Huu ndio ujumbe ambao Harmorapa aliandika baada ya kupanda Ndege kwa mara ya kwanza

Harmorapa ni mmoja wa wasanii ambao hawakuwa na hella wala starehe kabla ya kuanza biashara ya muziki.

Kama msanii ambaye anaelewa shida za kutokuwa na hela, Harmorapa amekuwa mtu ambaye anajipanga ili asiziharibu hella zake na kwa sababu hii imemchukua muda kabla yeye kupanda ndege maishani mwake.

Hata hivyo hivi karibuni aliweka picha huku akiwa kwenye uwanja wa ndege. Kulingana na alichoandika, hii ndio ilikuwa Mara yake ya kwanza kupanda ndege na hangeweza kuificha furaha yake. Aliandika kusema…

“Maisha ni safari ndefu na mpangaji ni mwenyezi Mungu. Ukweli sikuwahi kuwaza katika maisha yangu kama ipo siku nitatimiza moja ya ndoto yangu ya kupanda ndege.
So ndugu zangu nawasihi ni mwiko kukata tamaa, omba Mungu sana atakutimizia ndoto zako. Shukrani #bossladySabuka kwa kunifikisha hapa nilipo, leo pia naomba Mungu ajalie aendelee kua na moyo huo wa kizungu maana kiukweli ni mzungu wa pekee.”