Mheshimiwa Jokate Ala Kiapo Cha Kuwa Mkuu wa Wilaya Ya Kisarawe (+video)

Msanii na mfanyabiashara Jokate Mwegelo amekula kiapo rasmi siku ya leo cha kuwa mkuu wa mkoa wa Kisarawe.

Jokate ameapishwa siku ya leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo katika hafla fupi iliyofanyika wilayani humo.

Hii ni video fupi ya tukio hilo:

https://www.instagram.com/p/BmAl7EmBCpf/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1642csbb1n6uh

Steve Nyerere -Hakuna Msanii Yoyote alikasirishwa na Uteuzi wa Jokate .

Msanii wa bongo movies steve nyerere amefunguka na kukanusha ttesi zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuwa amekasirika kwa sababu ya  kuteuliwa kwa mwanadada Jokate kuwa mkuu wa wilaya ya kisarawe na kusema kuwa yeye anamshukuru sana rais kwa sababu ameleta heshima katika tansia ya sanaa.

Steve anasema kuwa maneno yamekuwa yakizunguka mengi sana huku wengine wakipinga uteuzi huo kuwa ni wa upendeleo lakini kwake ni furaha sana kwa Jokate kuwa mkuu wa wilaya.

moja ya kazi aliyonayo baada ya kuteuliwa ni kutuwakilisha sisi vijana wenzake na ametuwakilisha sisi vijana,kwa namna moja ama nyingine hakuna msanii yoyote au msanii yoyote  alikasirishwa na uchaguzi wa ma-DC wote tuko tayari kuwasapoti katika kazi kwa namna moja au nyingine. vinavyoongelewa na kuashiriwa ni vya kwenye mitandao tu wala hakuna kitu kama icho.

Ali Kiba Avunja Ukimya Kuhusu Uteuzi wa Jokate

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amevunja ukimya na kufunguka kuhusu uteuzi wa aliyekuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Ali Kiba ambaye alikuwa mpenzi wa Jokate amefunguka Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv,  kusema anamtumia salamu za pongezi na kumtakia kila la Kheri;

Siwezi kulizungumzia sana hilo lakini kwa ufupi tu ni kwamba nimefurahi na nampa hongera sana”.

Lakini pia kaka wa Ali Kiba, Abdu Kiba ambaye pia alikuwa na ukaribu na Jokate amefunguka na kumpongeza Jokate:

Namtakia kila la heri na aweze kuongoza vyema Kwenye uongozi wake. Sijapata nafasi ya kuongea naye kwa sababu naamini yuko bize lakini pia sijawahi kuwasiliana naye kwa kipindi kirefu lakini Kupitia hii Interview namtakia kila la kheri Kwenye maisha yake”.

Jokate aliteuliwa siku chache zilizopita na Raisi John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Barnaba Aongelea Uteuzi wa Jokate.

Msanii wa muziki wa bongo fleva kipaji bora kutoka THT , Barnaba classic amefunguka na kumpongeza sana mwanadada Jokate Mwegelo kwa kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya kisarawe na kusema kuwa hiyo ni moja ya hatua kubwa ambavyo nchi yetu inapiga kwa kutambua michango wa watu katika tasnia.

Akiongea na simple katika kipindi cha break, Barnaba anasema kuwa amefurahia uteuzihuo lakini anawaona wale ambao wanamsema na kumponda na hata kuchukia utezi wa jokate ni wapumbav na wamekuwa wakipoteza muda wao kufanya kitu kama hicho.

Nampongeza sana Jokate kwa uteuzi, na kwa wale ambao wamekuwa wakimsema vibaa naona ni wapumbavu tu, wapumbavu tena sana kwa sababu kama mtu una kazi zako za kufanya huweiz kukaa na kumsengenya mtu, nasema ni wapumbavu mara mbili.

Mwanadada Jokate anatarajiwa  kuripoti na kuapishwa na mkuu wake wa mkoa katika kituo chake cha kazi.

Nimependa na Kukubaliana na Uchaguzi wa Jokate- Irene Uwoya

Msanii katika tasnia ya Bongo Movie Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa amependa na amekubali kabisa katika uteuzi wa Msanii mwenzake Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa wilaya.

Uwoya amefunguka hayo wakati alipokuwa anajibu barua ya wazi ya msanii Rado ambaye alimhoji kuhusu ushiriki wake katika siasa na kudai anaona kama Uwoya amestahili pia kuchaguliwa kuwa mbunge.

