Juma Jux Kucheza Filamu Ndani Ya Bongo Movie

Msanii wa muziki wa Bongo fleva songwritter Juma Mussa maarufu kama Juma Jux ametangaza kucheza filamu yake ya kwanza ndani ya Bongo Movie.

Habari hiyo njema imedokezwa kwa mara ya kwanza Director wa video hapa nchini ikiwemo video nyingi za Jux Hanscana ameweka wazi kuwa hivi karibuni wawili hao wanampango wa kuja na movie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Hanscana ameweka wazi kuhusu Ujio wa filamu hiyo Lakini pia ameweka wazi kuwa Jux alitaka  kufanya siri iwe suprise kwa mashabiki zake.

Jux amekuwa na mchango mkubwa sana Kwenye ukuaji wa Hanscana Brand, alikuwa na uwezi wa kushoot na mtu yoyote yule projects zake lakini akaona Noo why hii riziki nisimpe huyu kijana mwenzangu ili naye asaidie familia yake na vijana wenzake pia.

Shukrani sana Jux mimi nitaendelea kuhakikisha projects zakowsikuangushi bro…Also na movie yetu japo unataka ije kimya kimya lakini natoboa tu kwani kesi bei gani? Movie coming soon..”.

 

Hanscana Amtetea Darasa, Asema Maneno ya Mashabiki Yanam-panikisha Darasa

Muandaaji wa video bongo Hanscana amefunguka na kumtetea Darasa kwa kuzingatia kuwa yeye ni moja ya watu wa karibu sana na msanii huyo na alikuwa nae kwa kipindi chote ambacho aliweza kufanya nae ngoma za huko nyuma ambazo zilifanya vizuri sana,

Akiongea na Shadee wa Clouds E ,Hanscana anasema kuwa ni kawaida kwa wasanii kukaa kimya kwa muda ili kujipanga na sio Darasa tu ambae amekaa kimya bila kutoa ngoma mpya lakini kwa nini watu wamekuwa wakimkomalia sana Darasa.

Akitolea mfano wa wasanii wengine kama Bob Junior, hanscana ansema kuwa wapo wengi wamekaa kimya lakini hiyo inakuwa ni umauzi wa mtu kujipanaga ili kurudi upya hivyo watu wasihofie swala la Darasa kukaa kimya.

Hanscana anasema kwa jinsia mbayo mashabiki wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii kuhusu Darasa , kama msanii huyo asingekuwa jasiri basi angekuwa amesha-panic sana na hata kuamua kuwaridhisha mashabiki kwa kutoa ngoma mpya lakini kwa kukurupuka kitu ambacho baadae wangesema tena ameharibu.

HLlakini pia , hanscana anasema kuwa anachoamini ni kwamba mashabiki wanampenda sana Darasa na ndio maana wamekuwa wakimsumbua yeye sana na wala sio wasanii wengine lakini pia Darasa kwa sasa anapaswa kuwa imara sana ili kuosikiliza maneno ya mashabiki na kujikuta anakurupuka na kutoa ngoma bila kujipanga vizuri.

Maneno ya Hanscana yanakuja baada ya watu wengi kusema kuwa msanii Darasa amekuwa kimya sana na wanahisi kuwa msanii huyo anaweza kuwa na matatzo au ameharibikiwa kabisa na kwamba amefulia hawezi kufanya tena kama mwanzo,hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Hanscana kuongea hayo kuhusu Darasa huku akisema kuwa msanii huo anajipanga ili kutoa kivingine tena.

Hanscana Azungumzia Kupotea Kwa Darasa.

Ni mwaka sasa unaelekea kuisha tangu msanii Darasa kutoa wimbo wake wa hasara roho ambao ndio ulimfanya akwa kimya katika tsania ingawa alipokuja mashabiki walijua ndio amekuwa kufunika katika muziki.Wengi wamekuwa wakihoji na kujiuliza yuko wapi darsa ambae aliinua hisa za mashabiki na kanza kuupedna muziki tena, hata hivyo Hanscana anajibu maswali ya mashabiki wa Darasa.

Hanscana ambae ni Director wa nyimbo nyingi na bora Tanzania na nje ya Tanzania,alikuwa ni moja ya watu wa karibu sana na darsa kwa kipindi chote Darasa alichokuwa akifanya kazi zake, na hata kumsaidia katika baadhi ya usimamizi ya nyimbo zake hivyo atakuwa anajua wapi alipo Darasa.

Akiongea katika Dizzim online hanscana anasema kuwa Daarsa yupo na amekuwa akijipanga ili kurudi kwa kishindo kwa sababu kazi ya muziki ni baishara kwake hivyo hawezi kuiacha.

Nafikiri ni mipango tu ,maana kila kitu kwenye maisha ni mipango tu,darasa muziki ni kazi yake , hiyo ndo ofisi yake , huwezi kumzungumzia darsa bila kuzungumzia muziki labda tumzungumzie Sharifu,Ramadhani au Hamis.

Naamini kila mtu anajua kazi zake na biashara zake kuliko mtu yoyote yule.ninaaamini kabisa darasa anajua biashara yake na muziki wake na kazi zake na kila kitu mtu anachokifanya kipo katika mipango yake na anavyokiona ni vizuri zaidi kuliko hata sisis tunavyomuona.labda kuna kitu anakuwa anakifanya kwa sasa ili akija kuachia basi iwe waooooh!.

Alichojibu Hanscana Kuhusu Kupima UKIMWI.

Inawezekana sio rahisi kwa baadhi ya watu kuwa na ujasiri wa kupima na kucheck afya zao mara kwa mara,waru wengi wamekuwa waoga sana kuhusu swala la kupima afya tena kupima UKIMWI.Kumbe hili swala liko tofauti kwa Hanscana moja ya music director  wakubwa bongo anaefanya vizuri na kazi zake kwa wasanii mbalimbali.

Akijibu swali la moja ya mashabiki zake katika ukurasa wake wa instagram baada ya kutoa fursa kwa mashabiki wake kuwa yuko tayari kuulizwa chochote , Hanscana aliulizwa kama alishawahi kupima ukimwi  na kwa haraka zaidi Hanscana alijibu'” jana tu“, akimaanisha kuwa ametoka kupima afya yake siku moja kabla ya kukutana na swali hilo.