“Sina Mahusiano Ya Kimapenzi na Nandy”- Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva Anayezidi kufanya vizuri hivi sasa Aslay amefunguka na kusema hana Uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii mwenzake Nandy.

Kumekuwa na maneno mengi mengi ambayo yamekuwa yakisababishwa na ukaribu uliopo kati ya Nandy na Aslay ambapo mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii imesemakana kuwa wawili hao ni wapenzi.

Kwenye Interview aliyofanya Friday Night Live ya East Africa Tv, Aslay amefunguka na kusema ukaribu aliokuwa nao na Nandy ni wa kikazi tu sio zaidi ya hapo na amesisitiza kuwa yeye tayari ana mpenzi wake na familia.

Nafikiri watu wanaonifatilia watakuwa wanajua kuwa mimi nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy nipo naye kwenye kazi zetu za kimuziki tunazofanya hakuna kingine cha zaidi kinachoendelea kati yangu na Nandy”.

Nandy na Aslay wanakimbiza na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao umefikisha zaidi ya viewers milioni tatu YouTube kwa mwezi mmoja lakini pia wameshawahi kufanya ngoma nyingine iliyofanya vizuri siku za nyuma iliyoitwa Mahabuba.

Aslay na Nandy Wafanya Bonge La Shoo (picha ndani)

Siku ya Jumamosi tarehe 17 February msanii mkubwa wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana Aslay na msanii mwenzake kutoka THT walipiga bonge la shoo Valentine’s Day Mapenzi Mubashara iliyojulikana kama Nandy Aslay pamoja na marafiki.

Shoo hiyo iliyohudhuriwa  na nyomi la watu ilipambwa na wasanii wengine wengi kutoka THT na mastaa wengine kama Ben Pol, Dogo janja na wengineo.

Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa siku ya tukio: