Odama Akiri Kujitenga Mbali na Watu Wambea

Muigizaji wa Bongo movie Jennifer Kyaka maarufu kama Odama ameibuka na kuweka wazi kuwa anapenda kujitenga na kujiweka mbali na watu ambao wanafatilia maisha ya wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Odama ameweka wazi kuwa ukurasa kufanikiwa kwenye maisha ya kufuata ya kwani na Ndio maana anapenda kuzungukwa na marafiki ambao sio wambea na wanaofanya yao.

Katika maisha yangu nawapenda sana watu ambao hawafuatilii mambo ya wengine, wako bize na yao, hata rafiki zangu wengi wako hivyo si watu wa mambo ya umbeyaumbeya“.

Mimi nikimuona mtu hafuatilii maisha ya mwingine nampenda sana na tena nampa heshima yake kubwa, kwa sababu najua anajielewa.

Kwangu mimi huyo anaweza hata kuwa rafiki yangu mkubwa, maana mtu ukiwa kila wakati unachunguza mambo ya mwenzako, yako utayafanya wakati gani?”.

“Msimamo Kwenye Maisha Ndio Kila Kitu”- Odama

Msanii wa filamu za Bongo Movie Jennifer Kyaka maarufu kwa Jina la usanii kama Odama amefunguka na kuweka wazi msimamo wake ambao anao Kwenye maisha.

Odama amesema kuwa siku zote amekuwa mtu mwenye msimamo na kusimamia jambo lake, lakini anapofanya hivyo watu wanamchukulia tofauti na kumuona kama anaringa na asiyependa kusikia mtu na hicho ndicho kinamponza.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Odama amefunguka kuwa amejifunza kitu kikubwa kwenye maisha kupitia mama yake mzazi kwamba, kuwa na msimamo ndicho kitu muhimu kwenye maisha na ndicho anachofanya na hadi sasa amefanikiwa katika mambo yake mengi.

Kikubwa ni kuwa na msimamo katika mambo yako mengi ndiyo unaweza kusonga mbele zaidi na siyo vinginevyo. Ndiyo maana watu wengi wananiona tofauti kama ninaringa na nisiyependa kusikia cha mtu mwingine kumbe ni msimamo wangu tu ndiyo unaniponza nionekane hivyo“.