Dully Sykes Afunguka Kukopiwa na Harmonize

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Abdul Sykes maarufu kama Dully Sykes amefunguka na kuweka wazi kuwa amefurahi Baada ya Msanii Harmonize kukopi nyimbo yake.

Harmonize ametumia melody ya wimbo Dully Sykes wa muda mrefu unaofahamika kama ‘Handsome’ katika wimbo wake mpya alioutoa wa Kainama na kusema amefurahi kwa sababu ameona kama amemuenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Dully alisema kabla Harmonize hajaweka maneno katika wimbo huo, alimshirikisha kwanza na hata wakati anarekodi alikuwepo studio na akamshauri baadhi ya vitu.

Wala sijachukulia kama kaniibia melody yangu ila nimechukulia kama hali ya kunienzi f’lani hivi kwa nilichokifanya huko nyuma nilifurahi sana alipotoa wazo la kuchukua melody hiyo ambayo nilitumia katika wimbo wangu wa zamani uliokuwa unafahamika kama Handsome, na ameutendea haki vilivyo nimefurahi sana”.

 

Harmonize Atoa Siri Kuhusu EP Ya Afro Bongo

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize amefunguka na kutoa siri kuhusu EP (Extended Playlist) yake ya Afro Bongo.

Wiki iliyopita Harmonize aliachia ngoma nne kwa Mpigo alizozipa jina la Afro Bongo Lakini jana  ametoa siri kuwa video za nyimbo zake nne zote zipo tayari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameweka wazi kuwa tayari video za nyimbo zote nne akizoziachia ziko tayari.

MHH…!!! USICHOKIJUA NIKWAMBA
NGOMA ZOTE ULIZOZISIKIA KWENYE 
#AFROBONGO VIDEO ZAKE ZOTE ZIPO TAYALI BASI HAPA NILIVYOKAA NI KAMA MZEE YUSUFU YANI SINA PLESHAAA KWENYE TAALUMA YANGU …!! ?
OYAAA…!!! LINK PA BIO × 
@yemialade ???? @krizbeatz_ LET’S GO …!!!”.

Ifahamu Sababu ya Harmonize Kuita EP yake AFRO BONGO

Msaii wa bongo fleva Harmonize amefunguka na kutoa sababu ya kwanini Album yake ameamua Kuita Afro bongo , album ambayo imetoka hivi karibuni huku ikiwa na wasanii kibao kutoka nchi mbalimbali.

Msanii huyo anasema kuwa pamoja na yote lakini kikubwa kilichomfanya mpaka kuamua kuita hivyo ni kwa sababu muziki wa Afrika unaitwa AFRO na muziki wa Tanzania unaitwa Bongo fleva , hivyo aliamua kuunganisha.

Kwa sababu muziki wa Tanzania unaitwa Bongo fleva na muziki wa afrika unaitwa afro beats, iliamua kuunganisha kwa sababu muziki wetu sio wa Tanzania tu ni muziki wa Afrika.

Hata hivyo harmonize pia alitoa sababu ya kwanini aliamua kutoa album hiyo na kwenda kuzindua nchini Nigria kwa kusema kuwa hata Nigeria pia ni Afrika na kwa sababu muziki huo ni kwa ajili ya afrika basi ndio maana aliamua kwenda huko.

 

 

 

 

 

Harmonize Akana Mahusiano Yake na Sarah Mzungu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea kwenye Label kubwa Bongo WCB, Harmonize amejikuta akijikanyaga Baada ya kuulizwa kuhusu Mpenzi Wake na kuishia kukana mahusiano yake na Sarah Mzungu.

Harmonize yupo nchini Nigeria na siku ya jana,  Jumatatu Februari 25, 2019 alitembelea kwenye kituo cha radio cha The Beat 99.9 FM cha jijini Lagos kwa ajili ya Media Tour.

Kwenye mahojiano hayo, Harmonize aliulizwa maswali kadhaa na swali la kwanza lilikuwa ni “Tunamuona mwenzio Diamond yupo na Tanasha vipi wewe upo single?”.

DAHH MIMI? NIPO SINGLE NA NATAFUTA PIA…HAPANA NATANIA SIPENDI KUZUNGUMZIA SANA MAHUSIANO YANGU, UNAJUA MIMI MASHABIKI WANGU NI WANAWAKE NINAVYOJIBU WENGINE WATAJISIKIA VIBAYA”.

