Lizer amtaja msanii ambaye anafurahia kufanya kazi naye Wasafi

Muziki wowote wa Wasafi ukianza mara mingi utamsikia mwanadada akisema ‘ayo Lizer’ lakini wengine hawafahamu kuwa yeye ndiye mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Wasafi Records.

Hivi karibuni Lizer alimtaja msanii wa WCB ambaye yeye hufurai kufanya kazi naye. Akizungumza kwenye interview Lizer alisema kuwa Rayvanny ni msanii ambaye ameweza kufanya kazi naye bila matatizo yoyote.

Aliendelea kwa kusema,
“Msanii yoyote anayejua mimi nina enjoy sana kufanya naye kazi, ukimuelekeza fuata hiki anafuata. Lakini naweza kusema kwa kuwa Raymond ndiye msanii aliyegundua kitu kilichopo ndani ya Lizer huwa nina enjoy naye zaidi kwasababu ndiye msanii ambaye nilitoka naye.”