JB- Siwezi Kuwa Mrithi Wa Mzee Majuto

Muigizaji wa Bongo movie Jacob Stephen maarufu kama JB amesema hata siku moja hawezi kuwa mrithi wa Marehemu Mzee Majuto.

Mzee Majuto alifariki mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ingawa alikuwa na umri mkubwa Mzee Majuto alikuwa mmoja wa komedian mkubwa sana Tanzania.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, JB amesema mashabiki wengi wamekuwa wakimwambia kwamba yeye ndiye mrithi wa Mzee Majuto, lakini haiwezekani kushika nafasi yangu maana alikuwa na ladha yake na yeye ana ladha yake katika uigizaji.

Haiwezekani mimi kuwa mrithi wa Mzee Majuto maana alikuwa na kitu cha tofauti sana na alipendwa na watu wengi hivyo ni vigumu kuwa mrithi wake ila ninawaahidi Watanzania kuwafurahisha kwa kadiri ya uwezo wangu katika kuigiza”.

 

Mke wa Mzee Majuto Adaiwa Kufukuzwa Nyumbani kwa Mumewe.

Mke wa marehemu Mzee Majuto anaripotiwa kuondoka nyumbani kwa mume wake jijini Tanga na watoto wake huku ikidaiwa kuwa sababu kubwa ya yeye kurudi nyumbani kwao jijin Dar ni kutokana na maneno aliyoambiwa na watoto wake wakubwa kuwa hawana uwezo wa kumlea mpaka arobaini.

Mwanamke huyo ambae alikuwa bega kwa bega na mzee majuto kwa kipindi chote cha uhai wake na ugonjwa wake mpaka anafariki, alikuwa mke wa pili wa mzee majuto na alibahatika kuwa na watoto nae huku mzee majuto akiwa na watoto wengine wakubwa aliozaa kabla ya kumuona mke huyo aliyepo sasa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mama huyo pamoja na kwamba alikuwa na watoto walikuwa wakisoma jijini Tanga, imemlazimu kuondoka na watoto hao na kuwaacha shule.

Baada ya kumtafuta moja ya watoto wa marehemu Mzee majuto alikiri na kusema kuwa ni kweli mama yao hayupo amerudi Dar lakini aliwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwao.

 

 

 

Muigizaji Mtoto wa Miaka Minne Amlilia Mzee Majuto

Mtoto wa miaka minne ambaye anakuja kwa kasik katika tasnia ya uigizaji na Uchekeshaji Maisara Mohamed maarufu kama Maizumo amefunguka kusikitishwa na Kifo cha Mzee Majuto.

Mtoto huyo ameweka wazi kuwa ndoto yake kub a ilikuwa ni kuigiza na Marehemu Mzee Majuto aliyeaga dunia siku chache zilizopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, mtoto huyo amefunguka kuwa alikuwa anampenda sana King Majuto na alimuomba baba yake amkutanishe naye lakini hakufanya hivyo.

Nilikuwa nampenda sana King Majuto, nilikuwa napenda kuangalia muvi zake pamoja na matangazo yake, baba aliniambia atanipeleka nikamuone lakini hatukwenda mpaka amekufa”.

Baba Mzazi wa Maizumo Mohammed Omary ambapo kwa upande wake alisema kuwa siku ya msiba unatokea hakuwa nyumbani lakini aliporudi alimuita Mai nakumwambia kuwa Majuto amefariki lakini chakushangaza alilia sana kama mtu mzima na hata shuleni alikuwa anakataa kwenda, hivyo wakafanya kumlazimisha.

Nisha: Sitoweza Msahau Mzee Majuto Maishani

Msanio wa filamu za kibongo na msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha amefungukia Kifo Cha Msanii mwenzake mkongwe wa Bongo movie na comedy Mzee Majuto aliyeaga dunia wiki iliyopita.

Nisha amefunguka na kudai yupo katika majonzi mazito katika kipindi hiki ambacho Msanii huyo Nzee Majuto amefariki dunia kwani pengo alilomuachia haliwezi kuzibika katu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nisha alieleza kuwa, kifo cha Mzee Majuto kimemuumiza kupitia kiasi na pengo alilomwachia moyoni mwake ni kubwa kwani mashabiki wa filamu hasa za vichekesho wasingemjua.