Kama utakumbuka mwaka 2015, Irene Uwoya aligombania nafasi ya Ubunge viti maalumu CCM na kusema ukweli alifanya vyema sana lakini Rado amemuuliza Uwoya kama anataka kuenda mbele kama Jokate je Dogo Janja anafaa kuwa kama mume wake?

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya ametoa majibu kuhusu hilo ambapo ameweka wazi kuwa hana wivu wala tatizo na Jokate kuchaguliwa kwani anaheshimu maamuzi ya Raisi Magufuli.

Naamini sana katika maamuzi na mapendekezo ya mwenyekiti wangu wa Chama. Naamini sana na nimependa uteuzi wa Jokate kwa sababu baada ya kampeni na uchaguzi kuisha watu wengi tuliendelea na mambo yetu binafsi lakini ukifuatilia kwa ukaribu Jokate amepambana na amekuwa karibu sana na harakati za chama na haswa kushiriki katika shughuli za kijamii kwa haya na mengi zaidi nampongeza zaidi kwani amepanda mbegu nzuri ambayo amevuna mavuno mazuri hongera kwake Mheshimiwa Jokate Mwegelo”.

 

Huddah Awachana Wabongo Kwa Unafiki Amkingia Kifua Jokate

Socialite maarufu kutoka pande za +254 Kenya, Huddah Monroe amewatolea uvivu wabongo kwa vitendo vya kinafki walivyomfanyia Jokate Mwegelo mara baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

Huddah amewatolea povu watu waliomnanga Jokate baada ya Ali Kiba kumuoa mwanamke mwingine ambaye ni Amina mwaka huu na kusababisha watu kumcheka sana Jokate.

Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Huddah ameandika ujumbe huu:

Ali Kiba alivyomuoa msichana mwingine mapema mwaka huu watu walimcheka sana na kumdhalilisha Jokate. Lakini sasa hivi anapata mafanikio hao hao watu wanageuka na kumpongeza ama kweli mitandao imeshindikana. Hana mashabiki wa kweli bali ni wanafiki tu na wanaondoka kwa upepo”.

Ali Kiba alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Jokate kwa muda mrefu lakini mapema mwaka huu alimuoa Amina.

Wikiendi iliyopita Rais Magufuli alimtangaza Jokate kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe jambo lilipelekea kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa mashabiki mbali mbali na hata wasanii wenzake.

Flaviana Matata Amkingia Kifua Jokate Kwa Wanaomponda Kuwa DC

Mlimbwende na Model wa kimataifa Flaviana matata amefunguka na kumkingia kifua Mrembo Jokate Mwegelo baada ya kupondwa sana baada ya kutangazwa Mkuu wa wilaya siku chache zilizopita.

Siku chache zilizopita Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti tofauti huku wapo waliofurahishwa na taarifa hiyo na kuona Jokate anastahili nafasi hiyo Lakini pia wapo walioona Jokate hastahili kupewa nafasi ya kuongoza wilaya.

Baada ya Mkanganyiko huo mashabiki mbali mbali walianza kuweka mambo ambayo yalikuwa negative huku wakimtupia madongo na asilimia kubwa waliokuwa wanafanya hivyo walionekana kuwa ni wanawake.

Flaviana Matata alishindwa kuvumilia na kumtetea Jokate ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter Flaviana aliwataka wanawake wapendane na wampe sapoti Jokate kwani amepata nafasi ya kusaidia wanawake wengine:

Wanawake hatupendani very sad. Not sure hii itabadilika lini we need to support her na kukumbuka anatuwakilisha wanawake wote”.

 

Jokate Afunguka Baada Ya Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya

Mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006-2007 Jokate Mwegelo amefunguka rasmi baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya siku ya Jumamosi.

Jokate ameteukiwa kuwa mkuu wa wilaya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki iliyopita.

Baada ya kupata nfasi hiyo Jokate amefunguka mazito ambapo ameweka wazi kuwa mwaka jana tu alikuwa Kwenye hatua za kukata tamaa Kwenye mambo ya siasa.

Jokate amesema mwaka jana alitaka kukata tamaa kwenye maisha yake ya siasa kwani aliona giza mbele yake lakini hakufanya hivyo hii ni kutokana na kupokea maoni mengi kutoka kwa vijana ambao alikuwa anawashawishi kuingia kwenye siasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate ameandika:

Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu. Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi.

Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako.

Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu.
Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni ??”.

Esha: Jokate Usinichukie Mimi Ni Bendera Fuata Upepo

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameendelea kumtolea povu zito mwanadada Jokate Mwegelo huku akimsihi asimchukie kisa Ali Kiba kuoa kwani yeye ni bendera fuata upepo tu.

