Vera Aibuka na Jamaa Mpya Siku Chache Baada Ya Kuachana na Brown

Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika ‘Queen Vee Bosset’ amedaiwa kuopoa mwanaume mwingine siku chache baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msanii Otile Brown.

Vera na Otile Brown walimwagana siku chache zilizopita baada ya kila mmoja kumnyooshea kidole mwenziye kwa tuhuma za utapeli wa kimapenzi.

Siku kadhaa kupita baada ya kuachna na Otile Brown Vera ameonekana na jamaa mwingine ambaye hakutambulika kwa jina ambapo wawili hao walionekana wakiwa wanapata msosi katika mgahawa fulani jijini Nairobi.

Vera na Otile walimwagana huku chanzo kikieleza kuwa kila mmoja alikuwa akinufaika kwa upande wake. Inaelezwa kuwa, Vera alikuwa akimtumia Otile kutengeneza jina lake kuendelea kuwa juu wakati Otile alikuwa akimtumia kufanikisha muziki wake akimtumia kama video queen.