Mzee Majuto nilikuwa namwita baba kwa sababu amenitoa kisanaa, yaani alikuwa ni kiungo muhimu sana maishani mwangu, machozi na maumivu yangu havitafutika, nashindwa kuamini na pengo lake halifutiki maishani mwangu”.

Mzee Majuto alifariki dunia siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Picha Za Kuagwa Kwa Mwili Wa Mzee Majuto

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ jana Agost 9, 2018.

Mzee King Majuto alifariki dunia jana Agosti 8, 2018 majira ya saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.

Baada ya kuaga,  mwili ulisafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa.

Hizi ni baadhi ya picha za matunzo ya kuuaga mwili wa MZee Majuto:

 

.

 

Rais Magufuli Akiri Kuguswa na Kifo Cha Mzee Majuto

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joh Pombe Magufuli amefunguka kuguswa na Kifo Cha mchekeshaji maarufu Mzee Majuto kilichotokea siku ya jana.

Rais Magufuli Martina barua ya Rambi Rambi kwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo DKT. Harrison Mwakyembe na kumtaka afikishe salamu hizo kwa Familia ya Mzee Majuto.

Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Mwakyembe kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya Marehemu, Wasanii wote nchini, wadau wa sanaa, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha King Majuto.

King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake”.

Tanzia- Mzee Majuto Afariki Dunia

Msanii mkongwe wa Bongo movie aliyejizolea umaarufu kwa vichekesho vyake amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mzee Majuto amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbil baada ya kulazwa kwa siku kadhaa tangu wiki chache zilizopita baada ya kuugua.

Taarifa za msiba kwa mara ya kwanza zilitolewa na mchekeshaji Joti Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu”.

Mzee Majuto alianza kuugua mwaka jana na mwaka huu serikali kwa kushirikana na wananchi walichanga pesa na kumpelekeka kwenye matibabu nchini India.

Hali ya Mzee Majuto si Shwari, Arudishwa Tena Muhimbili

Hali ya msanii mchekeshaji  maarufu na mkongwe tanzania mzee majuto imeripotiwa kurudi kuwa mbaya hivyo kufanya kurudishwa tena hospitali ya muhimbili siku ya leo.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika hospitali ya muhimbili aminiel aligaesha , ndie aliethibitisha taarifa za kupokelwa kwa mzee majuto aktika hospitali.

Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa mzee majuto kwenda hospitali lakini mara ya pili kurudishwa akiwa na hali mbaya kutokana na  operation aliyofanyiwa iliyosababisha kupelekwa india kwa ajilia ya matibabu zaidi.

Hatimaye Mzee Majuto Kulipwa Mamilioni Yake

Muigizaji Mkongwe wa Bongo movie Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto anatarajiwa kuanza kulipwa mamilioni yake ya pesa aliyokuwa anadai katika mikataba mbali mbali.

Habari hiyo njema imekuja Miezi michache tangu Waziri Mwakyembe alipoyataka makampuni mbali mbali yaliyoingia mikataba na Mzee Majuto kisha kumlipa pesa ndogo au kumzulumu Kupitia mikataba hiyo na kumlipa Tena pesa zake.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani Jumatatu iliyopita, nyumbani kwake, maeneo ya Bunju jijini Dar, Majuto alisema aliamua kusamehe ile mikataba midogomidogo ila kwenye ile mikataba mikubwa aliyodhulumiwa.

Niliamua kusamehe ile mikataba yangu midogomidogo ila hiyo mingine aliyosema ataishughulikia muheshimiwa Mwakyembe bado naendelea kuisubiri ila kwa sasa siwezi nikaongea chochote kuhusu hilo, hivyo naomba mumuulize msemaji wa chama cha waigizaji”.

Lakini pia gazeti hilo pia lilifanikiwa kuongea na msemaji wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany ambaye alisema hatua aliyofikia Mwakyembe ya ufuatiliaji wa mikataba ya wasanii akiwemo mzee Majuto inaendelea vizuri na hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa.

Siku ya jana Mzee Majuto alitangaza kuachana na mambo ya sanaa kutokana na maradhi mbali mbali yanayomsumbua.

Mzee Majuto Agoma Kuigiza Tena , Aomba Kuongea Na Waziri na Rais

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , Mzee Majuto amefunguka na kusem kuwa kwa sasa hana mpango wa kuigiza tena kwa sababu anataka kupumzika na wala hataki kusikia kitu kuhusu sanaa.

