Masanja Mkandamizaji Amuita Kanye West Chizi

Muigizaji wa Vichekesho Bongo ambaye hivi sasa amegeukia kuwa Mchungaji Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amejikuta akimtolea povu zito Rapa kutoka Marekani Kanye West.

Sakata hilo lilianza pale ambapo Msanii huyo kutoka Marekani ambaye anajulikana kwa vituko vyake aliandika Kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa:

We are Gods’ akimaanisha, ‘Sisi ni Miungu“.

Baada ya Kanye kuandika maneno hayo aliwachanganya mashabiki wengi ambao ni wacha Mungu akiwemo Masanja ambaye alishindwa kujizuia na kumwagia povu zito na kumuita chizi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Masanja aliandika:

Huwaga una umama sana.”“Acha kuvuta bangi.”“Wewe ni kenge.”

 

Masanja Mkandamizaji Ajitapa Kuwa na Pesa Zaidi Ya Bakhresa

Msanii wa comedy na Mchungaji Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ameibuka na kudai kuwa ana pesa nyingi Kuliko mfanyabiashara tajiri Bongo, Bakhresa.

Kwenye mahojiano na Kituo cha Clouds FM, Masanja amesema hawezi yakataa yale mazuri yanayozungumza na watu juu yake kwa kuwa midomo ya watu inanguvu sana kwaiyo anaamini kuwa yeye ni tajiri.

Kwa sababu ni jambo jema , unajua mtu akikwambia kuwa wewe unaoongoza kwa utajiri usikatae, ukikataa utakuwa umejikosea kwa sababu kitabu cha Mungu cha Biblia kinatufundisha nguvu iliyopo kwenye kinywa chako, kwahiyo mtu akisema kuwa mimi ni tajiri nitasema kuwa mimi ni tajiri ile mbaya na kwanini nisiwe tajiri wakati biblia inasema fedha na dhahabu ni mali ya baba yangu ninayemtumikia kwahiyo mimi kutumia au kumiliki vitu vya baba nimebarikiwa, ukiambiwa wewe ni tajiri usikae, ukikataa ina maana umeukataa utajiri’’.

Najisikia vizuri sana mtu akiniita tajiri na ulimi wangu lazima ukiri vitu vizuri kwahiyo ni kweli kabisa kama ambavyo wanasema mimi ni tajiri ile mbaya yaani Bakhresa anasubiri”.

Lakini pia Masanja Aliyah’s utajiri wake ikiwemo magari na majumba:

Nikwambie utajiri hautauhesabu kwa sababu ya kumiliki mjengo, ukimiliki mjengo ni sehemu tu ambayo Mungu amekubarikikwamba uwe unaweza kuwa na sehemu ya kuishi katikati ya watu wanaopanga, akikupa gari amekuhurumia tu kuepukana na mzunguko mingi ambayo ungetembea kwa miguu sasa unaweza kutumia usafiri kukurahisishia shughuli, utajiri wangu ni kuwa Yesu ambaye ana kila kitu, ukiwa na Mungu una kila kitu kwahiyo mimi ni tajiri zaidi matajiri kwa sababu nina kila kitu’’.

Masanja Atetea Kitendo Cha Diamond Kuvaa Kikuku na Kudai Mungu Anaruhusu Kwenda na Fasheni

Mchekeshaji maarufu Masanja Mkandamizaji ambaye sasa amegeukia Injili na kujiita Mchungaji amefunguka na kumkingia kifua Diamond Platnumz kwa kitendo chake cha kuvaa kikuku.

Masanja amefunguka Kwenye mahojiano na Masanja Tv, na kudai kuwa kwa imani yake ya Kikristo kuvaa kikuku mguuni kwa mwanaume sio dhambi kwani inahesabiwa kama cheni yoyote unayoweza kuvaa na Mungu hajakateza watu kwenda na fasheni.

Kama mchungaji nasema mwanaume kuvaa kikuu mguuni sio dhambi, lakini nikawaambia kwenye maadili kuvaa kikuku unamaanisha nini? soo shinda ikiwepo kwenye maadili haina maana ni dhambi watu wanadhani kuwa vitu wasivyovipenda wao kuviona, vitu ambavyo sio maadili mazuri wanafikiri kuwa ni dhambi kuna tofauti sana juu ya hivyo vitu. Kwa hiyo narudia tena kusema mwanaume kuvaa kikuku katika Biblia sio dhambi”.

Lakini pia Masanja amesema Cheni ni cheni tu na hakuna mtu wa kumpangia binadamu mwenzie sehemu ya kuvaa na hakuna cheni ya mwanamke zote ni cheni tu.

Kikuku ni cheni tu, hakuna cheni ya kivulana wala cheni ya kike cheni ni cheni na ukiamua kuvaa mkononi au shingoni sio dhambi kufikiria vibaya mtu kuvaa cheni mguuni huo ni uchizi wa hali ya juu. Kwahiyo kama kuna mtu anaona kuvaa micheni miguuni ndio raha muacheni avae”.

Pia Masanja amesema kuwa Mungu hajamuumba binadamu aokoke ili awe nyuma ya fasheni bali alimuumba aendane na fasheni.

Niliokoka Kwa Sababu ya Kuogopa Kifo:- Masanja

Aliyekuwa mchekeshaji wa Kundi la ‘Ze Comedy’ Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ambaye kwa sasa ni mshereheshaji na mchungaji, ameibuka na kusema kuwa kuogopa kifo ndio sababu iliyomfanya aokoke.
Masanja ambaye pia ni baba wa mtoto mmoja aliyasema hayo hivi karibuni mara baada ya kukutana na paparazzi wetu katika harakati za kuuaga mwili wa mtoto wa Muigizaji wa Filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’ aitwaye Patrick maeneo ya Leaders, Kinondoni jijini, Dar.
Msanii huyo alisema kuwa, aliokoka kwa sababu ya kuogopa kifo na kwamba katika vitu ambavyo hapendi kuvisikia katika maisha yake ni habari zinazohusiana na kifo kwani huingia woga sana.

Niliokoka kwa sababu ya kuogopa kifo na mtu akitaka tugombane azungumzie habari za kufakufa yaani huwa sipendi hata kuzisikia natamani kuishi tu na kwasababu ninaimani ukimfuata Yesu unakuwa mikono salama ndio maana nimechagua njia hiyo,” alisema Masanja.