Nini Ajutia Kuchanganya Mapenzi na Kazi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kufanya vyema amefunguka na kusema wazi kuwa sio vizuri kuchanganya mambo ya mapenzi na kazi kwani utapotea kimuziki.

Nini aliwahi kuwa kwenye mahusiano na ya kimapenzi na msanii mwenzake Ney wa Mitego ambaye pia alikuwa bosi Wake kwani alikuwa amesainiwa chini ya Label yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Nini amesema wazi kuwa kuna madhara makubwa sana endapo Msanii wa kike atasimamiwa na Mpenzi Wake kwani inaweza ikasababisha Msanii huyo kupotea kwenye gemu.

Kuna madhara kwa mtoto wa kike kusimamiwa na mpenzi Wake kwani tumeona wasanii wengi wa hivyo wameishia kati na hawajafikia malengo yao kwaiyo kama inaweza ikaepukika ni vizuri zaidi lakini cha muhimu wa wasichana kujitambua na kutambua wanataka nini”.

 

Nay Wa Mitego- Bado Ninampenda Nini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya muziki wa kuchana Emanuel Elbariki maarufu kama Nay wa Mitego ameibuka na kudai bado anampenda aliyekuwa mpenzi wake Msanii mwenzake Nini.

Nay wa Mitego walitangaza kuachana wiki chache zilizopita ambapo Nay alikiri kuwa sababu kubwa ya kumwagana ni baada ya Nini kumkamata akiwa na mwanamke mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nay amefunguka na kudai moyoni bado anampenda Nini na endapo atapata nafasi nyingine basi atampokea kwa mikono miwili.

Bado ninampenda sana Nini na hata kama akirudi leo hii akahitaji kurudiana na mimi, nitakuwa tayari kumpokea”.

Nini na Nay walificha mapenzi yao kipindi chote walipokuwa wote kutokana na kwamba Nini alikuwa amesainiwa chini ya Label ya Nay Free Nation ambapo Mpaka sasa pamoja na kwamba hawapo wote lakini Nini bado anafanya kazi chini ya Label hiyo.