Mambo matano ya kuvunja moyo Wema Sepetu aliyomweleza Harmorapa kwenye instagram

Wiki ambazo zimekuwepo, Harmorapa amekuwa akichangamsha mitandao kwa kuonyesha mapenzi yake kwa Wema Sepetu.

Amekuwa akiweka picha ya Wema Sepetu kila siku na kunena ananvyompenda. Kwa video moja alijiami kumuoa Wema Sepetu na kutoa hadi pete.

Soma pia: Harmorapa aongelea wanadada watano Tanzania ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao…nambari moja ni Wema Sepetu

Na si hayo tu, pia aliapa kumlisha na kumvisha.

Leo Wema aliongelea ishu hiyo na hakuwa na mazuri ya kumwambia Harmorapa.

Hivi ndivyo alivyo post kwenye instagramu:

 

Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe…. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*

A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on

Harmorapa aongelea wanadada watano Tanzania ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao…nambari moja ni Wema Sepetu

Harmorapa alikuwa kwenye Millard Ayo juzi ambapo alizungumzia mambo mbali mbali la kwanza ikiwemo wanadada ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao mle Tanzania.

Na kama wasanii wengine wote Tanzania, wa kwanza alikuwemo Wema Sepetu ambaye Harmorapa alisifia ubo lake sana na pia macho yake.

Wa pili alikuwemo Lulu and bado akaendelea.

Pata ujumbe wote kwenye hii video: