Baada ya mashabiki kumfananisha na Jay Z, Joh Makini asema haya

Wengi wanaopenda nyimbo za Bongo wananamtambua Joh Makini kama mmoja wa wasanii ambao wanapiga nyimbo ambazo zinapendwa na wengi Afrika Mashariki.

Joh Makini kwa kweli anatalanta ambayo imempa uwezo wa kufanya kazi na wasanii wakubwa kutoka Afrika na iwapo ataendelea hivyo miaka ijayo basi anaweza pia fanya kazi na wasanii kutoka nje ya Afrika.

Jay Z

Kwa sasa wengi wanamfananisha na rappa wa Marekani Jay Z, kitu ambacho kimemfanya kufurahi sana. Japo anajua kuwa bado anavitu vingi vya kufanya kabla kumfikia mkali huyu, Joh Makini amesema kuwa mashabiki wake kumuweka kiwango cha Jay Z ni kitu kubwa sana.

Akizungumza muimbaji huyo alisema,

“Jay Z ni ‘role model’ wangu…mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika ‘level’ ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye… Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z ‘yeah i like it’ kuliko ungenifananisha na mtu mwingine”