Odama Akiri Kujitenga Mbali na Watu Wambea

Muigizaji wa Bongo movie Jennifer Kyaka maarufu kama Odama ameibuka na kuweka wazi kuwa anapenda kujitenga na kujiweka mbali na watu ambao wanafatilia maisha ya wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Odama ameweka wazi kuwa ukurasa kufanikiwa kwenye maisha ya kufuata ya kwani na Ndio maana anapenda kuzungukwa na marafiki ambao sio wambea na wanaofanya yao.

Katika maisha yangu nawapenda sana watu ambao hawafuatilii mambo ya wengine, wako bize na yao, hata rafiki zangu wengi wako hivyo si watu wa mambo ya umbeyaumbeya“.

Mimi nikimuona mtu hafuatilii maisha ya mwingine nampenda sana na tena nampa heshima yake kubwa, kwa sababu najua anajielewa.

Kwangu mimi huyo anaweza hata kuwa rafiki yangu mkubwa, maana mtu ukiwa kila wakati unachunguza mambo ya mwenzako, yako utayafanya wakati gani?”.

Msimamo Wangu Unaniponza na Kuonekana Naringa :-Jenipher Kyaka

Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu nchini Jenipher Kyaka Maarufu kama Odama, amefunguka na kusema kuwa siku zote amekuwa ni mtu wa kukaa na kufatilia sana misiamamo yake katika maisha kitu kinachowafanya baadhi ya watu wake wa karibu kuona kama anaringa lakini sio kweli.

Odama anasema kuwa pamoja na yote lakini alijifunza kitu kutoka kwa mama yake mzazi kuwa kila siku katika maisha usikubali kuendeshwa bali inakubidi kuwa na msiamamo wako wa maisha utakao kuongoza ili usiweze kumlalamikia mtu pale mambo yanapokwama.

kitu kikubwa ni kuwa na msiamamo katika maisha yko na ndio utaona unasonga mbele kila siku,  na ndio maana watu wengi wamekuwa wakiniona kama naringa lakini sio kweli ni kutokana na msiamamo wangu ndo unaniponza kuonekana hivyo.

“Msimamo Kwenye Maisha Ndio Kila Kitu”- Odama

Msanii wa filamu za Bongo Movie Jennifer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amefunguka na kuweka wazi msimamo wake ambao anao Kwenye maisha.

Odama amesema kuwa siku zote amekuwa mtu mwenye msimamo na kusimamia jambo lake, lakini anapofanya hivyo watu wanamchukulia tofauti na kumuona kama anaringa na asiyependa kusikia mtu na hicho ndicho kinamponza.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Odama amefunguka kuwa amejifunza kitu kikubwa kwenye maisha kupitia mama yake mzazi kwamba, kuwa na msimamo ndicho kitu muhimu kwenye maisha na ndicho anachofanya na hadi sasa amefanikiwa katika mambo yake mengi.

Kikubwa ni kuwa na msimamo katika mambo yako mengi ndiyo unaweza kusonga mbele zaidi na siyo vinginevyo. Ndiyo maana watu wengi wananiona tofauti kama ninaringa na nisiyependa kusikia cha mtu mwingine kumbe ni msimamo wangu tu ndiyo unaniponza nionekane hivyo“.

 

Odama Afunguka Mazito Baada Ya Kuzushiwa Kifo

Muigizaji wa Bongo movie Jeniffer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amenena mazito baada ya kuzushiwa Kifo katika mitandao ya kijamii.

Wiki hii kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuna taarifa ilisambaa kuwa Msanii huyo ameaga dunia taarifa zilizowashtua watu wengi sana.

Odama akielezea kilichotokea ame-screenshot picha za matangazo na kuyaposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kujamii na kuujulisha umma kuwa habari hizo sio za kweli.

Baada ya sakata hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Odama amefunguka na kusema anamshukuru Mungu na Kifo hupangwa na yeye tu na sio mwanadamu:

KIFO KIPO NA HAKUNA ATAKAEKIKWEPA… KILA BINADAMU ATAONJA MAUTI NA KUKAMILIKA KWA MAISHA YETU HAPA DUNIANI…. LAKINI PIA HATA KAMA HUMPENDI MTU UNAMCHUKIA IWE ALIKUTENDEA UBAYA AU UMEAMUA TU KUMCHUKIA SIO VIZURI KUMUOMBEA KIFO TENA UKAONA HAITOSHI BASI UNAWEKA MATANGAZO MITANDANDAONI…. NAKUSHUKURU WEWE ULIEAMUA KUFANYA HILI.. NAJUA UNANIONGEZEA UMRI WA KUISHI.. NA NIKUAMBIE TU KUA MIMI NI MZIMA WA AFYA NA NINAISHI KWA KUDRA ZA MUNGU.. NITAKUFA TU PALE SIKU YANGU ITAKAPOFIKA MUNGU ATAKAPOAMUA KUNICHUKUA LAKINI SIO KWA KUTAKA WEWE…. SIJUI NILICHOKUKOSEA MPAKA KUFIKIA KUNITANGAZIA KIFO… NAKUOMBEA MAISHA MAREFU ILI UENDELEE KUNIONA NIKIVUTA PUMZI YA MUNGU…. BINADAMU SISI LAITI TUNGELIJUA KUA SI KITU KABISA TUNGEACHA CHUKI ZISIZO NA SABABU…. ASANTE MUNGU KWA KILA KITU“.

 

Odama Apata Kigugumizi Tetesi Za Ujauzito.

Kumekuwa na tetesi za muda mrefu kuhusu msanii wa bongo movie Tanzania kuwa ni mjamzito  na kwamba aamekuwa akificha jambo hilo,hata hivyo msanii huyo alipoulizwa kuhusu swala hilo alijikuta akipatwa na kigugumizi na kushindwa kutoa tamko rasmi kuhusu swala hilo la yeye kuwa mjamzito .

Akiongea na star mix ya GPL,Odama kwa njia ya simu alisema kuwa kuhusu swala la yeye kuwa mjamzito ni swala nyeti sana,  hawezi kuongelea swala hilo kwa sababu yuko mbali na nyumbani.Hata hivyo alimuomba mwandishi kuwa mvumilivu mpaka atakaporudi ndio waweze kuzungumzia swala hilo.

.  Nipe muda  nilitafakari  swali lako, lakini  kama hutojali  tunaweza kuzungumza  mambo mengi  hilo naomba tuachane kabisa aidha unaweza kuningoja mpaka nirudi tuzungumze ana kwa ana kuhusu swala hilo  kwa sasa wala hata siwezi kukwambia kama nina mimba au sina. -Alisema Odama kwa njia ya simu.

Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakishindwa kusema mbele za watu au katika vyombo vya habari kuhusu swala la wao kuwa wajawazito ingawa kuwa mjamzito ni swala la kheri kwa kila mtu