Mzee Majuto Aomba Msaada wa Matibabu Nchini India

Msani wa maigizo nchini Mzee Majuto anaomba msaada wa kuomba kuchangiwa ela kwa ajili ya matibabu yake anayopaswa kufanyiwa nchini india haraka iwezekanavyo,Mzee Majuto ambae alikuwa akisumbuliwa na tezi duma na kisha kufanyiwa upasuaji January mwaka huu alikimbizwa tena hospitali hivi karibuni baada ya kuonekana kuwa hali yake inaaanza kubaidlika baada ya kidonda alichokwa amefanyiwa upasuaji kushindawa kufunga.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi imebainika kuwa njia salama kabisa ya yeye kuendelea kutibiwa ni kwa kupoatawataalamu zaidi nchini india hivyo mzee majuto na familia yake wameomba msaada kwa watanzania ili kupata fedha kwa ajili ya shuguli hiyo.

Akiongea kwa kuthibitisha hilo, mtoto mkubwa wa Mzee Majuto amesma kuwa baba yake anahitaji fedha ili aweze kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, kiongozi ambae amekuwa akiwakilisha wasanii wengine, steve nyerere anasema kuwa huu ndio wakati wa watu kujitokeza na kutoa misaada yao na sio kusubiri mpaka mtu apate matatizo makuwa zaidi  au awe amekufa ndio watu waanze kujitokeza kwa kutoa misaada na kuposti katika mitandao kuonyesha masikitiko yao wakati alipokuwa hai walishindwa kumsaidia.

Mzee Majuto Bado Mgonjwa,Tumuombee:- Mke wa Majuto Awaomba Mashabiki

Mke wa mchekeshaji maarufu nchini Mzee Majuto anaejulikana kama Aisha  Yusuf ameowaomba wasanii, na mashabiki wake kwa ujumla kumuombea sana mzee majuto kutokana na hali yake kuwa mbaya kwa sasa baada ya kufanyiwa upasuaji na kidonda kushindwa kupona.

Hata hivyo aisha ansema kuwa mzee majuto alifikishwa hospitali hapo akiwa na hali mbaya sana wikiendi hii lakini anashukuru mungu kwa sababu kidogo hali yake imebadilika na kuwa nzuri.

Ninachowaomba tu watanzania, wamuombee mume wangu ili aweze kupona na pia tutoke hospitali kwa sababu akilala na mambo yote yanalala.

Mke wa Majuto anasema kuwa mzee majuto amefanyiwa upasuaji wa mara ya pili wa henia baada ya kuwa wanatafuta tiba ya ugonjwa mwinhine na ndipo walipogundua tatizo hili la tezi dume , walipomfanyia mwaka huu januari lakini kidonda bado kinasumbua kupona.

Wakati tunahangaika kupata matibabu ya nyoga ndipo alipogundulika kuwa anatezi dume ndipo alipofanyiwa upasuaji.

Mzee Majuto Akimbizwa Hospitali Baada ya Kuzidiwa Ghafa.

Mwigizaji wa maigizo ya vichekesho na filamu nchini, Mzee Majuto amekimbizwa hospitali  baada ya hali yake kubadilika ghafa na kuzidiwa .mzee majuto ambae amekimbizwa hospitali ya tumaini jijini dar ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu mara ya kwanza amepelekwa hospitali hapo kwa ajili ya kuangaliwa tena afya yake.

Ikumbukwe kuwa Mzee Majuto aliwahi kuuumwa mara ya kwanza na kuthibitisha kuwa alikuwa akisumbuliwa na tezi dume hivyo alifanyiwa uapsuaji kwa ajili ya kutibu mardhi hayo lakini hali yake baada ya kubadilika inasemekana kuwa kidonda chake kimekuwa kikimsumbua kwa muda mrefu hivyo kinashindikana kupona na kusababibisha kutoka maji.

Akiongea na waandishi wa habari, mke wa Mzee mMajuto amesema uwa ni kweli mume wake amepeleka hospitali baada ya hali kubadilika na kukimbizwa hospitali huku akisema kuwa tatizo kubwa ni kidonda alichofanyiwa upasuaji kushindwa kupona na kutoa maji.

Mzee Majuto Akiri Sinema Kuwa Ndio Kila Kitu Kwake.

Msanii mkongwe na maigizo na vichekesho nchi Mzee Majuto  ambae amekuwa ni kama mlezi kwa wasanii wengine wa bongo movies amekiri kuwa kazi za sinema na filamu ndio kila kitu katika maisha yake na ndio zinazompa kula na kuishi mjini kwa miaka yote.

Akiongea na wasanii wenzake Jb na Single Mtambalike hivi karibuni walipomtembelea hospitali ambapo amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Mzee Majuto anasema kuwa anaishukuru na kuheshimu kazi hiyo kwa sababu ndio iliyompa kula na kuishi mjini, huku kisema kuwa pamoja na kwamba amekuwa mgonjwa kitandani lakini ndani anakazi  nane ambazo hazijatoka huku akiitaja ya uganga ndio iliyotoka tu.