Siku chache zilizopita Esha alimtuhumu Jokate kwa kumchukia kisa na mkasa alihudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mkewe Amina Mombasa nchini Kenya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Esha amedai kuwa  amesikia kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba mwanamitindo huyo anamchukia kwa sasa kutokana na kuwa karibu na Kiba kwenye harusi yake na mrembo Amina Khaleef.

Kama ni kweli Jokate atakuwa ananichukia kisa mpenzi wake wa zamani Kiba kuoa kama watu wanavyosema, basi atakuwa ananichukia bure“.

Lakini pia Esha ameweka wazi kuwa sio kosa lake kwani yeye ni kama bendera fuata upepo anafanya alichokuwa anaelekezwa kwani haikuwa harusi yake:

Mimi ni kama bendera tu nafuata upepo kwa hiyo wa kumchukia ni Kiba mwenyewe aliyeamua kumuacha yeye na kuoa mtu mwingine, na wala si yeyote yule ambaye yupo karibu na Kiba”.

Tangu Ali Kiba Afunge ndoa aliyekuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo hajaposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii.

Esha Buheti Amlipua Jokate na Kudai Anaona Wivu Baada Ya Alikiba Kuoa

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kumtupia tuhuma nzito mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ baada ya kudai kuwa tangu amehudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na Amina mrembo huyo amekata naye mawasiliano.

Esha ni mtu ambaye ana ukaribu sana na familia ya Ali Kiba na hata kwenye harusi ya Ali Kiba alionekana mwanzo mwisho akishitiki kwani alienda hadi Mombasa.

Hapo nyuma kuna taarifa ilisambaa kuwa Esha ndiye aliyemtafutia mchumba huyo Ali Kiba (Amina) ingawa mwenyewe alishakataa na hata Ali Kiba na Amina waliweka wazi walikutana wenyewe Kwenye ndege.

Kwenye mahojiano na Shilawadu  Esha anadai kuwa tangu ahudhurie ndoa ya Ali Kiba basi Jokate kama kama kamkasirikia kwani zamani alikuwa anaangalia status zake WhatsApp lakini saivi ameacha.

Mimi na Jokate tukiongelea kuhusu kukutana basi tulikutana kama mara tatu tu lakini kama yeye ananichukia ni yeye tu lakini mimi siwezi kumchukia kwa sababu sio mimi niliyeoa aliyeoa ni Ali kiba, ingawa kabla alikuwa ana view status zangu lakini tangu niende Mombasa sijaona aki view tena Lakini sikuhangaika kuangalia kama ameniblock au vipi”.

Jokate hajaonekana aliposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii tangu harusi ya Ali Kiba hivyo pia hajajibu tuhuma hizi.

Jokate Akimbia Mitandao Ya Kijamii Baada Ya Ali Kiba Kuoa

Msanii na mfanyabiashara maarufu mitandaoni Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amepotea kabisa Kwenye mitandao ya kijamii tangu aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba alivyofunga ndoa.

Jokate na Ali Kiba walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini mwaka jana mwishoni habari zilisambaa kuwa wameachana ingawa hakuna aliyethibitisha taarifa hizo.

Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Khalef tarehe April  19 / 2018 Mombasa nchini Kenya na kiukweli Jokate aliandamwa sana na mashabiki juu ya ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Siku ya shughuli ya Alikiba Jokate aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na caption iliyosomeka; LoL (Laugh Out Loud). Post hiyo ya Jokate ilienda mbali sana baada ya watu kuhusisha na hatua aliyochukua Alikiba ya kufunga ndoa.

Sasa basi, tangu April 20, 2018 siku moja baada ya Alikiba kufunga ndoa Jokate hajaonekana katika mtandao huo wa Instagram, hivyo hivyo katika mtandao wa Twitter na Facebook, mashabiki wanahoji ukimya wake umesababishwa na nini?.

Ingawa na Jokate aliweka wazi siku yake ya birthday kuwa anategemea Kuolewa mwaka huu.

Mange Amvaa Jokate Baada Ya Ali Kiba Kuoa Mwanamke Mwingine

Mwanaharakati wa siasa Mtandaoni Mange Kimambi amemvaa Jokate na kumtolea povu zito baada ya aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Asubuhi ya Leo Ali Kiba Kumuoa mke wake Amina huko Mombasa nchini Kenya lakini Ex wake Jokate anashika headlines ambapo Mange amemjia juu Jokate huku akimcheka kuhusu hilo.

