa au nje.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, Wolper alisema anaamini mwaka huu kwake utakuwa na neema kubwa, ikiwemo kujaaliwa mtoto kama ambavyo amekuwa akitamani iwe hivyo.

Nina mipango mingi sana kwa mwaka huu, unajua kila unapoweka mikakati yako mwanzoni mwa mwaka ndio nafasi nzuri ya kufanya mambo yako kwa umakini zaidi, kwa sasa ninachowaza ni mtoto”.

Wolper ambaye amewahi kuwa muwazi sana kwenye Suala la mahusiano katika siku za nyuma amesema hawezi kufanya hivyo kwa sasa kwani Mitandao ndio iliyoua mahusiano hapo nyuma.

Wolper Akumbwa na Fedheha Ya Aina Yake Mwanza

Muigizaji wa Bongo movie na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amejikuta akipata fedheha ya aina yake Baada ya kula mweleka wa nguvu mbele za watu.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mbwembwe zilizmponza Wolper kwenye ukumbi uliopo katika Ufukwe wa Jembe ni Jembe jijini Mwanza ambapo Lebo ya WCB  chini ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platinum’ au ‘Mondi’ ilikuwa ikifanya pati ya awali (pre-party) ya onesho lao la Wasafi Festival lililofanyika katika Uwanja wa CCM-Kirumba, juzi.

Katika tukio hilo, wakati watu wakipata kilaji, mastaa ambao walitarajiwa kufanya makamuzi kesho yake kwenye Wasafi Festival walikuwa wakitambulishwa. Ulipofika wakati wa Wolper, yeye aliamua kupanda juu ya meza kama wafanyavyo wanenguaji wa staili ya kusasambua. Akiwa juu ya meza, DJ aliweka Wimbo wa Kwangwaru ambapo Wolper aliendelea kuonesha umahiri wa kukicheza kwa kukata mauno baab’kubwa. Kwa bahati mbaya, wakati akiendelea kufanya yake, maskini mwanadada huyo mrembo alipiga mwereka matata na kuangukia kisogoni.

Hata hivyo, alisaidiwa kunyanyuka na mabaunsa na mashabiki waliokuwa karibu ambao walimuinua kisha wakamkagua na kubaini hakupata maumivu makali hivyo shoo yake ikaishia hapo. Baada ya kushuhudia tukio hilo, baadhi ya mashabiki walisikika wakisema, eti huenda mambo yaliyompata Mondi kule Sumbawanga yalitaka kujirudia kupitia kwa Wolper.

Source- Ijumaa Wikienda

“Siwezi Kurudiana na Mkongo Tena”- Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi tena kurudiana na aliyekuwa Mpenzi Wake anayejulikana Kama Putin maarufu kama Mkongo.

Tetesi za Wolper kurudiana na aliyekuwa mchumba Wake zilisambaa Wiki iliyopita Kupitia mitandao ya kijamii Baada ya Wolper kumposti katika ukurasa Wake wa Instagram.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wolper alisema kuna watu wamekuwa wakivumisha kwamba amerudisha mapenzi kwa Mkongo huyo kwa sababu tu wanapostiana picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, lakini hiyo siyo sababu ya kurudisha penzi lao la nyuma bali wanafanya hivyo kimazoea tu.

Watu wanaonijua vizuri wanafahamu, siwezi kurudia matapishi yangu hata siku moja. Huyo Putin tumekuwa kama washikaji tuliozoeana, lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi kuwa wapenzi tena”.

Wolper na Putin walikuwa kwenye mahusiano kwa muda mwaka mmoja ambapo walifikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba, lakini waliachana baada ya mwanaume huyo kugundulika kuwa ana mwanamke mwingine nchini kwao.

Lynn Afungukia Mapenzi Yake Kwa Jacqueline Wolper

Video Vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Louis maarufu kama Lynn amefunguka na kuweka wazi kuwa anamkubali sana mwanadada mkali wa fasheni Jacqueline Wolper.

Lynn alifunguka hayo Baada ya kuulizwa sababu iliyomfanya Mpaka awe namfuatilia Msanii mmoja tu Bongo kupitia ukurasa wake wa Instagram na sio wasanii wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari nchini, Lynn ameweka wazi kuwa sababu ya kwanza ni kuwa anamkubali sana Wolper na pili ndio mtu ambaye kibongo bongo anaendana naye:

Mimi naona toka tujuane tunakuwa tupo sawa tu kishikaji tunaongea, kwa hiyo yeye kama kuna kitu tumefanana ndio maana tumekuwa hivyo. Nahisi damu zetu zimeendana, labda wengine watakuja”.

Siku chache zilizopita  Jacqueline Wolper alifabya bonge la party kwa ajili ya kusherehekea miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, Mwanadada huyo ( Lynn) ni miongoni watu waliojumuika.