Kiukweli ni kwamba Harmonize yupo kwenye mahusiano ya muda mrefu na Mpenzi wake Sarah ambaye pia yupo kwenye moja ya nyimbo zake ambayo ipo kwenye EP yake.

Harmonize Adai Kuwa Yeye na Diamond Wanamiliki Hisa Sawa Sawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amefunguka na kuweka wazi yeye na Bosi wake  Diamond Platnumz wanamiliki hisa pasu kwa pasu kwenye kampuni ya Zoom Production.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha redio cha A FM cha jijini Dodoma, Harmonize ameanika ukweli ambapo amesema kuwa wote wawili wamegawana hisa sawa kwa sawa.

Wazo la kuanzisha Production company ni langu na nilipolipata nilienda Africa ya kusini na Marekani kununua kamera na baadae nikaja kusambaa Diamond, Bro! mimi naona tunapoteza hela nyingi sana kwenye video, mimi nimepata wazo la kuanzisha kampuni ya Video Productions wewe unaonaje?“

Harmonize amesema Diamond akakubali wazo hilo na kwa kuwa alikuwa ameshanunua kila kitu alivyorudi Bongo alimrudishia nusu ya manunuzi na kwa muda huo anasema kuwa alikuwa ameshmtafuta Director Kenny.

Zoom Production ni moja ya kampuni zinazofanya vyema kwenye ulimwengu wa Burudani na haimilikiwi na Diamond pekee ilivyoaminika hapo awali bali na Harmonize pia ana mkono mule.

Harmonize Apishana Kauli na Uongozi Wake Wa WCB

Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika Label ya WCB, Harmonize hana maelewano mazuri na viongozi wa Label yake.

Siku ya juzi Harmonize alitoa taarifa ya kwamba EP hiyo ataiachia February 18 siku ya jana lakini ilipigwa ‘stop’ tena na uongozi wa WCB na kuahidi siku ya leo watatoa taarifa rasmi.

Jumatano hii mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Sallam SK ametoa taarifa ambayo inaonyesha kuna kitu kinaendelea kati ya uongozi wake na Harmonize.

TAARIFA KWA UMMA.. Maelezo ya utokaji wa EP ya Harmonize @harmonize tz : Uongozi wa WCB unaomba msamaha kwa ucheleweshaji kama ahadi ya awali ilivyo, muda mwingine msanii anakuwa na shauku kubwa kuwapa mashabiki wake burudani na kufikia sehemu anasahau kuwa hizo burudani pia ni biashara ambayo itakayompatia kipato yeye ili aweze kutoa burudani zingine, kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote, kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao. Kwahiyo ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, tunashukuru Basata walitoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa. Kwa haya mafupi sasa EP ya Harmonize ya #AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi. Tunaomba radhi kwa yoyote tuliyemkwaza kwa namna moja ama nyingine tunajua bila nyie mashabiki hakuna WCB. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BONGO FLAVA ??“.

Taarifa hii inaibua maswali mengi juu ya mahusiano kati ya WCB na muimbaji huyo Uongozi wa WCB haukutangaza kwamba Harmonize ataachia EP kama ilivyo kwa wasanii wengine wote wa WCB.

Meneja Wa WCB toa Tamko kuhusu EP Ya Harmonize

Meneja wa WCB Sallam K amefunguka na kusema kuwa ile album ya Harmonize ambayo ilitangazwa kutoka hivi karibuni huku ikitazamiwa kuwa ni wiki hii haitatoka tena mpaka wiki ijayo kwa sababu za mashabiki na mipango ya kibiashara.

Meneja huyo amesema kuwa wameamua uplea mbele swala hilo kwa sababu wanataa pale inapotoka iwe ina uwezo wa kuwafikia mashabiki owte bila kubagua , hivyo wanajaribu  kutengeneza mazingira ya matabaka yote uweza uipata EP hiyo.

Hata hivyo sallam k anasema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa sababu kama kiwanda lazima kuwe na uataratibu mzuri wa kuuza na kusambaza bidhaa zao kwa watumiaji.

Hata hivyo kucheewa kwa kutoa kwa EP hiyo kumezua mambo mengi ikiwepo la usema kuwa Harmonize hayupo tena katika Lebo hiyo na ndio maana swala hili limekuwa gumu kitu ambacho wao wenyewe wanakanusha na kusema sio kweli.