Mange amekuwa akiipinga ndoa hii kufanyika hivi sasa kwa hofu ya kwamba itazima haraka tu zake za Maandamano Lakini pia amekuwa katika vita na Jokate kutokana na Jokate kuwa chama tawala na alikuwa kiongozi.

Mange amemtolea povu zito Jokate huku akihusisha ndoa ya ALi Kiba ambapo kwenye ukurasa wa Instagram wa Jokate aliandika maneno haya:

Jokate Aonesha Mapenzi Yake kwa Watoto, ni Baada ya Kuwafadhiri Katika Soka

Mwanadada ambae siku za karibuni amekuwa akishindwa kutabirika kutokana na kujikita sana katika kutoa misaada katika jaii kwenye mambo mbalimbali ameibuka tena na kuwaonyesha watoto wa kiume hasa wanaopenda mpira kuwa yuko nao pamoja.

Jokate ambae aliungana na Shaffih Dauda katika hilo ameweza kumfadhiri na kutembelea baadhi ya familia za vijana ambao watashiriki Ndondo Cup mwaka huu  na kuwatia moyo wa kuendeleza vipaji vyao.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Jokate aliweka  baadhi ya picha akwa pamoja na  vijana wanaopenda soka na kuwepo pamoja na baadhi ya familia za vijana ho huku akiseamkuwa ameweza kumuunganisha kijana huyo na Shafih Dauda katika Foundation yake ya kukuza vipaji vya vijana katika soka ili kumfisha mtoto huyo katika daraja la soka analolitaka.

Jokate anaonyesha kuamua kutimiza aahadi yake aliyoiweka mapema mwaka huu kuwa kwa sasa anaamua kujikita zaidi katika kutoa huduma kwa jamii kwa sababu anaamini kuwa kuna watu wengi sana wanahitaji kuinuka hasa pale wanaposhikwa mikono.

jokate akiwa na kijana  hazzard ibrahim pamoja na Shaffih Dauda

akiwa na familia ya kijana aliyempa ufadhili

Jokate Aonyesha Mahaba Yake Kwenye Soka

Sio tu kwa sababu ni mwanamitindo basi ajikite huko, kumbe ukiachana na siasa na ujasiriamali bali pia mwanadada Jokate Mwegelo anapenda sana mpira na kwa kutibitisha ilo ameonyesha timu anayoipenda na pia mchezaji wa mpira anaemkubali katika soka.

Katika baadhi ya post zake Jokate alishawahi kusema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa taem ya arsenal lakini hakuwahi kusema wazi ni mwanasoka gani amekuwa akimkubali kati yao.Katika ukurasa wake wa instagram, Jokate ameandika kuwa anamkubali sana Ronaldo na kusema kuwa mwanasoka huyo anakipaji kikubwa kuliko Messi.

                               

 

 

 

Jokate Atumbuliwa Uongozi UVCCM

Mwanadada mrembo na mjasiriamli Tanzania, Jokate Mwegelo ametenguliwa uongozi katika chama cha mapinduzi, nafasi alikuwa ameteuliwa mwaka jana kuwa katibu Mwenezi wa uhamasishaji kwa vijana uvccm.

Utenguzi huo ulifanyika March 25 katika kikako cha dharura kilichofanyika jijini baada ya kamati kuu ya uvccm ikiongizwa na Denis James ambae ni mwenyekiti wake kuamua kumtoa uongozi huo dada huyo.

Hata hivyo mpaka sasa bado haijafahamikani kwa nini mwana dada huyo ametenguliwa cheo hicho, lakini kwa katiba na sheria zao viongozi husika wanayo mamlaka ya kufnya hivyo.

Ikumbukwe kuwa baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, Jokate aliweza kufanya shughuli nyingi zaidi za kijamii kupitia chama chake na alihaidi kufanya mengi zaidi.

Hasheem Thabeet Amkumbuka Ex Wake Jokate

Mwanamichezo anayecheza mpira wa kikapu ‘basketball’ nje ya nchi, Hasheem Thabit amemkumbuka aliyekuwa mpenzi wake mrembo Jokate kwa kumpa Zawadi siku ya birthday yake.

Hasheem alijzolea umaarufu baada ya kuanza kucheza basketball katika ligi ya NBA nchini Marekani miaka ya nyuma. Hivi sasa Hasheem anacheza basketball nchini Japan.

Hasheem na Jokate walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka mitatu na baadae kuweka wazi kuwa wameachana lakini Siku chache zilizopita ilikuwa ni birthday ya Jokate na Hasheem alimpa zawadi ya maua rose.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Jokate alianika zawadi hiyo aliyopewa na Ex boyfriend wake na kuandika maneno ya shukrani: