“Naenda South Africa Kama Kazi Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra ametoa povu zito na kusema anaweza kwenda South Africa muda wowote akitaka kwenda kuwaona wajukuu zake na hawezi kukatazwa na mtu.

Mapema mwaka huu Zari the Bosslady alimpiga kibuti cha maana aliyekuwa mpenzi wake na  Baba watoto wake supastaa wa Bongo fleva Diamond siku ya Valentine’s baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Baada ya kuachana Diamond alienda South Africa kwa ajili ya maandalizi ya Albamu yake lakini cha ajabu ni kwamba hakufika kwenye nyumba aliyonunua aliyokuwa anaishi na Zari na watoto na Tena hakufika hata kwenda kuwaangalia watoto wake.

Baada ya sakata hilo kutokea habari zilianza kusikika kuwa Diamond na familia yake na mama yake mzazi hawatakaribishwa tena kwenye nyumba ya South Africa hasa kwa sababu wamejenga ukaribu na adui namba moja wa Zari, Wema Sepetu.

Siku ya jana Bi. Sandra alitoleana povu na shabiki baada ya kumuuliza kwanini hapendi kumposti mjukuu wake wa Hamisa au anamuogopa Zari kwa sababu hataruhusiwa tena kwenda South Africa kuwaona wajukuu wake? Basi bwana povu la Mama Diamond lilikuwa hivi:

South Africa naenda kama kazi kwa taarifa yako na siwezi kukatazwa na mtu yoyote”.

Zari alishasema Kwenye Interview aliyofanya na BBC Swahili kuwa hana tatizo na familia ya Diamond kwani muda wowote wakitaka kuona watoto wao wanakaribishwa hata Diamond akitaka kuona wanaye.

“Wewe ni Wangu” Mama Diamond Amfungukia Mumewe

Ikiwa jana ilikuwa ni siku ya Valentine’s Day au maarufu kama Siku ya Wapendanao duniani watu mbali mbali hawakuwa nyuma kuonyeshana mapenzi na Baba wa Kamba wa msanii Diamond Platnumz alimgungukia mkewe.

Ingawa siku ya jana haikuwa nzuri sana kwa Diamond kwani alipigwa kibuti na mama watoto wake mrembo Zarinah Hassan baada ya kumtuhumu kwa tabia ya kupenda michepuko.

Lakini ilikuwa siku nzuri kwa mama mzazi wa Diamond anayejulikana kama Bi. Sandra ambaye siku ya jana alirushwa na mumewe Maisara Abdul Shamte ambaye alimfungukia mazito yaliyo moyoni mwake.

Ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamte alidai kuwa bado anakumbuka siku aliyomuona kwa mara ya kwanza kwa maana ilikuwa ni siku ya furaha kuliko siku zote katika maisha yake alimuandikia Mama Diamond ujumbe huu katika kumtakia Valentines njema:

I still remember the day i met you and smile because it was the happiest day of my life.. meeting you was like listening to the song for the first thing and knowing it would be my favorite, Happy Valentines”.

Baada ya kupewa ujumbe huu na mumewe Mama Diamond hakuona hiyana kujibu kwani alimjibu mumewe kwa kuandika “You are mine, happy Valentines “. Akimaanisha kuwa wewe ni wangu na Valentine njema.

 

Tangu Mama Diamond aolewe  na mumewe huyu ambaye ni Serengeti boy kumekuwa na skendo nyingi za kuwa ni tapeli na kuwa hapatani na mtoto wake wa kambo Diamond habari ambazo familia imekuwa ikizikataa.

 

Mama Diamond Amkingia Kifua Wema.

Mama mzazi  wa msanii Diamond Platinumz amekuwa ni mzazi anakuwa mstari wa mbele katika kumsapoti mtoto wake na hata kufikia hatua ya kugombana na mashabiki wake katika mitandao pale anapoona kuwa mtoto wake anakuwa ameandamwa sana.

Wikiendi hii kulikuwa na party ya kumtambulisha msanii mpya katika kundi  la wasafi ambapo mwandada Wema Sepetu alikuwa ameharikwa katika party hiyo.Swala la uwepow a mwandada huyo lilizua gumzo kubwa kwa mashabiki wake na hata kuanza kumtukana Wema na familia ya Diamond kwa kusema kuwa wamekuwa wakisapoti uchafu anaofanya ndugu yao.

Kwa kuonyesha kuwa hajali maneno hayo ya watu mama Diamond alipost moja ya video zilizosambaa sana katika mitandao ambayo ilikuwa ikiwaonyesha Wema na Diamond wakiwa katika muonekano wa kimahaba na kuandika kuwa watu waongee tu lakini wao wanapiga hela.

