Linex- Asilimia 90 Ya Wimbo Wa Leka Dutigite Ni Wangu

Msanii wa Bongo fleva Linex ‘Sunday Mjeda’ ameibuka na kudai kuwa asilimia 90 ya wimbo maarufu ulioimbwa na wasanii kibao wa kikundi cha Kigoma All star.

Wimbo huu ulikuwa maarufu sana kipindi cha nyuma na basically kilichotokea kwa watu ambao hawakumbuki ni kuwa kikundi cha wasanii kadhaa ambao wote ni watu wa Kigoma walikuja pamoja na kufunga nyimbo ya kuimusifia mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya wasanii waliounda kikundi cha Kigoma All star ni pamoja na Ali Kiba, Diamond, Ommy Dimpoz, Rachel, Linex, Baba Levo, Banana Zorro, Linah, Chege, Queen Darleen, Mwasiti, Makomando.

Kwenye mahojiano aliyofanya na TV E, Linex ameibuka na kudai yeye ndiye mmiliki wa wimbo Ule kwa asilimia 90 na aliwapa wasanii wengine waimbe wimbo Ule kwa sababu wengi wao walikuwa hawajui mitaa ya Kigoma:

Kigoma wimbo sio wa kundi ni wa kwangu mimi nikaamua kuwapa watu, tufanye wote..

Kwa hiyo ule ni wimbo wangu na asilimia kubwa ya ule wimbo mimi ndio nimechora kwa sababu asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa wameimba kwenye ule wimbo walikuwa hawajui ule mtaa ukoje zaidi ya Baba Levo na Chege”.