Harmonize aachia picha mpya na mpenzi wake mpya, lakini hana ujauzito!

Muimbaji kutoka Wasafi records Harmonize amewaacha wengi wakijiuliza mimba ya mpenzi wake iko wapi. Hii ni baada ya kuachia picha mpya ambapo anaonekana akistahereka na mrembo huyo.

Hata hivyo Harmonize aliamua kuzima comment section yake ilimashabiki wake wasimchane kwa maneno. Katika picha hizi muimbaji huyo anaonekana akiwa na mrembo wake huyo akicheza pool table mbele ya nyumba ya kifahari inayosemekana wawili hao wanaishi.

Katika moja ya picha hizo msanii huyo aliweka wazi uwanja wa kutuma komenti lakini mashabiki wengi walionekana kuacha komenti mbaya kwa mpenzi wake na kwa hivyo akafunga komenti kwenye picha hizo zingine.

Tazama picha hizo hapa;

Harmonize adai kuwa ‘kuna mtoto na kuna mtoto wa kizungu

Harmonize kwa hivi sasa ameweka wazi anatoka na mtoto wa kizungu na kama mwanaume yeyote ambaye amelowa kwenye mapenzi, msanii huyu hajakuwa akificha furaha yake.

Msanii huyo wa Wasafi records alimzindua mrembo huyo hivi karibuni baada ya kuwachana na Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu. Hata hivyo akiongea kwenye kipindi cha 255 ya XXL ya Clouds FM Harmonize alisisitiza kuwa anatarajia mtoto wake atachukua rangi ya mamake.

Alisema,

“Ngoja nikwambie kitu kuna kuzaa mtoto na kuna kuzaa mtoto wa kizungu ni vitu viwili tofauti,” alisema Harmonize. “Naenda Marekani mara moja si unajua mke wangu anatakiwa kusarifi kaniambia kuna ishu tunaenda kufanya sasa mimba ikiwa kubwa atazuiliwa kupanda ndege,”