Nina miaka 70 sasa na kazi kubwa inayoniweka mjini ni hii ya sinema,nina movis nane nimeziweka ndani kwaio sina presha.nikisikia njaa natoa moja nauza napata kula. na katika hizo nane nimeuza moja tu ya uganga basi.-Alifunguka Mzee Majuto.

Mzee Majuto yuo katika hospitali ya Tumaini jijini Dar, ambapo alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya upasuaji wa tezi dume iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu, hata hivyo hali yake inasemekana kuimarika .

Mzee Majuto Aomba Wasanii na Mashabiki Wamuombee.

Msanii wa maigizo ya  vichekesho na filamu nchini Mzee Majuto amewaomba wasanii na mashabiki zake kuendelea kumuombea kwa sababu hali yake sio nzuri sana pamoja na kwamba ameshatoka hospitali  alipokuwepo kwa ajili ya matibabu yake aliyokuwa  anapatiwa.hata hivyo mzee majuto anasema kuwa alitakiwa kufanyiwa upasuajai lakini ilishindikana kwa sababu ya matatizo aliyokuwa ameyapata daktari wake.

Mzee Majuto aliekuwa akiumwa ugonjwa watezi dume amesema kuwa ugonjwa huo ni hatari kuliko  ambavyo watu wanafikiria kwa sababu unaweza kukutoa Duniani bila hata ya wewe kujua kwaio anaomba watu wamuomee ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

Mzee Majuto alilazwa wiki chache zilizopita katika hospitali ya tumaini jijini dar ambapo mh raisi laikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali  msanii huyo na kmpa pole kitu ambacho pia kilimfariji sana msanii huyo.

Hata hivyo Mzee Majuto ambae kwa sasa yuko nyumbani anasema kuwa february 11 anatakiwa kurudi tena hoispitali kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake na kufanyiwa upasuaji kwa sababu daktari aliyekuwa ana mpatia matibabu alikuwa amefiwa hivyo kufanya kusimammishwa kwa matibabu yake.

Niliruhisiwa jumamosi iliyopita lakini kwakweli bado ninaumwa, tezi dume wala sio mchezo kwakweli.ninachoweza kuwaambiwa na kuwaomba ni kwamba ninaomba mniombee  tu , sala zenu pia zinahitajika.

 

 

,

Mzee Majuto Atembelewa na Mh.Rais Hospitalini.

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , Mzee Majuto amaetembelewa na Mh .Raisi Magufuli hospitalini alipokuwa amelazwa  mpaka sasa ambapo bado anapokea matibabu ya ugonjwa wa tezi dume aligundulika kuwa nao siku kadhaa zilizopita.

Mzee Majuto ameonyeshwa kufurahishwa na ujio wa Raisi na kumpongeza kwa kazi yake nzuri anayoifanya sasa ya kuwafanya wananchi wote kuwa na moyo wa kufanya kazi na kujituma , lakini pia amesifia na kusema kuwa uongozi wa Raisi huyo umekuwa wenye baraka na neema kwa sasa sasa hivi nchi iko vizuri kwa kila mtu,

Akiendelea kuongea baada ya Mh.Raisi kutoka hospitalini hapo, Mzee Majuto anasema kuwa yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kutabiri kuwa Magufuli angeweza kushinda uraisi na angeweza kuiendesha nchi na ndicho anachokifanya sasa.

mii ndie mtu wa kwanza kutabiri kuwa akiwa raisi itakuwa shughuli hapa,nilishukuru kuchaguliwa kwa huyu bwana, hapa tumepata raisi sio masihara hasa, watu wote sasa wana adabu zao.wanajua nini maana ya kazi na akisema tu jambo watu wanatekeleza haraka sana.

wezi wanakamatwa, wala rushwa wanakamatwa, na wenye vyeti feki hata kama ulifanya kazi miaka 20 iliyopita fukuza, hii safi sana.

Sisi wazee tunafarijika sana, hivi viwanda sasa hivi vinatapakaa kila sehemu na leo hamekuja kunitembelea hospitali siujui kama kuna watu hawajajikojolea hapa kwa uoga maana hataki masihara kabisa.hii ndio raha ya kupata kiongozi bora mwenye msimamo.

Pamoja na kumpongeza lakini pia Mzee Majuto anasema kuwa sio kazi rahisi kwa wananchi kupata kiongozi mzuri kama Magufuli hivyo waweze kumtumia vizuri.

Mzee Majuto amelazwa katika hospitali ya Tumaini iliyopo jijini Dar wiki iliyopita baada ya kutolewa nyumbani kwake Tanga na kuletwa huku kwa matibabu zaidi na kukutwa na tezi dume , na mpka sasa bado yuko hospitali kwa kuendelea na matibabu.

Mh.Raisi alipokutana na Mzee Majuto akiwa hospitalini.

Mzee Majuto Kam-miss Lulu

Akiwa kama msanii mkongwe katika tasnia ya filamu Tanzania , ambae kwa sasa amepumzika kufanya kikazi zake za sanaa kutokana na umri kwenda  Mzee Majuto ameonyesha hisia zake za kum-miss msanii Lulu Michael ambae kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili.

