Kassim Mganga-Tusionee Wivu Mafanikio Ya Diamond

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kassim Mganga ameibuka na kumkingia kifua staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kuwataka watu wasimuonee wivu.

Diamond Platnumz anatajwa kuwa moja kati ya wasanii walioiweka Bongo fleva katika ramani ya kimataifa baada ya kufanya kolabo na Staa kutoka Naigeria Davido miaka Michache iliyopita.’

Mmoja kati ya wasanii ambaye amejitokeza na kumkingia kifua Diamond ni Kassim Mganga ambaye ameibuka na kuwataka Wasanii Wenzake na mashabiki kutomuonea wivu Diamond.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Kassim Mganga amefunguka haya kuhusu kipaji cha Diamond:

Tusimuonee wivu kwa sababu amefanikiwa sana, ila Diamond amebadilisha sana muziki wetu”.

Pamoja na kwamba Diamond sio mmoja ya wasanii ambao waanzilishi wa muziki wa Bongo fleva lakini anatajwa kuwa msanii ambaye amekuza na anaendelea kuikuza Bongo fleva.

Ndoa Ya Dogo Janja na Irene Uwoya Haijavunjika- Kassim Mganga

Msanii wa muzik wa Bongo fleva kutokea Tip Top Connection Kassim Mganga ameibuka na kudai ndoa ya staa wa Bongo fleva Dogo Janja na Mkewe Uwoya haijavunjika.

Kassim Mganga ambaye alikuwa mmoja kati ya watu wachache waliohudhuria ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Mwaka jana mwishoni amesema hana taarifa ya ndoa hiyo kuvunjika.

 

Kwenye moja ya Interview alizofanya hivi Karibuni katika kituo kimoja cha habari Kassim amefunguka na kudai kuwa hajui kama Ndoa hiyo imevunjika kwa kuwa hajapata taarifa Rasmi.

Sina taarifa ya kuvunjika kwa ndoa kati ya Dogo Janja na Irene Uwoya ninachojua bado wako pamoja mpaka hivi sasa”.

Lakini pia Kwenye Mahojiano hayo Kassim amewataka watu wasimuonee wivu Diamond kwa ajili ya mafanikio anayoyapata kwani kiukweli amebadilisha sana muziki wa Bongo fleva.

Kassim Mganga Awataka Mastaa Wote Wanaoishi Na Wapenzi Mwezi Huu Waache

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Kassim Mganga amewatolea povu wasanii au mastaa wote ambao wanaishi na wapenzi wao mwezi huu waache.

Ukiwa ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo waislamu wote duniani wanafunga kwa kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu, wanahimizwa kufanya matendo mema.

Kassimu Mganga amewataka mastaa wenzake wauheshimu mwezi hasa kwa wale ambao bado mpaka sasa hivi wanaendelea kuishi na wanawake/ wanaume ambao sio wake/ waume zao Kwenye mwezi huu.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Kassimu alifunguka haya:

Sio mimi ninayesema haya lakini ni agizo la Mwenyezi Mungu kwaiyo inapokuwa halitekelezwi inakuwa haipo sawa kwani kuna umuhimu mkubwa wa kuweza kuheshimu maandiko hasa huu mwezi ingawa najua wengi wetu bado vijana na wengi bado hawajaoa kutokana na kwamba hawajajipanga na wengine wakati bado lakini unaweza ukaupisha Kwanza mwezi ukapita baada ya hapo ukaendelea”.