 Katika ukurasa wake wa instagram mama yake diamond alionyesha kuwa aamekuwa hakiyaona maneno yao lakini wao wanaingiza hela kupitia amneno yao.kwa herufi kubwa nyie hongeeni,chambeni cc tunapiga hela.

Ikiwa bado kuna lile fukuto la Zari kumwambai mAma Diamond wahame madale na kwamba wamuachie Diamond guest house ikiwa ni dongo kubwa kwa Doiamnd , hakuna aliyetaka kuamini kuwa mama Ziamond angeweza kuandika hivyo kwa kumtetea diamond na mtoto wae ilhali wengi waliamini kuwa mama huyo yuko upande wa zari ambae kwa sasa inasemkana kuwa hana mahusiano mazuri na mzazi mwenzie Diamond Platinumz.

Mume Wa Mama Diamond Kuwajibu Wanaomsema Vibaya

Ikiwa ni muda mchache nyuma tangu mamam mzazi wa msanii mkubwa nchi Diamond Platinumz kuthibitisha kuolewa na mwanaume ambae wengi wamekuwa wakisema kuwa kijana huyo ni mdogo sana kwa mama huyo, mwanaume huyo ameamua kujibu tuhuma hizo ambazo amekuwa akibebeshwa katika mitandao.

Mwanaume huyo anaejulikana kwa jina la Rally na Mama Diamond walionekana katika baadhi ya picha za pamoja wakiwa katika ndege ikisemekana kuwa walikuwa wakielekea Afrika ya Kusini kwa ajili ya honeymoon yao baada ya kufunga ndoa muda wa wiki chache zilizopita.

Hata hivyo mama wa msanii huyo alishawahi kuwajibu watu kuwa mwanaume huyo hana udogo wowote hivyo watu wawaache kama walivyo kwa kuwa wanapendana  ingawa katika mitandao watu wamekuwa wakisema kuwa ni pesa ndio zilizomfanya mwanaume huyo ajiingize kwenye mapenzi na mama Diamond.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram,Rally aliweka picha akiwa na mke wake huyo huku akiandika ujumbe kuwa wanaosema kuwa ana umri mdogo, umri kwake sio shida wanachojali wao ni kuwa wanapendana na hiyo kwao inatosha.

ndoa sio umri ni makubaliano baina ya watu wawili na Allah hutia mkono wake ,mimi sio wa kwanza alianza  mtume S.A.W , Allah atuujalie kwenye maisha yetu mapya @mama dangote #honeymoon #SouthAfrika.

Wawili hao wamekuwa wakioneka wakiweka picha za pamoja wakiwa south afrika waki-enjoy maisha yao baada ya kufunga ndoa.

Mama Diamond Athibitisha Kuolewa

Mama wa msanii mkubwa wa bongo fleva nchini na nje ya nchi Diamond platinumz   anaejulikana kama BiSandra amethibitisha kufunga ndoa  hivi karibuni.Mama huyo anasema kuwa kwa muda mrefu walikuwa wakisema amekuwa akionekana na mwanaume akitoka nae na kusemekana kuwa ni mpenzi wake basi ni kweli kuwa mwanaume huyo ni kweli  ndie aliemuoa kwa sasa.

Akionesha hadi pete  ya ndoa kidoleni kwake , mama huyo anasema kuwa ni kweli ameolewa na wanaosema kuwa mwanaume huyo ni mdogo kwake wamuache kwa sababu angekuwa mdogo asingeweza kuoa , lakini kwa sababu umri wake unaruhusu ndio maana ameweza kuoa.

Nimeolewa na mwanaume yule yule ambae walikuwa wanamsema katika mitandao kwa sababu ndio nilimpenda,wanaosema mdogo anaudogo gani angekuwa mdodgo asingeweza kunioa.

Hata hivyo mama huyo anasema kuwa kwa sasa watu wategemee kuona mdogo wake na Diamond anakaribia kuja,kwa sababu watu wanataka mdogo basi na yeye atamuongezea Naseeb mdogo wake wa mwisho.

Akiongelea posti ambazo amekuwa akizituma huku zingine zikiwa zinasheheni mambo ya ugomvi na umbea umbea mama huyo amesema kuwa anaamua kuweka posti hizo ili kuweza kusisimua watu wanaomfuata waweze kuendelea kumfuata na kuongea mashabiki kwa sababu ustaa ndio unawafanya wao kufanya hivyo.