Otile Brown Ajiachia na Mrembo Mpya Baada Ya Kukashifiwa na Vera Sidika

Msanii wa muziki kutoka Kenya Otile Brown ameamua kumuanika mrembo mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram siku chache Baada ya sakata lake na Ex Wake Socialite Vera Sidika.

Wiki iliyopita Vera aliweka screenshots za maongezi yake na Otile Brown ambapo ndani yake alimtuhumu kwa kutomrudhisha chumbani kwa madai kuwa alikuwa hamfikishi wanapokuwa sita kwa Sita.

Baada ya tuhuma hizo nzito Otile alijitetea na kusema Vera alikuwa anapenda sana ngono kiasi ya kwamba alikuwa anajichezea mwenyewe hata pale wanapokuwa wamelala wote ambapo Vera alisema anafanya hivyo kwa sababu hakuwa akimridhisha Kama mwanaume.

Lakini siku chache Baada ya sakata hilo na Vera Otile Brown ameonekana kuendelea na maisha yake ambapo ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram unaomuonyesha akiwa na mrembo mwingine ambapo kwenye video wanaoenekana wakikumbatiana na kucheza kimahaba.

 

 

 

Otile Brown na Sabby Angel Wasemekana Kuwa Wapenzi.

Mwanadada Sabby Angel kutoka tanzania anasemekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii kutoka kenya Otile Brown ambae hivi karibuni alisikika kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi Vera Sidika wa nchini humo.

Wakati wawili hao wakihaha kujinasua katika mapenzi hayo na kila mmoja akitaka kujiona kuwa hana makosa kwa mwenzake, Sabby angel pia alitafutwa ili kuelezea ukweli wa swala hilo ambapo hakupatikana kusema ukweli wa mambo.

Watu wake wa karibu walisema kuwa mwanadada huyo kwa sasa yuko nje ya nchi ingawa haijajulikana yupo nchi gani , lakini hawakusema kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa.

Penzi la Otile na Vera Sidika Lafika Ukingoni.

Penzi la mwanadada maarufu nchini Kenya Vera Sidika na msanii Otile brown lasemekana kufika pabaya baada ya wawili hao kusadikika kuwa wameachana na kila mtu kwa sasa anaendelea na mambo yake.

Mahusiano hayo ambayo yalikuwa gumzo katika mitandao kutokana na umaarufu wa mwanadada huyo kutoka na kijana  huyo ambae alikuwa akionekana mdogo wa umri kwa mwanadada huyo.

Wawili hao ambao walidumu kwa zaidi ya miezi mwili walionekana kuwa pamoja maeneo mengi hasa katika baishara za mwanadada huyo na katika shughuli mbalimbali za kijamii haijaelezwa kitu gani kimevunja mahusiano yao.

katika kurasa zao za instagram, kila mmoja alikuwa akiweka picha nyingi za mwenzie na zile walizokuwa pamoja zinaonekana kufutwa kutoka kila upande.