Linex Ajutia kutoonana na Godzilla Kabla ya kifo chake.

Msanii Linex Sunday Mjeda amefunguka na kuonyesha jinsia alivyoguswa na msiba wa msanii Godzilla hasa baada ya kujutia uamuzi wake wa kutotaka kuonana nae kabla ya kifo chache.

Linex anasema kuwa , msanii mwenzake huyo alitaka kuonana siku kama tatu kabla ya kifo chake lakini alimuomba wakutane siku nyingine kwa sababu alikuwa na kazi nyingine hivyo wakapanga kukutana siku nyingine lakini cha ajabu ni kwamba amefariki kabla hata hawajakutana.

Linex anasema “Niliongea na zilla wiki moja kabla na alinitaka tukutane, wiki iliyopita alinipigia tena akaniomba nionane nae alipolakini kutokana na ratiba zangu nilishindwa kukutana nae , sijui alitaka kuniambia nini.Mungu ampumzishe mahali salama. “

Kifo cha msanii huyo kimetia simanzi sana hasa kutokana na kifo chake cha ghafla kilitomuacha kila mtu akishanga.

 

Linex Afunguka Kutomuona Mtoto Wake Kwa Miaka Minne

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Sunday Sangu maarufu kama Linex ‘Sunday Mjeda’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mzazi mwenzake amempora Mtoto Wake.

Linex ameeleza kisa cha mwanamke ambaye alikuwa Mpenzi Wake na kuzaa naye kumgeuka na kumchukua Mtoto wao ambaye hajamuona kwa miaka kadhaa sasa.

Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa Wikienda , Linex alisema kuwa hajamuona mtoto wake huyo wa kiume takribani miaka minne iliyopita tangu aliponyang’anywa nyumbani kwa mama yake.

Yaani kinachoniuma mtoto wangu ana miaka 12 sasa, najua angekuwa na furaha sana ya kuwa na mimi lakini mpaka sasa sijui alipo wala pakumpata maana mama yake mpaka simu kabadilisha nasikia tu anaishi Kahama, nina hamu sana na mwanangu”.

Inadaiwa sakata hilo lilitokea Baada ya Linex na mzazi mwenzake kuvurugana ndipo mwanamke huyo alibeba kilicho chake na kuondoka na Mtoto wao.

Linex Alizwa Kisa Mapenzi,Akumbua Mengi ya Nyuma na Mpenzi Wake.

Mwanamuziki wa muda mrefu Linex Sunday Mjeda amefunguka na kuonyesha jinsi kumbukumbu ya mapezni ambavyimekuwa ikumuumiza kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu alipoachana na mwanamke aliyekuwa akidhani kuwa ndie atakuwa mke wake wa ndoa.

Miaka miwili iliyopitalinex aliwahi kutambulisha wimbo wake ambao aliyekuwa video queen ambae alivaa shela la harusi alikuwa ndie mpenzi wake na walikuwa wamepanga kufunga ndoa, lakini kwa sasa hawapo tena kitu ambacho mpka sasa ,linex amekuwa akikikumbuka na kumuumiza sana.

katika ukurasa wake wa instagram linex aliandika”i wish haya yasingekuwa mapito daah saizi si ningekuwa zangu mme wa mtu  na mimi kama wenzangu…daah i miss rica and still love you.”

Linex anazidi kuumiza pale anapoona wasanii wengine wenzake wakiwa wanasonga mbvele na kufunga ndoa na maisha yakiwa yanaendelea.

Linex- Asilimia 90 Ya Wimbo Wa Leka Dutigite Ni Wangu

Msanii wa Bongo fleva Linex ‘Sunday Mjeda’ ameibuka na kudai kuwa asilimia 90 ya wimbo maarufu ulioimbwa na wasanii kibao wa kikundi cha Kigoma All star.

Wimbo huu ulikuwa maarufu sana kipindi cha nyuma na basically kilichotokea kwa watu ambao hawakumbuki ni kuwa kikundi cha wasanii kadhaa ambao wote ni watu wa Kigoma walikuja pamoja na kufunga nyimbo ya kuimusifia mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya wasanii waliounda kikundi cha Kigoma All star ni pamoja na Ali Kiba, Diamond, Ommy Dimpoz, Rachel, Linex, Baba Levo, Banana Zorro, Linah, Chege, Queen Darleen, Mwasiti, Makomando.

Kwenye mahojiano aliyofanya na TV E, Linex ameibuka na kudai yeye ndiye mmiliki wa wimbo Ule kwa asilimia 90 na aliwapa wasanii wengine waimbe wimbo Ule kwa sababu wengi wao walikuwa hawajui mitaa ya Kigoma:

Kigoma wimbo sio wa kundi ni wa kwangu mimi nikaamua kuwapa watu, tufanye wote..

Kwa hiyo ule ni wimbo wangu na asilimia kubwa ya ule wimbo mimi ndio nimechora kwa sababu asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa wameimba kwenye ule wimbo walikuwa hawajui ule mtaa ukoje zaidi ya Baba Levo na Chege”.

Msanii wa Bongo Fleva Linex adai kuwa kiki inaua muziki

Linex, msanii maarufu wa bongo amefunguka na kusema kuwa mtindo wa kupa mziki kiki unapoteza ladha na focus ya mziki nchini Tanzania.

Akiongea na waandishi wa global punlishers Tz nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es Salaam, Linex amesema kuwa imekuwa kama trend ya wasanii wa Bongo kutokea na skendo wakati wanpotaka kuachilia mziki siku hizi. Kulingana na yeye vitendo kama hivi havina maana kama msanii anaamini kazi yake ni nzuri.

Msanii huyu aliendelea kusema kuwa mashabiki ndio wanaoamua kama projects za wasanii ni za kuvutia au la. Linex alisema,

“Nachoweza kusema turudi kushabikia muziki mzuri, tuache kushabikia skendo. Nachokiona hapa muziki unapotea kabisa”

Ata hivyo hit maker huyo wa Kiherehere aliwasihi mashabiki kuwa makini na kufuatilia muziki wa maana badala ya kushabikia skendo za watu maarufu.