Mtoto kapendeza! Zari Hassan amnyoa Nillan mara ya kwanza tangu azaliwe

Mtoto wa pili wa Zari Hassan na Diamond Platnumz , Prince Nillan ameachwa akifanana na babake baada ya kunyolewa na mama make hivi leo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Zari aliweza kupost picha hizi mpya za Nillan huku akimsifu alivyopendeza baada ya kumnyoa nywele zake.

Ni kweli kuwa Mtoto huyu ambaye ni mmoja wa mastar awachanga Tanzania anafanana sana na babake Chibu Dangote na Tiffah.

Wengi wa mashabiki wake wamekuwa wakimfananisha na dadake Tiffah na kusema ukweli hawa wawili wanakaa mapacha ingawa Tiffah atafikisha miaka miwili mwezi wa Agosti.

Ikiwa hujaziona picha mpya za Nillan, basi ziangalia hapa chini.