Jokate Atangaza Ndoa Hivi Karibuni

Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006/07 na mfanyabiashara maarufu Jokate Mwegelo amefungukia nia yake ya kuolewa hivi karibuni.

Jokate ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa kabisa ya urembo inayoenda kwa jina la Kidoti, amefunguka hayo siku ya jana alipokuwa ansheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Ambapo kwenye ujumbe huo Jokate alifungukia harusi yake lakini pia aliongelea nia yake ya kuzaa watoto baada ya kuolewa.

Jokate alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

March Baby, March Queen soon to be somebody’s wife and mummy God is great and faithful, Grown but forever baby girl ni kwa Rehema na Neema tu”.

June mwaka jana katika mahojiano na Gazeti la Mtazania Jokate alisema anatamani umri ukifika apate watoto mapacha na wote awalee katika maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote mbili na kuweza kujifunza kilimo na kula chakula vya asili.

Jokate Ahaidi Kuwashika Mkono Wanawake

Mfanyabiashara na mmiliki wa brand ya Kidoti, Jokate Mwegelo amewatolea ofa wanawake wajasiriamali wote ya kuwashika mkono kwenye biashara zao kwa kusaidia kuwatangazia biashara.

Jokate alianza kupata umaarufu baada ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006/ 2007 na kuwa mshindi wa pili tangia hapo Kidoti aliendelea na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam mpaka alivyomaliza masomo yake.

Jokate alijiingiza kwenye biashara na kutengeneza kampuni yake ya Kidoti ambayo imemletea mafanikio mengi sana na kukua kwa kasi ya ajabu mbali ya kuwa mfanyabiashara Jokate pia hivi sasa ni mwanasiasa wa CCM na ni kaimu Katibu wa uhamasishaji UVCCM.

Jokate baada ya kupata mafanikio hayo amefunguka kuhusu nia yake ya dhati kabisa ya kutaka kusaidia vijana hasa Wanawake ambapo kwenye ukurasa wake wa Instagram ametangaza fursa ya kuwatangazia Wanawake biashara zao:

Wanasema kutoa ni moyo na sio utajiri kuna wengi wana vingi lakini mioyo yao migumu kutoa na wapo ambao wako tayari kugawana kile chao cha mwisho hata ikimaanisha wasibaki na chochote ilimradi wewe upate na ufanikishe lako. Mpaka kufika nilipofika Mwenyezi Mungu amenipa watu wengi sana wakunishika mkono na kunisogeza karibu na ndoto yangu. Nimepitia kurasa zenu na kusoma matamanio yenu. Naomba mwaka huu kwa ajili ya sikukuu ya Wanawake Duniani naomba nifanye kitu tofauti kidogo naomba Wanawake/ wadada chini ya miaka 35 wake kwangu na biashara wanazofanya na mimi nitawa  support tutawapa kiasi cha shilingi  milioni 1”.

 

Hatimaye Wema Na Jokate Kufanya Kazi Ndani Ya Wizara Moja.

Yawezekana walishawahi kukutana mahali lakini wakawa sio kama watakavyokuwa sasa hivi , ni mategemeo ya wengi kuwa baada ya wawili hao kuweka sehemu moja kwa ajili ya kufanya kazi basi watakuwa marafiki na watu wa karibu kuliko hapo awali.

Wema Sepetu   na Jokae wameteuliwa kuwa wajumbe kwa mwaka huu katika wizara ya maliasili ili wawezi kuwa  mabalozi katika swala la utunzaji wa mali ya asili ikiwa ni mwezi wa maadhimisho ya Urithi wa maliasili Tanzania.

Mapema jana waziri wa maliasili Mh. Kigwangala aliteua mabalozi nane watakao kuwepo katika kamati ya  maalumu ya taifa itakayohusika na  maandalizi ya maadhimisho ya utunzaji wa maliasili tanzania ambapo Wema Sepetu  na Jokate Mwegelo watakuwepo kaatika kamati hiyo.

