Magufuli apiga marufuku Brookside Dairy – kampuni linalomilikiwa na rais wa Kenya

Brookside Dairy ni miongoni mwa kampuni 20 kutoka nchi jirani ya Kenya ambazo zimepigwa marufuku Tanzania siku mbili zilizopita.

Ubishi kati ya Kenya na Tanzania ulianza Aprili 2017 baada ya serikali ya Kenya kupiga marufuku gesi na ngano kutoka Tanzania.

Serikali ya Rais John Magufuli ililipisha kisasi kwa kuweka vikwazo kwa ununuzi wa sigara na bidhaa za maziwa kutoka Kenya.

Hatimaye Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Kenya na Tanzania – Amina Mohamed na Augustine Mahiga walifanya mazungumzo Nairobi wiki jana na kuamua kutatua mvutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Kenya na Tanzania – Amina Mohamed na Augustine Mahiga wakifanya mazungumzo Nairobi

Hata hivyo serikali ya Tanzania lilirejea hatua ya awali ya kuweka vikwazo kwa bidhaa kutoka Kenya. Kampuni 20 kutoka Kenya zimepigwa marufuku kufanya biashara Tanzania.

Brookside Dairy, kampuni inayohusishwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, ni miongoni mwa kampuni zilizopigwa marufuku.

Rais Uhuru Kenyatta na John Pombe Magufuli

Rais Magufuli hakupenda jinsi Brookside inaendesha shuguli zake Tanzania tangu achukue mamlaka 2015. Rais Magufuli alilaumu kampuni za Kenya zinazonunua maziwa Kaskazini mwa nchi akisema wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza kufanya kazi hiyo. Alisema kampuni za Kenya zinawadhulumu wafugaji wa Tanzania.

Kampuni hiyo – Brookside Dairy ina matawi matatu Tanzania, moja Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

 

Staa wa nyimbo za Injili Upendo Nkone atuma ujumbe maalum kwa Rais John Magufuli

Mwimbaji Upendo Nkone ametuma ujumbe maalum kwa rais Magufuli akimwambia kwamba yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge.

Nkone ata hivyo amesema hataki kujiunga na siasa kwa ubunge wa kugombea jimboni ila kama mbunge mteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema kuwa yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge iwapo Magufuli atamteua.

Upendo Nkone

“Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea…. Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba,” alisema Upendo Nkone.

Nkone alisisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa kumteua kwasababu kuwa yeye mchakato wa kupata ubunge wa kugombea ni mgumu na una mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama, jambo ambalo haliwezi.