Beka Fleva: Mbosso Hajanitetemesha, Aslay Nayeye Acha Tushindane

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya Kiben10 amefunguka na kusema hajatetemeshwa na ujio mpya wa msanii Mbosso kutoka WCB lakini pia Aslay atashindana naye tu.

Beka fleva, Aslay, Mbosso na Bella waliunda kundi la Yamoto band waliojipatia umaarufu miaka ya nyuma lakini baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa kundi hilo liliishia kuvunjika na kila mmoja alishika njia yake na kuanza solo careers.

Wasanii wote wamekuwa wakifanya vizuri na kukubalika na kila mmoja wao amekuwa akidai hakuna uhasama kati yao na kila mmoja anamtakia heri mwenzake na mafanikio.

Lakini pia Beka fleva ameongelea tetesi za yeye kukasirikia mafanikio ya Mbosso kusainiwa WCB na hivyo kusababisha kutohudhuria halfa yake ambapo amedai alichelewa kupata taarifa za shughuli hiyo hali iliyopelekea kushindwa kufika.

Beka fleva amefunguka kuwa alivyoona Utambulishi wa Mbosso kwenye bonge la hoteli la Hyatt Regency na baadae kijamii uwanjani Mwembeyanga hakutetemeshwa hata kidogo ndio kwanza alifurahi kuona mafanikio ya mwenzake lakini pia amesema anafurahia ushindani wake na Aslay kwani unaleta mziki mzuri.

Mbosso Wa Mkubwa na Wanawe Asainiwa chini ya Label ya Diamond

Mwanamuziki Marombosso au maarufu kama Mbosso wa Mkubwa na wanawe amekula shavu la maana baada ya kusainiwa chini ya label maarufu Wasafi Classic (WCB) Iliyo chini ya mwanamuziki Diamond Platnumz.

Ikiwa Leo ni siku yake ya kuzaliwa ya Mbosso Raisi wa label hiyo ya Wasafi Diamond alitumia fursa hiyo kutangaza habari hii ambapo aliandika;

“Happy birthday Mbosso words can’t express how big of fan of hours I am i can’t wait to officially introduce you as a member of WCB I can’t wait for the world to hear the special and unique talent that you have that makes me be your number one fan, Kheri ya kuzaliwa mbosso maneno kamwe hayatoweza kutosha kukueleza ni kwa kiasi gani mimi ni shabiki wako…Heshima na busara hunifunza mengi nasubiri kwa hamu siku ya utambulisho wako rasmi kama msanii na mwanafamilia wa WCB, Vilevile ulimwengu upate kusikia kipaji kingine kutoka Tanzania. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu Upendo na furaha”.

Mbosso ataungana na wasanii walio ndani ya WCB Kama Mr. lavalava, Harmonize, Rich Mavoko, RayVanny, na wengineo wengi.