Wolper: Siwezi Kusapoti Tena Kazi Za Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hawezi hataweza kukaa na kusapoti kazi za Harmonize sababu anamuonea huruma mpenzi wake Sarah.

Siku chache zilizopita Wolper alitengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye na mpenzi wa Harmonize Sarah kurushiana vita ya maneno kwenye Instagram.

Ambapo Sarah alimtaka Wolper aache kumtumia Meseji za kumtaka Mpenzi wake Harmonize jambo ambalo lilinkera Wolper kwani aliweka wazi kuwa akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa hivyo hakuwa yeye aliyekuwa anatuma Meseji.

Kwenye mahojiano aliyofanya leo na Sam Misago Wolper amesema kuwa ameamua kuacha kabisa kusapoti kazi za Harmonize:

Mimi sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kusapoti kazi zako lakini sasa naona ili nisikwaze mahusiano yako naona bora nisisapoti kazi za Harmonize kwa sababu yule mwanamke wake anahitaji kuhurumiwa”.

Lakini pia Wolper amesisitiza kuwa amefikia uamuzi wa kumblock Harmonize na Sarah kwenye Instagram ili aepushe maneno maneno.

Wolper: Sarah wa Harmonize Ana Matatizo Ya Kisaikolojia, Anahitaji Msaada

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu, Jacqueline Wolper amemtolea povu zito hasimu wake namba moja Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Ex boifrendi Harmonize.

Siku ya jana Wolper na Sarah waliongia kwenye vita ya maneno kwenye mitandao ya kijamii baada ya Sarah kwa mara nyingine kumtuhumu Wolper kwa kumtaka Harmonize.

Sarah alimpa onyo Wolper na kumtaka aache kuongea na Harmonize ambapo alitupia screenshots za meseji ambazo amekuwa akimtumia Harmonize huku imeonekana wazi kuwa hamjibu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Wolper amemjia juu Sarah huku akidai lazima atakuwa na ugonjwa wa kisaikolojia na kutaka watu wampe msaada:

Hivi ni vitu vya kuona huruma na kusamehe kwa sababu yule dada ana wasi wasi maskini anaamini kwamba nitachukua chombo chake wakati mimi muda huo sina lakini anajua mimi ni kiboko yake kwaiyo anaamini kuwa nitamchukua kitu ambacho siwezi mimi nikipita nimepita siwezi kumchukua tena na cha muhimu yule dada anahitaji mtu wa kumpima akili yule dada sio mzima ana matatizo ya kisaikolojia haiwezekaani kitu kidogo analipuka vile”.

Wolper amefunguka kuwa akaunti yake ilikuwa hacked na mtu ambaye ali hack alikuwa anatuma meseji kwa watu mbali mbali dm ikiwemo kwa Harmonize.

Wolper na Sarah Warudi Vitani Kwa Ajili Ya Penzi la Harmonize

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper na Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

Baada ya kutolewa povu hilo, Wolper alimrudishia kombora hilo Sarah na kuandika maneno haya:

 

Hii  sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

Sarah Amwaga Mamilioni Kumfurahisha Mpenzi Wake Harmonize

Harmonize amezidi kudhihirisha kuwa mpenzi wake mzungu ana hela chafu kwani amemzawadia saa yenye gharama kubwa.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na taarifa kuwa Sarah ambaye ni mzungu mwenye asili ya Uitaliano ana mkwanja mrefu ambao ndio unamuweka mjini Harmonize na kumpa jeuri ya kutanua na kuishi kistaa.

Sarah kwa kuonyesha jeuri ya pesa aliyonayo ameamua kumnunulia mpenzi wake Harmonize saa ambayo inatajwa kuwa na gharama sana ambapo Harmonize aliweka saa hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kumshukuru mpenzi wake kwa Zawadi hiyo na kuwasihi watu watafute bei yake.

Saa hiyo aliyozawadiwa Harmonize na mpenzi wake Sarah inajulikana kama brand ya Patek Phillipe saa hiyo inaonekana kwenye mtandao kuwa na thamani ya kuanzia dola za kimarekani 78,999 hadi 119,999 sawa sawa na shilingi za Kitanzania 177,755,649- 270,009,749.

Wolper: Sina Wivu Nimemualika Harmonize na Mpenzi Wake Kwenye Party Yangu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hana hata chembe ya wivu wa kimapenzi kwa Harmonize na mpenzi wake Sarah na ndio maana amewaalika wote wawili kwenye party ya birthaday yake.

Wolper na Harmonize waliachana miezi michache iliyopita baada ya kuwa pamoja kwa muda. Baada ya kuachana kila mmoja alimtuhumu mwenzie kwa kuchepuka huku Wolper akiweka wazi kuwa waliachana kwa sababu Harmonize alikuwa na uhusian na Sarah kwa sababu ya fedha alizonazo mzungu huyo. Lakini hata baada ya kuachana na kila mmoja kupata mpenzi ambapo Harmonize alianzisha uhusiano na Sarah na Wolper alianza uhusiano na Brown lakini bado wawili hao wamekuwa na bifu la chini chini.

