Mama Kanumba Adai Anaogopa Maneno Ya Kejeli Kutoka Kwa Lulu

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ amedai kuwa anahofia Elizabeth Michael ‘Lulu’ atamtolea maneno ya kejeli pindi atakapotoka jela.

Miezi michache iliyopita Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.

Tangu Lulu amefungwa Mama Kanumba amekuwa akiongea mambo kadhaa kuhusu Lulu ambaye miaka michache nyuma alikuwa hana uhusiano naye mzuri sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Mwanaspoti, Mama Kanumba amefunguka na kudai kuwa hofu yake kubwa ni Lulu kumezeshwa maneno akitoka kuhusu na kuishia kumtolea maneno ya kejeli.

Mtoto wangu huyu anaweza kurudi mtaani na kushikwa masikio tena na watu kunifanyia vibweka kama alivyofanya awali, wala asithubutu wala kujihangaisha kwa kuwa iliyomshtaki ni Jamhuri hivyo anapaswa kuniheshimu. Hakuna neno lililoniuma kama siku aliyonipigia na kuniita kubwa jinga huku akiniambia haogopi polisi wala mahakama”.

Lakini pamoja na hayo Mama Kanumba amesisitiza kuwa hana bifu na Lulu wala kinyongo na atakuwa tayari kumtembelea jela kumsalimia kama ndugu zake watakuwa tayari.

 

Mama Kanumba Aonyesha Wazi Alivyochukizwa na Matendo ya Lulu .

Mama wa marehemu Steven Kanumba ambae alikuwa moja ya wasanii wakongwe, maarufu na waliokuza  tasnia ya filamu bongo ameonyesha hasira zake za kuchukizwa na msanii Lulu Michael ambe ndie alimuua mtoto wake huyo bila kukusudia  na kupewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, hukumu iliyotoka mwaka huu mwezi Novemba huu tareh 13.

Akitoa madukuduku yake kuhusu Lulu Michael mama yake na marehemu anasema kuwa hakuwahi hata kujua hata siku moja kuwa mwanae Steven alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Lulu na kwa sababu kanumba alikuwa msiri sana.

Hata  hivyo mama huyo anasema kuwa kwa mara ya kwanza yeye kukutana na Lulu ilikuwa katika msiba tu na  baada  ya hapo Lulu alipelekwa rumande na baada ya kurudi huku alijua kabisa kuwa mashabiki wa Kanumba watakuwa na hasira na yeye kutokana na kumuua msanii wao kwaiyo gia aliyoamua kuingia nayo ni kuja kwake na kumuomba msamaha na baada ya kumaliza shida zake akaondoka na kuanza kunitusi.

watu wanashindwa kuelewa kuwa Elizabeth ni msanii tu, na alikuja kwangu kwa sababu alijua kuwa watu watakuwa na hasira nae kwaiyo akaja kuniomba msamaha, alikuja nyumbani kwangu na mamake akafanya mazingara yake akayafanya na akaondoka.

Lulu alikuja kwangu akaja kujipretend tu, alivyoamliza akaondoka zake,baada ya miezi miwli akaanza kunitukana na kuniundia tume huku kwenye mitandao ya kijamii na kunitukana sana.Nakumbuka lulu aliwahi kunitukana kwenye simu na kuniita kubwa jinga mimi , akasema yeye haogopi polisi.

Mama Kanumba anaendelea kuelezea kuwa hata baada ya miaka kadhaa kupita , ambapo ilikuwa tarehe ya marehemu kufariki, Lulu alifanya party kubwa sana na mashoga zake bila kuja hata kuangalia kaburi.

Tarehe 12,April 2015,alifanya party kubwa sana na kuwalika watu mbalimbali huku akiniacha mimi nililia peke yangu.Sidhani hata kama alikuwa anaenda hata kaburini, na hata kugombana kwetu hakuusiani na pesa, I swear upon God,Lulu hakuwahi kunipa hata pesa kidogo zaidi ya kunilipa pesa yangu baada ya kucheza muvi ambayo ilimpatia tuzo huko Nigeria inayoitwa Mapenzi ya Mungu.

Akiendelea kusema kwa uchungu katika kipindi cha Shilawadu, Mama Kanumba anasema kuwa anachojua ni kwamba washauri waliokuwa karibu na lulu walikuwa wanampoteza na walishindwa kutambua kuwa damu ya mtu huwa haipotei hata kidogo.Lakini pia amesema kuwa  kuna watu katika mitandao ya kijaii ambao wamekuwa wakijifanya ni yeye , amesema kuwa yeye hajiusishi na mitandao ya kijamii.

Lakini maneno hayo hayakuishia hapo tu, katika mahojiano mengine tena yaliyofayika juzi usiku ambapo mama huyo alikuwa amealikwa katika uzinguzi wa filamu ya Zero Player , iliyochezwa na wasanii mbalimbali akiwemo Hamisa Mobeto, mama huyo aliongelea tena swala la Lulu na kusema kuwa  hawezi  kwenda kumuona Lulu jela mpaka kwanza aongee na Mungu wake ndioe haende huko