Lulu ambae alitunukiwa kifungo chake cha miaka miwili tarehe 13 November baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia msanii mwenzie Steven Kanumba ambae pia alikuwa mpenzi wake ameanza kutumukia kifungo hicho mara baada tu ya kukipokea siku hiyo.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram Mzee Majuto aliweka picha waliopiga siku za nyuma na msanii lulu michael na kuandika  ‘nimekumiss mjukuu wangu

Tangu Lulu kufungwa gerezani watu mbalimbali ikiwepo wasanii ambao wamekuwa wakionesha kusikitishwa na hukumu hiyo.Hata hivyo wapo baadhi ya wasanii waliokuwa wakitoa ushuari kwa lulu walimuomba kutokata rufaa hili kuondokana na mzizi wa fitina katika jamii.

Maisha Ya Mzee Majuto Matatani,Asakwa Na Wasiojulikana

Inadaiwa kuwa ni siku kama kumi zimepita tangu itolewe taarifa  kuwa msanii wa maigizo na vichekesho nchini Mzee Majuto alipotapeliewa fedha zake na kampuni mojawapo hapa nchini  inayohusika na filamu.Akimuelezea Waziri wa habari Mzee Majuto alidai kuwa kwa sasa hali ya maisha yake iko mashakani baada  ya watu hao wasiojulikana kutaka kumuuua kwa sbabau tu amekuwa akidai haki yake.

Akielezea sakata hilo moja ya watu wa karibu kutoka Tanga ambae akutaka jina lake litajwe alidai kuwa ;

Mzee Majuto hana amani kwa sasa , amekuwa akilalamika kuwa kuna watu wanataka kumuua kwa kuwa alikuwa anadai ela zake ambazo mpaka sasa hajapatiwa hata shilingi kumu na yupo tu hajui cha kufanya, mbaya zaidi ni kwamba alipoteza simu yake kwaio hana wa kuwasiliana nae kumsaidia kwa hilo.kwaio kuogopa kwake kunamfanya anyamaze tu sasa hivi.

Akiulizwa na waandishi kutoka kampuni ya Global alipofuatwa nyumbani kwake, Mzee Majuto alikiri kuwa kweli kuna watu wamekuwa wakimtishia kumnyonga na kumpiga risasi lakini hana ufahamu na watu hao.

Licha ya kumweleza waziri lakini mpaka sasa sijapata kitu changu chochote kwa siku,na ninaogopa kuendelea kudai kwa sababu ninatishiwa kuuawa,si unajua siku hizi mtu ukidai haki zako unaweza kunyongwa au ukiwa barazani  unashtukia unapigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nilikuwa na namba za waziri na nilimpigia baada ya siku ile kunihaidi atashughulika swala langu,lakini siku ile aliniambia yupo kwenye kikao nimtafute wakati mwingine.Siku chache baadae nikiwa nasafiri kwenye ndege nilipoteza simu kwaio nikawa sina namba tena,imebidi nitulie nimwachie mungu tu  atanilipa hizo fedha ninazodai maana naogopa kunyongwa jamani.

Hata hivyo bado Mzee Majuto anamkumbusha na kumuomba Waziri  mwenye mamlaka hiyo kushughulikia swala lake kwa sababu peke yake anaona ameshindwa kabisa.Mwisho wa mwezi uliopita Waziri wa habari alikutana na wasanii na kuzungumza nao ili kujua changamoto zinazowakabili, na katika mazungumzo yake alihaidi kushughulikiwa watu wote ambao wamekuwa wakiwadhulumu na kuwaonea wasanii katika kuwapatia haki zao.

 

Mzee Majuto aeleza vitu ambazo atajishugulisha nazo baada ya kuamua kustaafu

Alhaji Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto sasa ameamua kuachana na mamba ya sanaa baada ya kufanya kazi ya uigizaji kwa takriban miaka 30.

Mwezi jana muigizaji huyo mkongwe aligonga vichwa vya habari baada ya taarifa potovu kuidai kuwa ameaga dunia ghafla nyumbani kwake Tanga.

Mzee Majuto sasa ameeleza kuwa ameamua kustaafu baada ya kuona umri wake unaenda na uwingi wa changamoto wa kazi yake ya uigizaji.

kwenye mahojiano yake na gazeti la Habari Leo, muigizaji huyo alifunguka na kusema kuwa yeye sasa atajishugulisha na kilimo na kumtumikia Mungu.

“Kwa sasa hivi mimi sanaa basi , nasema kwa kweli sanaa basi labda kutokee mtu anahitaji nimfanyie tangazo lake nikimaliza narudi shambani kwangu nimtumikie mwenyezi Mungu nimuombe toba kwa sababu tuliofanya ni mengi na kuna mazuri na mabaya na mabaya ndiyo yanayotawala kwenye maisha ya ujana kwa hiyo tumuombe toka Mwenyezi Mungu, kwani wakati ndiyo huu ukisema upange siku kila siku utapanga,” Mzee Majuto alisema.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://youtu.be/Sf9_vue0ttc