” Nina Mimba ya Rayvanny” Reality TV staa wa Kenya akiri

Watoto ni baraka kutoka kwa mungu na kila mmoja huja na sahani yake. Basi, Rayvanny anawatarajia watoto wawili mwaka huu kutoka kwa mpenzi wake Fahyma na mwanamke mmoja kutoka Kenya aitwaye Mishi Dorah.

Kulingana na ubuyu mjini Rayvanny na Mishi Dorah walikutana Instagram na kulingana na Mishi wakati huo Rayvanny alikuwa anamtaka awe kama Video vixen wake.

Mishi Dorah

Lakini baada ya kujuana miezi kadhaa wawili hawa walianza kuingiana kimapenzi na hivyo ndivyo Mishi alivyopata mimba.

Mishi ambaye ana watoto wawili alisimulia Rayvanny alivyokuwa akimsihi amzalie na hivi sasa ametambua kuwa ana mimba ya muimbaji huyu ambaye amekuwa akimkana mitandaoni.

Kwa kweli hakuna anayejua kilichotokea kati ya wawili hawa na yupi anasema ukweli au uongo. Hata hivyo ikiwa Mishi ana mimba basi Rayvanny atabarikiwa na watoto wawili mwaka huu