Jacqueline Wolper Ashabikia Mapenzi Ya Harmonize na Sarah

Muigizaji wa Bongo movie na mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper ameshangaza wengi Baada ya kuonekana akiwa anashabikia Penzi la hasimu Wake Sarah na Harmonize.

Wiki iliyopita kuna tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Harmonize na Wolper wamerudiana Baada ya kuonekana wakiwa karibu katika tamasha zima la Wasafi Festival.

Lakini Harmonize na mpenzi Wake Sarah walionekana kuzima tetesi hizo Baada ya kuposti video iliyowaonyesha wawili hao wakiwa wanacheza pamoja na kukumbatiana kwenye nyumba yao.

Siku ya jana ilikuwa ni siku ye kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Wolper ambaye alifanya party yake kubwa na kualika wasanii wakubwa lakini cha kushangaza aliwaalika Harmonize na Sarah pia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wolper aliposti video ya Harmonize na Wolper na kuisindikiza na maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BrDmRCCnUsh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ijbkt2241p33

Katika kuonyesha kuwa Harmonize na yeye Hana tatizo na Wolper alimposti katika ukurasa wake wa Instagram na kumtakia Birthday njema.

Wolper Ajitapa Kuwekewa Ulinzi Mzito na Mpenzi Wake

Msanii wa Bongo movie na mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hivi sasa amewekewa ulinzi mkali na Mpenzi Wake kwa sababu ya usalama wake binafsi.

Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa ulinzi mkubwa ambao amewekewa unatokana na Tamasha la Wasafi Festival ambalo anaendelea kushiriki hivyo kila mkoa amewekewa Bodyguard kwa kila mkoa ambao ataenda.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa  Dizzim Online Wolper amesema kuwa Mpenzi wake huyo sio mtu wa camera hivyo hawezi kuonekana .

Actually Mr wangu kila mkoa ameniwekea Body Guard na dereva kwahiyo ulimuona Body guard wangu , lakini sio mtu wa camera kwahiyo hawezi kuonekana.

Unajua mikoa tuna wapenzi wengi mtu anaweza akakuhug kama vile kwa Diamond wakachukua cheni, kwahiyo hiyo ndio sababu kubwa kwahiyo sio kwamba unakuja na Body guard kwasababu gani nafikiri hiyo ndio sababu kuu, tunawapenda mashabiki zetu hatutaki kuwakosea“.

Jacqueline ni mmoja kati ya wasanii ambao wameonekana kushiriki katika matamasha yote ya Wasafi Festival katika mikoa mbali mbali.

 

 

“Sarah Hajakasirika Nilivyokumbatiwa na Wolper”- Harmonize

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika label ya WCB Harmonize ameibuka na kudai kwamba Mpenzi Wake Sarah hajamind kitendo cha yeye kukumbatiana na Ex Wake Wolper.

Wikiend iliyopita mkoani Mtwara kwenye tamasha la Wasafi Festival Harmonize alirekodiwa akikumbatiana na Ex Wake Wolper wakati wa kusalimiana mara moja tetesi zilianza kusambaa kwamba wawili hao wamerudiana.

Tetesi hizo zilizimwa na Mpenzi wa Harmonize, Sarah ambaye Kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema yeye na Harmonize hawajaachana na hawategemei kuachana na muda si mrefu angejiunga naye Mtwara kwa ajili ya shoo hiyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Harmonize alisisitiza yeye na Wolper ni washkaji tu na wapo kikazi ila Mpenzi Wake ni Sarah na hajamind alivyoona video za wawili hao kukumbatiana:

Wolper ni mtu wangu wa karibu na nilifurahi  kumuona akishiriki tena na Wasafi na kuhusu Sarah najua hawezi kumaindi kwani anaelewa kuwa tupo Mtwara kikazi zaidi”.

Fashion Ya Gauni Yampa Wakati Mgumu Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mbunifu wa mitindo Jacqueline Wolper alijikuta katika wakati mgumu baada ya Gauni alilovaa katika shughuli hivi karibuni kumletea kero.

Global Publishers wanaripoti kuwa tukio lilitokea Wikiend iliyopita katika ukumbi wa Club Next Door Arena, Dar ambapo Wolper alivalia gauni lililomwacha wazi sehemu kubwa ya kifua hivyo kila alipokuwa akiendelea na burudani alikuwa akikosa raha kutokana na sehemu ya matiti kutoka nje kwani kila alipoweka sawa baada ya muda hali ilijirudia ileile.

Baada ya sakata hilo kuendelea kwa muda mrefu Mwanahabari alimuuliza sababu ya kubuni fasheni hiyo ya gauni iliyoonekana kumnyima raha lakini alishindwa kutoa jibu lolote na kusema ana haraka hivyo aachwe akapumzike.

Wolper ambaye anasifika kwa kubuni na kushona mavazi yake anayovaa mwenyewe na hata kuuza katika boutique yake ya Wolper house of stylish, amedaiwa kukosea safari hii.

