Lynn na Tunda Vitani Kisa Penzi La Diamond

Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ Lynn ameingia Kwenye vita kali na video queen mwenzake Tunda Sebastian na inadaiwa kisa ni Diamond.

Global Publishers wanaripoti kuwa warembo hao hivi sasa ni kama Paka na panya kutokana na wote wawili kumpenda Diamond na kuchanganywa kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, mrembo Lynn ambaye haambiliki kwa Diamond, mara baada ya kusambaa kwa video ya Tunda na Diamond pamoja  ndipo lilipotangazwa bifu jipya mjini kati ya Tunda na Lynn.

Si unajua ni juzi tu Lynn alidaiwa kuzawadiwa mpaka gari na Chibu (Diamond) wakati wa bethidei yake?

Sasa hiyo video ya Tunda imemtibua Lynn na timu yake kwa sababu Lynn humwambii kitu kwa Diamond ‘so’ sasa hivi ni mwendo wa vijembe tu huko social media (mitandao ya kijamii).

Wenyewe wanasema kama mwanamke akitaka kumtibua Lynn, basi ajisogeze kwa Diamond kama alivyofanya Tunda maana ameshasema kuwa yupo tayari kuolewa na jamaa huyo, sasa hataki mtu amtibulie”.

Baada ya Tetesi hizo za bifu gazeti hil lilimsaka Tunda ili kumhoji kuhusu bifu na Lynn ambaye alifunguka:

Jamani kama ujuavyo ile ilikuwa ni sherehe na kila mtu pale alikuwa ameshakunywa (amelewa) na wengi walikuwa wanacheza, nashangaa sana wameniona mimi tu ndiye nilikuwa nacheza na Diamond, kama siyo mambo ya ajabu ni nini?.

Mimi kucheza na Diamond imekuwa ishu kubwa, kitu ambacho kinanishangaza sana. “Ina maana watu waliniona mimi tu? Lakini mimi naona ni kitu cha kawaida kabisa kwangu hivyo watu wasipate tabu sana,” alisema Tunda. Alipoulizwa kuhusu mwanaume wake anasemaje juu ya video hiyo, Tunda alisema kuwa, kwa sasa hana mtu anayemhofia kwani alishaachana na Casto Dickson muda mrefu.”.

Lynn alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizi alikataa kuzungumza chochote Lakini tangu sakata hili litokee Diamond ameonekana kwenye party mbili tofauti akiwa na video vixen mwingine maarufu kama Kim Nana.

Irene: Sina Mpango wa Kuolewa na Mwanaume Wa Bongo Ni Wababaishaji

Video vixen anayejulikana sana mitandaoni Irene Hillary maarufu kama Official Lynn amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa Kuolewa na wanaume wa kibongo kwa sababu wengi wao ni wababaishaji.

Irene alijizolea umaarufu siku za nyuma kutokana na kuonekana katika video ya kwetu iliyoimbwa na Rayvanny Lakini pia umaarufu ulizidi baada ya kusemekana kutoka kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Jumamosi, Irene  alisema kuwa ameona wanaume wengi wa Kibongo wanapenda sana kuchezea wanawake hivyo haoni sababu ya kuutesa moyo wake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo.

Yaani kwa niliyoyapitia sitarajii kabisa kuolewa na Mbongo wala sina wazo hilo kabisa maana naona wazi nitautesa moyo wangu bure“.