Harmonize Kuja na ‘EP’ Aliyowashirikisha Diamond na BurnaBoy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema chini ya Label ya WCB Harmonize ameweka wazi ujio wa ‘EP’ yake ambayo itakwenda kwa jina la ‘Afro Bongo’.

EP (Extended Playlist) inategemewa Kubeba jumla ya nyimbo 4 na nyimbo hizo nne zitatolewa kwa Mpigo na itawashurikisha wasanii Kama Diamond Platnumz na BurnBoy wa nchini Nigeria.

https://www.instagram.com/p/BuDqYQ-nYJT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1b911qv81c77n

Lakini pia Harmonize ameweka wazi kuw wasanii ambao watasikika katika EP hiyo ni pamoja na Mr. Eazi, Yemi Alade na Mpenzi Wake Sarah.

https://www.instagram.com/p/Bt_nrHcnuHw/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ok4sqy5qjy8y

 

Harmonize Ajisalimisha Kituo cha Polisi

Msanii Harmonize ameamua kujisalimisha kituo cha polisi ili kutii amri ya mkuu wa mkoa Paul Makonda aliyoiagiza wiki iliyopita alipokuwa katika mkutano na wasanii nchini.

Harmonize ambae alikuwa akituhumiwa kwa kosa la uvutaji wa madawa ya kulevya yanayosadikika kuwa ni bangi hasa baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kijamii akiwa ameweka kitu mdomoni chenye uashiria wa kilevu icho.

Msanii huyo ambae ametua hivi karibuni akitokea nchini Ghana, aliamua kufika kituo kikuu cha polisi jijini na kujisalimisha ili kutii amri hiyo huku ikisemwa kuwa aliweza kushikiriwa zaidi ya saa tano kwa ajili ya mahojiano.

Harmonize Ajibu Tuhuma Za Makonda Za Kuvuta Bangi

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutokea katika Label ya WCB, Harmonize amefunguka na kukiri tuhuma zlizotupiwa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuhusu kuvuta Bangi.

Wiki iliyopita RC Makonda alimtuhumu Harmonize  kwamba huwenda akawa anatumia bangi baada ya kuonekana akivuta sigara yenye moshi mzito katika moja ya video ambayo aliiweka mitandaoni.

Katika hali ya kujitea Harmonize ameibuka na kukataa kabisa tetesi hizo na kusema wazi kuwa moshi ambao umeonekana kwenye video za Instagram ulikuwa moshi wa sigara na sio wa Bangi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alijibu tuhuma hizo kwa njia za utani akilihusisha na suala la Simba kufungwa goli 5 na Al Alhy ya Misri.

WAKATI MWINGINE TUACHENI UTANI TUWENI SERIOUS …!!! HIVI MIE NILIEJIPOST NA MIMOSHI YA SIGARA TENA SIGARA EMBASY HIYO BANGE YENYEWE NAISIKIA KWENYE BOMBA…!!! NA HAWA WACHEZAJI WA @SIMBASCTANZANIA
NANI WAKUSOKOMEZWA NDANI TUKITUA BONGO…???? ??? HEBU ANGALIENI WANAVOTESA WATU WASIOKUWA NA HATIA ?
MINAZANI TUNGEANZA NA @HAJISMANARAKWANZA AKAMATWE ACHUNGUZWE….!!! ??”.

 

“Harmonize Akitua Tu Tanzania Akamatwe Apelekwe Jela”-Makonda

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kutaka msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize achunguzwe na kama anatumia bangi basi Akamatwe na aswekwe rumande.

Mheshimiwa Paul Makonda ameagiza vyombo vya usalama kumchunguza msanii Harmonize kama anatumia bangi au lah! ili achukuliwe hate za za kisheria.

Makonda amezungumza hayo siku ya jana  Alhamisi Januari 31, 2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah

Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje”.

 

RC Makonda Aagiza Harmonize Akamatwe Kama Anavuta Bangi

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameagiza Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize Akamatwe kama atakutwa na hatia ya kuvuta bangi.

Makonda ameyasema hayo siku ya jana katika mkutano Wake aliyofanya na wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na Bongo Movie ambapo amekemea matumizi ya madawa ya kulevya.

Makonda ameweka wazi kuwa serikali inafanya kazi kubwa ya kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na hivyo haitawavumilia watu ambao watasika kujiingiza huko.