Tumeongeza majina ya wajumbe wa kamati ya utunzaji wa urithi tanzania, ilikupata wawakilishi wa watu wa zanzibar na viajana pia, kamati hiyo itahusika na  kuweka sawa wazo hili nakuweka swa mambo yote.- .Alisema waziri mwenye dhamana hiyo

Haijawai kusemwa hadharani kama wawili hao walishawai kuwa maadui lakini mashabiki wanapata tumaini kubwa kuwa wawili hao watakapofanya kazi pamoja basi kila kitu kitakuwa sawa tena hasa ukizingatia wawili hao wamekuwa ni watu wenye nafasi kubwa sana katika jamii hasa katika maswala ya uhamasishaji.

Jokate:Kwenye Siasa Tumefuata Uongozi Sio Pesa

Mwanadada Jokate Mwegelo ambae kwa sasa amejikita sana katika kutoa huduma kwa jamii kupitia brand yake ya kidoti na pia anaefanya vizuri kama katibu wa UVCCM, amesema kuwa ukiachana na kazi ya kuwa mrembo lakini bado kuna mambo mengi mwanadada anaweza kuyafanya yataakayo nufaisha jamii kwa ujumla.

Akiongea na GPL, Jokate anasema kuwa katika kupambana na maisha kuna nyanja nyingi unatakiwa kuwa nazo  ili kupata pesa na sio kujibweteka kukaa katika upande mmoja tu. Hata hivyo Jokate anasema kuwa watu wanadhani kuwa katika siasai ni kufuata ela ,hii sio kweli bali watu wanakaa katika siasa ili kupata uongozi ela kila mtu anatafuta.

Jokate ambae ana nembo ya Kidoti anasema kuwa ni moja ya vitu vinavyoinua sana vijana na yeye ni kiongozi tu lakini kuna watu wengi wanaonufaika hapo.

Akiendelea kuwaasa wasichana Jokate anasema kuwa hakuna jambo linalofanyika kirahisi kila kitu ni lazima  uwe tayari kulipa gharama, anaendelea kusema kuwa watu wengi hasa wanawake wamekuwa wakitaka kupata urahis katika maisha lakini  bila kulipa gharama.

Hata hivyo jokate anasema kuwa watu  hawapaswi kuisi kuwa changamoto ni kutokufanikiwa bali mtu anaepitia matatizo ndio anaweza kufikia pale anapopata kwa sababu uvumilivu ndio kila kitu kinachoitajika ili kuweza kufanikiwa.

Jokate anasema kuwa kwa mtu yeyeote anaetaka kufanikiwa ni lazima kupanga mikakati itakayomfanya yeye kuwa na mafanikio,kupambana na ndoto zao na bila kukata tamaa, kama una ndoto hakikisha ndoto hiyo inatimia na kama inafeli basi ni bora kujaribu tena na tena na sio kukata tamaa.

Jokate Ageukia Kwenye Uhandishi, Amwaga Sifa Kwa Raisi

Ni moja kati wa wasichana wa kitanzania aliopiga hatua kubwa sana katika sekta ya uchumi hasa kutokana na kujituma kwao.Alianza kwa platform ya urembo lakini baadae aliona fursa aliyoipata kwenye urembo inaweza kumfanya akaanzisha vipaji vingine vilivyo ndani yake.Jokate alianza kuwa mjasiriamali kupitia tasnia hiyo hiyo.

Kadri mafanikio yalivyozidi Jokate aliona anaweza kufanya urembo, biashara na bado akasaidia jamii yake katika mahitaji mbalimbali ya jamii yake, hivyo akaanza kusaidia sekta ya elimu kwa kuwapa hasa wasichana waliopo mashuleni vifaa mbalimbali kama mabegi,vitabu na hata baiskeli ili kuinua kiwango cha elimu kwa mtoto wa kike.

Lakini kumbe kuna baadhi ya walioona mchango wake katika jamii, Jokate aliteuliwa kuwa kaimu katibu mhamasishaji wa Chama Cha Mapinduzi yaani CCM, hii ilimuongezea Jokate fursa ya kukutana na watu mbalimbali hata kutambua matatizo yanayoikumba jamii yake kwa ujumla.

