Young Killer amjibu Nay Wa Mtego baada ya kumdiss

Nay Wa Mtego ni msanii ambaye anajulikana kuwachana wasanii wenzake kupitia mziki wake. Hapo mbeleni ameskika akiwachana akina Wema Sepetu, Ommy Dimpoz na wengi kupitia nyimbo zake.

Nay wa Mitego

Hivi karibuni aliachia wimbo mpya ‘moto’ ambapo aliskika akimwambia Young Killer “Young Killer chali, safari ya Mwanza inanukia, usiwadharau waliokufanya ukatoba” kitu ambacho kimemfanya Killer kumjibu Nay.

Kupitia mtandao wa Instagram Young Killer aliandika, “Nasikia kuna mtu kanidiss” kuonyesha kuwa alikuwa ameupokea ujumbe wa Nay. Hata hivyo jambo hili halikumshtua rapper huyu kwani alimjibu Young Killer kwa kuandika ” #Ney True Boya,” kupitia mtandao wake wa Instagram.

Hata hivyo, hakuna anayejua kinachoendelea kati ya wawili hawa.