Majuto amesema kuwa maamuzi yake hayo kwa sasa ni ya mwisho na hakuna wa kuyabadilisha tena isipokuwa mh mwakyembe au mh raisi magufuli endapo watapata muda wa kuongea nae,lakini si vinginevyo.

Majuto anasema kuw akwa sasa haoni haja ya kuendelea kuigiza lakini kama atapokea ushauri kutoka kwa viongozi hao wawili wakubwa kuhusu sanaa anaweza kuwasilikiza na kubadili mawazo lakini sio mtu mwingine yoyote yule.

Natoa kauli yangu rasmi kuwa sitaku kuigiza tena labda raisi wangu mpendwa Magufuli  au mzee wangu Mwakyembe waniambia hapana endelea ndipo nitawasilikiza,hakuna mtu mwingine wa kunishauri baba yangu alishafariki na mama yangu alishafariki na marafiki zangu wote ni wasanii watupu.

Mara ya kwanza Mzee majuto aliwahi kutangaza kuwa anaachana na kazi ya sanaa na wasanii wengi walimlilia na kumfanya arudishe moyo wake nyuma ili kuendelea na sanaa lakini kwa hapa karibuni Mzee majuto alipatwa na maradhi yaliyomfanya kukaa hospitali kwa muda mrefu hivyo anaona kuwa anahitaji kupumzika kwa sasa.

 

 

Mzee Majuto Atangaza Kuwasamehe Wanaomdai

Msanii wa bongo movies mzee majuto  ametangaza kuwasamehe wale wote waliokuwa wakimdai na kusema kuwa hana haja ya juwadai tena hata kama ilikuwa pesa nyingi kiasi gani.

mzee majuto amemuomba mh mwakyembe hasiendelee kuwadai wala kushughulikia swala la madai yake tena kwa sababu alishawasamehe wote anaowadai.

pindi mzee majuto anaumwa na kukosa pesa ya matibabu , waziri mwakyembe akitangaza kufuatilia mikataba yote ya mzee majuto ikiwemo matangazo na kila biashara ya filamu aliyoifanya ili kuangalia sehemu gani wamemdhulumu ili aweze kupata haki yao.

ambapo baada ya kutangaza hivyo aliomba familia ya mzee majuto kutafuta nyaraka zote za mzee majuto ili kufuatilia madai hayo lakini baada ya mzee huyo kupata nafuu amesema kuwa hakuna haja hata kama kuna mtu anamdai shilingi 100.

Mzee Majuto Azungumza Kuhusu Kuzushiwa Kifo

Baada ya kuzushiwa kifo kwa msani wa bongo movies Mzee Majuto, mzee mwenyewe amemzungumza na waandishi wa habari na kukanusha kifo hiko na kusema kuwa yeye bado yuko hai lakini hata kama atakufa anawaomba sana watanzania wamuombee ili aweze kufa kifo  chema.

Akiongea na Global Online tv, mzee majuto anasema kuwa  kuwa anawashukuru watanzania kwa sara zao lakini anawaomba sana waendelee kumuombea huku akiishukuru serikali ya Tanzania kwa matibabu waliompatia.

Ninawaambia watanzania washtute , mimi sijafa mimi mzima jamani,kama mwenyezi mungu atanichukua basi mje mnizike kwa wingi , mniombee ili niende mahali pazuri, mlimpenda sana rafiki yenu kanumba lakini Mungu alimpenda zaidi.

Taarifa hizo ziliazna kusambaa juni 26 mwaka huu lakini mwanae wa kiume aliongea na kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa baba yake alikuwa akiendelea vizuri.

TDFAA Wakanusha Taarifa za Kifo cha Mzee Majuto.

Kumekuwa na taarifa ya kifo cha Mzee Majuto katika mitandao ya kijamii  ilhali ni uongo kwa sababu mzee majuto tang ametoka nchini india bado yupo katika hospitali ya Muhimbili na anaendelea vizuri na bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.

Baada ya kuzushwa kwa taarifa hizo za kifo,Chama cha wasanii na waigizaji wametoa taaraifa ya kusikitishwa kwao na taarifa hizo “chama cha uigizaji kinasikitishwa na taaraifa zinazosambaa za uzushi zinazosambaa katika mitandao kuhusu kifo cha mzee majuto na kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.mzee majuto yupo hai na yupo nyumbani kwake.