Ukiachana na urembo, ujasiriamali na kuwa mhamasishaji bora kwa vijana, lakini pia Jokate amekuwa ni moaj ya watu waliowahi kuingia katika tasnia ya muziki na wakafanya vizuri.Mwanadada huyo sasa amegeukia katika swala la uhandishi wa vitabu na makala.

Akiitambulisha kazi yake ya uhandishi katika ukurasa wake wa instagram, Jokate amesema kuwa sasa ameweza kuwa mwandishi ambapo katika kazi hiyo mwanadada Jokate ameandika maoni yake na kutoa  sifa za kumsifia raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. raisi John Pombe Magufuli na utendaji wake wa kazi akiwa katika kiti cha uraisi kwa miaka miwili aliyotimiza sasa.

 

 

Katika makala hiyo Jokate ameonyesha kazi mbalimbali alizofanya mheshimiwa raisi, uzalendo na utendaji kazi wake, mabadiliko kipindi cha awamu yake na misimamo mikali aliyonayo raisi katika kutekeleza kazi zake.Katika kazi yake hiyo Jokate amemfananisha raisi na nabii Mussa  anaepatikana katika vitabu vya dini.

 

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh. John Magufuli.

Jokate anazidi kuonekana mmoja wa wasanii na warembo waliokuwa wakijituma bila kusubiri mafanikio kutoka kwa watu wengine, anaweza kuwa ni msichana wa kuigwa wa watu wengine.

Jokate akiwa katika moja ya mikutano yake ya kiharakati.

 

Jokate Kustaafu Muziki, Ni Baada Ya Kutoa Ngoma Yake Ya Mwisho

Mwanadada mwenye vipaji vingi nchini Jokate Mwegelo amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anataka kuachana kabisa na muziki na kujikita katika vitu vingine kabisa kwa sababu anavitu vingi vya kufanya.

jokate Mwegelo  ambae aliwahi kushiriki Miss Tanzania , amekuwa ni mmoja wa wanawake wa kitanzania walioingia katika list ya kufanikiwa na kujituma sana katika jamii mpaka kufikia kutambulika kimataifa na kwa juhudi zake akiwa bado kijana na amekuwa akirudisha fadhila kwa kujikita kusaidi wasichana wanaosoma katika mazingira magumu.

Ukiachana na kazi ya jamii anayofanya , lakini pia Jokate Mwegelo ni mjasiriamali na pia ni mwanamuziki ingawa amekaa kwa uda mrefu kidogo kutokana na kuwa na mambo mengi katika jamii yanayomtaka kuyatimiza.

Hivi karibuni Jokate  Megelo amewaambia mashabiki wake anategemea kutoa wimbo mpya ambao ndio utakuwa wimbo wake wa mwisho na kisha kuacha muziki huku akisema kuwa   hana sababu yoyote ya kuacha muziki lakini baada ya wimbo huo ndio itakuwa mwisho wake wa kufanya kazi za muziki.

“Nafikiria kutoa wimbo mmoja wa mwisho,alafu baada ya hapo ninategemea kustaafu kabisa maswala ya muziki,kwaweli sina sababu yoyote ile ya msingi ya kuacha muziki ila ni maamuzi yangu tu” alisema Jokate Mwegelo

Hivi karibuni jokate alisema kwa sasa anajikita katika kutetea na kusaidia wanawake katika kupata haki zao kwa sababu amegundua pia kuwa wanawake wengi wako mitaani na wanaonewa lakini hawajui wapi pa kukimbilia, hivyo kitendo cha Jokate kuachana na muziki inaweza kumpa pia muda mrefu zaidi katika kusaidia jamii.

Nyota Za Warembo Hawa Zazidi Kung’aa Zaidi (picha)

Katika kuonyesha kuwa kweli wanajitihada ya kazi wanazofanya warembo Elizabeth Michael ‘Lulu’,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Jokate Mwegelo wamekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwa ujumla kutokana na jitihada zao na uwezo wao wa kufanya kazi na zikaonekana na jamii.

