Mahakama Yaagiza Nabii Tito Apimwe Akili Upya

Mahakama ya wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa  mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma, Tito Machibya maarufu kama Nabii Tito kupimwa upya akili yake katika taasisi ya afya ya akili Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kujiridhisha kama ana ugonjwa wa akili.

Nabii Tito alijizolea umaarufu kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai ana kanisa lake linalojulikana kama kanisa la walevi. Ambapo alifika mbali mpaka kuanza kufanya matendo machafu na wanawake mbali mbali ndipo aliposhikiliwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma.

Hata hivyo Nabii Tito aliwekwa rumande baada ya kutaka kufanya jaribio la kujiua kwa kujikata na wembe kwenye tumbo januari 25 mwaka huu nyumbani kwake Ng’ong’ona alipokuwa anakaguliwa na polisi.

Nabii Tito alidai kuwa ana ugonjwa wa akili ndipo mahakama ilipotaka vielelezo vya daktari ili kujiridhisha kama kweli ana ugonjwa wa akili ili vitumike katika kesi yake ambapo anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua au kujaribu kujiua kwa kitumia wembe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo James Karayemaya alisema jana kuwa kutokana na mshtakiwa kuiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili na aliiambia mahakama kuwa alijaribu kujiua kwa sababu alisikia sauti au vitu vilivyokuwa vinamwamuru ajikate, mahakama itabidi apate uthibitisho wa vielelezo vya anachokisema hivyo mahakama imeamuru vipatikane kabla ya kesi yake haijaanza kusikilizwa. (Chanzo: Global Publishers)

Mama Kanumba Afunguka Kuhusu Picha za Nabii Tito na Mwanae

Mama wa marehemu Steven Kanumba amefunguka baada ya kusambaa kwa picha za Nabii Tito na mwanae maraehemu steven kanumba  miaka ya nyumba kipindi cha uhai wake.Mama huyo amekiri  kuwa mwanae alishawahi kukutana na nanbii huyo lakini nia yake iligonga mwamba.

Mama Kanumba anasema kuwa nabii tito alikutana na Kanumba na kumuomba ajiunge katika kanisa lake alilokuwa amelianzisha kwa niaba ya kuwavutia watu watakaokuwa wanakuja kwa ajili ya kumshangaa Kanumba   lakini kwa upande wake itakuwa faida kwa sababu atakuwa amejaza watu.

Mama Kanumba anasema kuwa marehmu Steven alikataa kata kata kuhusu ombi hilo kutokana na imani yake haukumtaka kufanya hivyo lakini pia Kanumba hakutaka kuhama kanisa analosali hata siku moja.

Kwa upande wa Seth ambae ni mdogo wake na marehemu Kanumba ambae poia kwenye pia hizo amekuwa akionekana amesema kuwa ni kweli Nabii Tito aliwahi kuja ofisini kwa kaka yake zilizopo Sinza-Mori kipindi hicho kaka yake alikuwa hai na kuwashauri wahamie katika kanisa lake lakini walikataa na ndipo alipowaomba wapige nae nae picha.

Tabii tito ni mkazi wa Dodoma alieibuka kama nabii huku akihubiri neno la Mungu kwa kutumia biblia lakini akisapoti unywaji wa pombe kanisani na kuwa kuoa mwanamke zaidi ya mmoja ni swala halali huku alishauri hata kuona wasaidizi wa ndani pia ni sahihi.

Nabii Tito aliendelea kupata umaarufu baada ya kumuomba msanii Wema Sepetu kusali katika kanisa lake na pia aweze kumuoa ilhali yeye mwenyewe akiwa na wake watano na watoto 12, nabii tito alimuona wema aje katika kanisa lake ili aweze kupata idadi kubwa ya wafuasi kwa kuwa watakuwa wanakuja kumshangaa yeye kanisani.

Mpaka sasa Nabii Tito amekamatwa na kufanyiwa vipimo ambapo alikutwa na magonjwa ya akili na kuanza matibabu lakini pia kesi yake ikiendelea mahakamani, kosa kubwa  la Nabii huyo kufanya mahubii ya dini ya kikristo kwa kutumia msalaba na biblia kinyume na taratibu za kanisa.