 

Lord Eyes Afungukia Skendo Ya Mapenzi na Wolper

Msanii mkongwe wa muziki wa hop hop nchini kupokea katika kinda la Weusi Lord Eyes amefungukia tetesi zinazotrend kuwa Ana mahusiano na staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.

Kwa muda mfupi sasa kumekuwa na tetesi kuwa Lord Eyes na Wolper wamekuwa kwenye mahusiano hi ilitokana na picha kadhaa zilizowaonyesha wasanii hao pamoja.

Wiki iliyopita kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Wolper alikataa tetesi hizo Lakini pia aliweka hao tatizo Kama ikitokea hivyo:

Unajua hata mimi ambaye naambiwa natoka naye nimeona kwenye mitandao tu lakini pia siku ikitokea, freshi tu.Sio mwanaume mbaya maana ana sifa zote za mwanaume ninayempenda au wamesema hivyo kwa sababu niliimba wimbo wake nikauposti mtandaoni ndio tatizo basi ngoja tuone itakavyokuwa maana Wabongo wape picha tu maneno wataweka wenyewe”.

Lakini pia Lord Eyes amefungukia tetesi hizo kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv na kusema habari hizo hazina Ukweli wowote:

Wolper ni radioing yangu tu na unajua maana ya rafiki ni mtu anayeweza kukusitiri na ndoto unamuita rafiki wa kweli”.

 

Wolper- Sioni Tatizo Kutoka na Lord Eyes

Mbunifu wa mavazi na muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hana uhusiano na msanii mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Waziri Makuto maarufu kama Lord Eyes.

Kumekuwa na tetesi zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Lord Eyes wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini Wolper amefungukia madai hayo na kusema kuwa hayana ukweli wowote.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wolper  alisema yeye ameona kwenye mitandao taarifa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Lord lakini pia hata siku ikitokea ikawa hivyo sio mbaya kwani sio mwanaume mbaya kwake na pia anavutiwa na jinsi alivyo.

Unajua hata mimi ambaye naambiwa natoka naye nimeona kwenye mitandao tu lakini pia siku ikitokea, freshi tu.Sio mwanaume mbaya maana ana sifa zote za mwanaume ninayempenda au wamesema hivyo kwa sababu niliimba wimbo wake nikauposti mtandaoni ndio tatizo basi ngoja tuone itakavyokuwa maana Wabongo wape picha tu maneno wataweka mwenyewe.” 

 

 

Mbasha Apangua Tetesi Za Kupombeka na Wolper

Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha ameibuka na kupanguia tetesi zote zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba mtumishi huyo wa Mungu alikuwa amekaa na msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper wakinywa pombe.

Kwenye interview aliyofanya na kituo kimoja habari, Mbasha amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa alikuwa anakunywa soda. Mbasha amesema watu wamemjia juu kwa kukaa karibu na Wolper na kusema akiendelea kukaa karibu na  Wolper atampoteza na pengine anaweza akafanya mambo ambayo hayaendani na wokovu wake kama watu walivyomzoea kwamba yeye ni mtu wa dini.

Mimi na Wolper ni marafiki wa karibu na ukweli ni kwamba mimi nampenda Wolper kama dada yangu na namkubali kwa kazi zake anazozifanya hata hivyo naamini kwamba na yeye ananipenda kwa kuwa tumekuwa karibu kwa muda mrefu sasa”.

Lakini pia Mbasha alimalizia huku akitolea maelezo picha ambazo zimesambaa mitandano zikimuonyesha akiwa karibu na Wolper na kusema kwamba picha hizo zilitokana na kazi ambayo waliipata kwa pamoja ikawakutanisha na kuwaweka karibu.

 

 

Jacqueline Wolper Ahaidi Kupambana na Marafiki Wanafki

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper ametoa neno kwa marafiki wote ambao wamekuwa na tabia za kinafki na kuhaidi kupambana nao.

Wolper amefunguka na kudai siku akimkamata mtu ambaye wanafahamiana vizuri akiwa anamsema kwenye Mtandao wa Instagram atafurahia shoo kwa atakachomfanya.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Wolper kama mtu mnajuana na ukaona amekosea ni vyema ukamfuata mwenyewe na kumwambia kuliko kuandika unavyotaka Instagram kwani huo ni unafiki.

Siamini kabisa mtu mwenye mapenzi ya dhati na wewe anaweza kukuandikia ujumbe kwenye Instagram. Mimi huo ninauita unafiki na siku nikimkamata mtu wa aina hiyo atanijua“.

Siku chache zilizopita Wolper aliingia kwenye mgogoro na msanii mwenzake Esha Buheti baada ya kuamua kumsema Wema Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo Wolper alidai hajapenda na kumtaka Esha amfuate pembeni na kumsema Wema badala ya kumsema Instagram.