Harmonize afafanua script ya video yake mpya kwa mashabiki wasioilewa

Imebidi Harmonize kuwaeleza mashabiki wake uhusiano wa video yake mpya na wimbo wake niambie unaowachanganya wengi. Muimbaji huyu wa Wasafi records amekuwa akiona malalamishi ya mashabiki wake wanoaamini kuwa alikuwa off script kwenye video yake mpya.

Harmonize akiwa na Wolper
Harmonize akiwa na Wolper

Kulingana na lyrics zake za Niambie, Harmonize anaonekana kuwa mtu ambaye hana pesa wala kwake ilhali video ya wimbo huo anaonekana akiishi kwa nyumba ya kifahari na maisha yake kuwa ni ya tajiri kitu ambacho hakiambatani na anachoimba.

Hata hivyo Harmonize alichukua fursa ya kuwafafanulia mashabiki wake alipokuwa kuwa kwenye interview na Prince Ramalove kupitia Kings Fm. Harmonize alielezea maana ya script ya hiyo video kwa kusema…

“Sina mtonyo lakini naishi kwake,sasa nikiishi kwake na yeye ana hela,ntafanyaje?”

Kwa ufupi muuimbaji huyo alikuwa akimanisha kuwa nyumba na magari zinazooonekana kwenye vdeo ni mali za Wolper kwa mujibu wa script.