Jah Prayzah aingia studio na Harmonize baada ya kutoa collabo kali na Diamond

Kila mtu anakumbuka ‘Watora Mari’ – wimbo huo bado ni hit kubwa mieze nane baada ya kuachiliwa. Msanii Jah Prayzah alishirikiana na Diamond kutoa wimbo huo.

Umaarufu wa Jah Prayzah ulienea barani mzima baada ya kumhusisha Diamond kwa wimbo wake. Msanii huyo kutoka Zimbabwe alinyakulia tuzo ya Listener’s Choice Awards ya MTV MAMA mwaka jana.

Jah Prayzah sasa imeingia studio na Harmonize – ujumbe aliouandika kwa mtendao wa Instagram unashiria ujao wa collabo yake na staa huyo kutoka WCB Wasafi.

“In the studio again with another Tanzanian big star @harmonize_tz .Zimbabwe neTanzania ?,” Jah Prayzah aliandika.