Makonda ameweka wazi anataka Harmonize achunguzwe kama anatumia bhangi kama anavyoonekana kwenye pich zake kwenye Mitandao ya kijamii na kama kweli basi Akamatwe awekwe Ndani.

Harmonize Atangaza Kolabo Yake na Burna Boy Toka Nigeria

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize ameibuka na kudokeza kwa ujio wa kolabo yake na staa wa muziki kutoka Nigeria maarufu kama Burna Boy.

Harmonize ambaye yuko nchini Nigeria kwa sasa ameonekana akiwa na Burnay Boy katika maeneo tofauti tofauti lakini pia akipost moja ya picha aliyopiga na Burna Boy na kuweka wazi kuwa kuna ujio wa kolabo yake mpya na mshindi huyo wa tuzo tatu za Sound city.

Lakini pia Htonize amedokeza ujio wa kolabo hiyo bila kutoa taarifa zaidi Mpaka sasa Harmonize ameshafanya kolabo na wasanii zaidi ya wanne wa Nigeria.

 

Harmonize Afungukia Sakata La Kuwatukana Wakenya

Staa wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rajab Abdul ‘Harmonize’ amefunguka na kuweka wazi Sakata lilimkuta siku chache zilizopita alipokuwa nchini Kenya.

Harmonize alifanya tamasha la Wasafi Festival Kenya tarehe 31 mwaka jana ambapo stejini aliwaambia Wakenya wanampenda kwa sababu Wakenya ni maskini wenzake ndiyo maana wanamuonesha mapenzi ya kweli katika muziki wake, lakini wao walitafsiri vibaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko Harmonize alisisitiza hakuwa na maana mbaya ila kilichotokea kilikuwa ni lugha gongana tu:

Unajua Kiswahili cha Wakenya na Watanzania ni tofauti ndiyo maana walitafsiri vile, ila mimi niliwaambia kwa nia nzuri tu kuwa watu wengi wananiuliza kwa nini Wakenya wanakusapoti sana kwenye muziki wako? Nikawaambia ni kwa sababu wao ni maskini kama mimi ghafla nashangaa watu wananishautia huku wanatikisa vichwa.

Huku wakisema usituite maskini maana tumelipa viingilio, sikutegemea kama itafikia hivyo, lakini nilitamani wajue kuwa sikumaanisha vibaya nawezaje kuwaita maskini wakati wao ndiyo wananiwezesha jamani”.

 

Harmonize Afunguka Baada Ya Raisi Kenyatta Kucheza Nyimbo Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Harmonize amefunguka Baada ya video kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii inayomuonyesha Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa anacheza wimbo wake.

Video huyo ambayo inekuwa ikitrend kwenye Mitandao ya kijamii imemuonyesha Raisi Kenyatta akicheza Wimbo wa Harmonize ‘Happy birthday’ alipokuwa Anasheherekea Birthday yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amemuandikia ujumbe wa shukrani dj wa Kenya ambaye alipiga wimbo huo ambao ulichezwa na Raisi Kenyatta Lakini pia Governor John.

https://www.instagram.com/p/BsV4EfsnBIl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rcu8l7jgntg1

 

Aliyekuwa meneja wa Harmonize Ayakwaa Maneno ya Mashabiki.

Aliyewahi kuwa meneja ya msanii Harmonize amejikuta akiingia katika wakati mgumu hasa baada ya meneja huyo kusema kuwa sababu kubwa iliyomfanya aachane na msanii Harmonzie na kuacha kumuongoza ni kutokana na taba ya msanii huyo kubadilika  kutokana na pesa.

Meneja huyo anasema kuwa sababu kubwa ni kuangalia tangu ameanza kufanya kazi na kijana huyo hakuwa kama alivyo sasa hivi kwa sababu hapo awali alikuwa akijituma na kufanya kazi hata kusikilizana lakini kadri siku zinavyozidi kwenda na mafanikio kuongezeka ndivyo anavyozidi kushusha nidhamu ya kazi.

Naelewa kuwa ni kijana mdogo ambae ametoka katika familia ya kimasiki lakini , utajiri , umaarufu na mafanikio aliyyapata yamemfanya  na kumuathiri tabia yake.

Maneno hayo yamewafanya mashabiki kumshambulia meneja huyo huku wakisema sababu kubwa ni yeye na wala sio msanii wao.