Mzee Majuto aliyekwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume alifanyiwa upasuaji nchini lakini kidonda kilishindw kupona kwa haraka hivyo kulazimu kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi na alirejea siku kama mbili zilizopita.

JPM Ahusika Kufanikisha Safari ya Matibabu ya Majuto Nchini India.

Msanii wa filamu za maigizo na vichekeshao Mzee Majuto amefanikiwa safari yake ya matibabu kwenda nchini india kwa ajili ya matibabu  kwa matatizo aliyoyapata alipokuwa nchini kushindwa kufanikiwa hivyo kwenda nchini india .

Akiongea na waandishi wa habari siku ya tarehe 1 May, Steve Nyerere ambae alisaida sana katika zoezi hilo anasema kuwa siku hiyo Mzee Majuto  atatarajiwa kusafiri kwenda india kwa ajili ya matibabu yake huku akiwataja na kuwashukuru sana baadhi ya watu waliokuwepo  katika kfanikisha hilo huku akiwataja Mh Magufuli na Mh Mwakyembe katika kufanikisha hilo.

niseme ahsante sana kwa mh raiis john pombe magufuli , mh mwakyembe pamoja na Ummy Mwalimu kwa kufanikisha hili, lakini pia niwashukuru wasanii kwa kujitoa kwao, Mungu akipenda leo mzee majuto atakuwa njiani kwenda India kwa matibabu.

Hata hivyo Steve Nyerere pia amewatolea povu baadhji ya wasanii wanaokaa kujinadi katika mitandao kuhusu maisha yao lakini mwisho wa siku wanabaki wakiangaika na kuwa wanaomba misaada  wanapopata shida.

Sidhani kama miaka nenda rudi tutakuwa na kazi ya kuwa tunaomba omba tu,tumekuwa watu wa kufanya maparty kila kukicha na kujinadi kuwa ngu zetu za miliona 3, 4 lakini ukimuuliza umejipangaje kwa kesho hamna kitu.

 

 

Mh. Mwakyembe Kupitia Upya Mikataba ya Mzee Majuto.

Baada ya kutangazwa katika vyobo vya habari kuwa msanii mkongwe nchini mzee majuto ni mgonjwa sana na aanahitajika kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu kuhu akiomba msaada wa kupewa fedha za matatibabu, mh waziri anaeshughulika na maswala hayo ameliambia mbunge kuwa Mzee Majuto ni msanii mkubwa sana na amefanya matangazo na kuingia mkataba na makampuni mengi sana mabyo yamekuwa yakirusha matangazo yake katika televisheni lakini mzee huyo hakufaidia  na kitu chochote.

Akiongea akiwa bungeni mh mwakyembe anasema kuwa “Mzee Majuto mwanasanaa mzuri anaumwa anaomba pesa, mimi leo nachanga kutoka mfukoni lakini leo hii nusu ya mabango ya biashara ni Mzee Majuto, matangazo ya biashara kwenye TV ni Mzee Majuto naomba sasa nitumie nafasi hii kusema nimeunda kamati ya wanasheria tumeanza na kesi ya Mzee Majuto mashirika yote na kampuni zote zilizoingia mkataba na Mzee Majuto tutapitia hiyo mikataba kama ameonewa lazima ilipwe familia yake tumeshachoka, tukimaliza Majuto tuna kuja mikataba ya Kanumba na msanii yoyote ambaye aliingia mkataba wa kipumbavu atuone”  .

Wasanii wengi wamekuwa wakiomba misaada pale wanapopata matatzo ilhali walikuwa na nguvu na jina kubwa ambalo lingeweza kuwaingizia pesa kwa kipindi chote cha ugonjwa au uzee kama Mzee Majuto.

Mzee majuto ameanza kuumwa tangu janauary mwaka huu na kufanyiwa upasuaji , ambapo hivi karibuni alirudishwa hospitali baada ya hai yake kuwa mbaya tena na kusemekana kuwa kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeshindwa kufunga, mpaka sasa Mzee Majuto ameamishiwa hosptali ya muhimbili na wizara imepanga kumsaidia ili kupata hali zake za mikataba na matangazo mbalimbali aliyowahi kuyafanya.