Odama Afunguka Mazito Baada Ya Kuzushiwa Kifo

Muigizaji wa Bongo movie Jeniffer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amenena mazito baada ya kuzushiwa Kifo katika mitandao ya kijamii.

Wiki hii kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuna taarifa ilisambaa kuwa Msanii huyo ameaga dunia taarifa zilizowashtua watu wengi sana.

Odama akielezea kilichotokea ame-screenshot picha za matangazo na kuyaposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kujamii na kuujulisha umma kuwa habari hizo sio za kweli.

Baada ya sakata hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Odama amefunguka na kusema anamshukuru Mungu na Kifo hupangwa na yeye tu na sio mwanadamu:

KIFO KIPO NA HAKUNA ATAKAEKIKWEPA… KILA BINADAMU ATAONJA MAUTI NA KUKAMILIKA KWA MAISHA YETU HAPA DUNIANI…. LAKINI PIA HATA KAMA HUMPENDI MTU UNAMCHUKIA IWE ALIKUTENDEA UBAYA AU UMEAMUA TU KUMCHUKIA SIO VIZURI KUMUOMBEA KIFO TENA UKAONA HAITOSHI BASI UNAWEKA MATANGAZO MITANDANDAONI…. NAKUSHUKURU WEWE ULIEAMUA KUFANYA HILI.. NAJUA UNANIONGEZEA UMRI WA KUISHI.. NA NIKUAMBIE TU KUA MIMI NI MZIMA WA AFYA NA NINAISHI KWA KUDRA ZA MUNGU.. NITAKUFA TU PALE SIKU YANGU ITAKAPOFIKA MUNGU ATAKAPOAMUA KUNICHUKUA LAKINI SIO KWA KUTAKA WEWE…. SIJUI NILICHOKUKOSEA MPAKA KUFIKIA KUNITANGAZIA KIFO… NAKUOMBEA MAISHA MAREFU ILI UENDELEE KUNIONA NIKIVUTA PUMZI YA MUNGU…. BINADAMU SISI LAITI TUNGELIJUA KUA SI KITU KABISA TUNGEACHA CHUKI ZISIZO NA SABABU…. ASANTE MUNGU KWA KILA KITU“.