Siku ya jana ilikuwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wolper ‘birthday’ ambapo yeye mashabiki zake pamoja na ndugu zake walienda kushiriki kula chakula cha mchana na kituo  cha kulelea watoto yatima Temeke. Lakini aliweka wazi kuwa party kubwa ya birthday yake itafanyika leo tarehe saba.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Wolper aliweka wazi kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na Harmonize wala  mpenzi wake mzungu Sarah ndio maana amewaalika kwenye sherehe yake:

Nimemualika Harmonize na sio yeye tu hadi mwanamke wake Sarah ili kuonyesha kuwa sina wivu wowote tupo sawa kabisa alafu ningekuwa nasikia wivu kama watu wanavyosema basi nisingewaalika kabisa yaani kwenye maisha mapenzi yanaisha na unatakiwa uendelee na maisha yako sasa mimi nimesha-move on na maisha yangu na nashukuru kwa sasa tumekuwa ndugu na Sarah inabidi tu awe ndugu yangu ili nimsaidie hata kujua kiswahili na pia nimsaidie kama Harmonize akichepuka nimpe nyendo zote ili nimwambie kama anachepuka kwaiyo inafika wakati watu inabidi tu muwe marafiki”.

 

Harmonize Amefunguka Kuhusiana na Ujauzito wa Mpenzi Wake Mzungu

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Harmonize amezidi kusisitiza kuwa mpenzi wake mzungu  Sarah ni mjamzito.

Baada ya kutangaza kuwa yeye na mpenzi wake huyo wanatarajia kupata mtoto na kuweka picha mbali mbali mtandaoni zinazomwonyesha mtoto akiwa tumboni (ultrasound), watu wamekuwa wakihoji ile mimba imeenda wapi kwani tumbo lake limezidi kuonekana dogo badala ya kukua kama wanawake wajawazito wengine.

Kwenye mahojiano na Times Fm Lilommy alimuhoji Harmonize juu ya ujauzito huo na haya yalikuwa majibu yake:

Sarah bado ni mjamzito na ninavyoongea na wewe amesafiri maana anajisikia vibaya kutokana na mimba yake amesafiri ameenda Italy nyumbani ila kingine ninachoweza kusema ni kuwa sisi waswahili na wenzetu tunaweza kuwa ni tofauti kidogo na vitu nitofauti yaani ukitumia jicho la kawaida huwezi kujua yaani hapa ninavyo zungumza na wewe anaumwa anaumwa vibaya sana ujauzito unampelekesha”.

Harmonize ameongezea kuwa endapo mtoto wake atazaliwa wa kiume basi atapendelea kumwita ‘Ibrah’.

Baada ya kutangaza kuwa wanategemea kupata mtoto miezi kadhaa iliyopita watu walishangaa kuona Sarah haonyeshi mabadiliko yoyote katika mwili wake ndipo habari za chini chini zilianza kuwa Sarah sio mjamzito bali ni stories waliotengeneza ili kupata kiki na kumuumiza roho mpenzi wake Wa zamani Jacqueline Wolper, habari ambayo Harmonize ameikana mara moja.

Harmonize: Namchukulia Wolper Kama Shabiki Wangu Tu

Msanii wa Bongo fleva maarufu kama Harmonize ameibuka na kudai kuwa anamchukulia Wolper kama shabiki wake tu na hakuna kingine.

Mwanzoni mwa wiki hii Jacqueline Wolper, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Harmonize na Sarah, ambaye ni mpenzi wa sasa wa Harmonize waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya Sarah kudai kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize. Sarah alivujisha meseji za Wolper mtandaoni na kupelekea Wolper kuchefukwa hivyo kumwambia Sarah kuwa alimuazima Harmonize kwa muda tu anaweza kumchukua muda wowote.

Baada ya hapo Wolper alianza kujirekodi anaimba wimbo mpya wa Harmonize unaotamba hivi sasa ‘Shulala’ na hivyo kupelekea minong’ono ya watu kuwa Harmonize na Sarah wameachana na Wolper kamchukua tena Harmonize kwani alimwambia siku nikimtaka Harmonize namchukua tena.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na XXL ya Clouds Fm, Harmonize aliweka wazi kuwa anashukuru mchango mkubwa wa Wolper katika nyimbo yake mpya kwani amejirekodi video mbili akionekana akifurahia wimbo huo.

Nadhani mwanzo ilikuwa ni hasira tu, nashukuru kuona mchango wa Wolper kwani namchukulia kama shabiki wangu tu”.

Pia kwenye mahojiano hayo Harmonize aliweka wazi mipango yake ya kuupeleka mziki wake kimataifa zaidi kwani hivi karibuni anategemea kusafiri kwenda Ghana kwaajili ya kurekodi video ya wimbo aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana, huu ni muendelezo tu wa mafanikio ya Harmonize kwani wimbo wake huu mpya wa ‘shulala’ amemshirikisha msanii Mkubwa kutoka Nigeria, Korede Bello.