Haya ni baadhi ya mafanikio waliyofikia warembo hawa ambao wanahitaji pongezi:

  1. Vanessa Mdee
Vanessa kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram leo hii ametangaza kuwa ataungana na hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam ambapo atakuwa Balozi wa Hoteli hiyo, hayo ni mafanikio mazuri sana kwa Vanessa na anastahili pongezi. 

2. Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwania Tuzo za Vjana 100 wenye ushawishi mkubwa Africa(100 Most Influential Young Africans) kama Mfanyabiashara kupitia kampuni yake ya Kidoti. Hivi sasa Jokate yupo nchini Marekani kwaajili ya kushiriki Mkutano unaojulikana kama Forbes Under  30 Summit kwaajili ya kukutana na Vijana Wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

3. Elizabeth Michael

Elizabeth Michael kupitia Azam TV amechaguliwa kuwa Balozi wa Tamasha la tuzo za filamu kwa upande wa Africa Mashariki ikimaanisha kuwakilisha Tasnia ya Filamu za Bongo Movie katika Tuzo hizo.

Wanawake wote hawa warembo wamethubutu na wameweza na ni vyema kuwapongeza mara kwa mara katika Jamii Zetu.

Jokate Mwegelo aeleza malengo yake baada ya kukutana na Jay Z, Beyonce, Akon na Thiery Henry

Jokate Mwegelo amekutana na baadhi ya wasanii mashuhuri dunia kote akiwemo Jay Z na mkewe Beyonce, Akon, Thiery Henry na wengineo.

Mwanamitindo huyo amesema sasa malengo yake ni kukutana na rais mustaafu wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama.

Jokate Mwegelo na Akon

Jokate pia anatamani kukutana na mwanamuziki Rihanna. Alisema kuwa muimbaji huyo mashuhuri anafanana na yeye hadi mauombo yetu.

“Natamani sana kukutana na mwanamuziki Rihanna pia Obama na mkewe. Rihanna namuelewa sana kwa sababu tunafanana hadi mauombo yetu, itakuwa safi sana nikikutana naye,”alisema Jokate.

Jokate Mwegelo na Thiery Henry

 

“Muda wa Ali kuoa sasa umefika” Familia ya Ali Kiba wamtaka afunge ndoa na Jokate Mwegelo

Mamake na dadake Ali Kiba wametoa kauli zao kuhusu staa huyo kufunga ndoa. Wawili hao walisema muda umefika kwa Ali Kiba kuoa.

Akiongea na Global Publishers, mamake Ali Kiba alisema kuwa mwanawe anahitaji mke wa kumchungia watoto wake wanne ambao walizaliwa na wanawake tofauti.

“Mimi kama mzazi, ninaona muda wa Ali kuoa sasa umefika maana kama ni maisha ya ujana amesha­fanya kila kitu, ana watoto wanne na kila mmoja na mama yake, ni vi­zuri sasa akachukua mke ili aweze kuwalea hawa watoto wake. Mimi kama mzazi huu ndiyo msimamo wangu, ninamtaka ata­fakari na kuchukua uamuzi mara moja, maana ingawa siyo vizuri kwa mzazi kumpangia mtoto wake cha kufanya, lakini inapofikia suala la kuoa ni muhimu ukasimama na ku­toa msimamo, wakati wa kuoa ume­fika,” alisema mamake Ali Kiba.

Dadake Ali Kiba – Zabibu alisema kuwa Jokate Mwegelo ndo mwanamke ambaye Ali Kiba anafaa kufanga naye ndoa. Zabibu alimsifu Jokate kwa kusema kuwa ni msichana mwenye busara.

Jokate Mwegelo

“Mimi namchukulia Jokate kivingine kabisa, ni msichana mwenye busara zake na amekuwa kama mshauri wangu wa karibu mno, ningetamani angekuwa mke halali wa kaka yangu kwa sababu ana vigezo vyote vya kuwa hivyo. Kwa kuwa kaka yangu bado hajaoa, ninaomba kila kukicha na­fasi hiyo ichukuliwe na Jokate kwa sababu ni mwanamke anayestahi­li kuipata nafasi hiyo ya kuwa wifi yangu,” alisema Zabibu ambaye pia ni rafiki wa mastaa wengi,”alisema Zabibu.