Sasha Aanika Wowowo La Mama Yake Kuthibitisha Kuwa ni ‘Origino’

Video vixen maarufu kwenye tasnia ya Bongo fleva  Sasha Kassim ameibuka na kuweka maungo ya mama yake hadharani ili kuthibitisha kuwa maungo yake ni halisi na sio mchina.

Sasha alifikia uamuzi wa kufanya kufanya hayo Baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa umbo namba nane alilojaliwa sio origino Bali ni mchina taarufa ambazo amekuwa akizikana tangu mwanzo.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa,a Sasha alidai kuwa watu wengi wamekuwa wakimsema kuwa anatengeneza shepu bila kujua kuwa shepu hiyo inayompa matatizo kila kukicha ameirithi kwa mama yake ambaye amefanana naye vitu vingi.

Unajua kila siku nawaambia watu kuwa si-fake shepu lakini hawaelewi, sasa nimeamua kumuanika mama yangu ili waone kuwa ‘matatizo’ haya nimepata kutoka kwa mama yangu“.

Sasha aliweka wazi kuwa hivi sasa amepotea na hasikiki kama zamani kwani yuko bize na shule ambapo amedai kuwa anasoma kama chuo cha udaktari Bugando.

 

Mrembo Aibuka na Kudai Anatongozwa na Ali Kiba

Video vixen maarufu kunako gemu la Bongo fleva Sasha Kassim ameingia Kwenye headlines baada ya kudaiwa kuleta mtafaruku Kwenye ndoa ya Ali Kiba na Mke wake Amina Khalef.

Global Publishers wanaripoti kuwa Sasha Meseji hizo zilizovuja zilionekana kutoka kwa Kiba kwenda kwa Sasha usiku mnene, jambo ambalo ni hatari kwa jamaa huyo ambaye inasemekana mkewe alijifungua juzikati.

Rafiki wa karibu wa Sasha amefunguka kuhusu meseji za Ali Kiba na Sasha ameiambia

Hivi mnajua kuwa Sasha ana mawasiliano na Kiba na kuna wakati anawasiliana naye mpaka usiku mwingi? “Kama hamuamini, mimi nitawaletea ushahidi wa chatting zao kwani nimezinasa kutoka kwenye simu ya Sasha mwenyewe, hata hivyo Sasha hamtaki Kiba, mkimbana nyinyi kwa njia zenu, atawaeleza ukweli”.

Baada ya Tetesi hizo gazeti la Risasi lilimsaka Sasha na kumhoji kuhusu Tetesi hizo za mawasiliano na Kiba ilhali anajua ameoa Sasha alifunguka:

Sasa akijua kwanimimi najali? Sikia, mimi huyo Kiba simtaki yeye mwenyewe ndio ananisumbua. Tena kwa taarifa yako, sio Kiba tu hata wasanii wengine kibao wa Kibongo wananisumbua kweli siwataki, siwezi kutoka na msanii wa Bongo labda wa mantoni kama Chris Brown hivi”.

Baada ya Tuhuma hizo nzito dhidi ya yake Ali Kiba alisakwa ndipo alipofunguka haya kuhusu tuhuma hizo:

Samahani sina tabia ya kuchati na watu ovyo”.

 

 

Sasha Atishiwa Kuuliwa Baada Ya Kuiba Mume Wa Mtu

Video vixen maarufu kutokana na umbo lake Sasha Kassimu amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa maisha yake na mwanamama Aliyedaiwa kumpora mume.

Sasha amekimbilia kituo cha polisi cha Mtongani jijini Dar akidai kuwa, mwanamke mmoja aliyemtaja kwa jina la Mama Aisha anatishia kumuua.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Sasha alikiri kuna muda aliwahi kudaiwa kuiba mume wa mwanamke huyo na tangia hapo amekuwa akipokea vitisho  mbali mbali juu ya maisha yake:

Huyu mama (mama Aisha) alipoachana na mumewe, akadai eti mimi ndiye nimemvunjia ndoa, nikashangaa sana lakini hivi karibuni nimepata taarifa kuwa anapanga kunimwagia tindikali.

Nilipata hofu sana lakini jamani labda leo niseme ukweli kwamba sikuwa na uhusiano na mume wa mama huyu, nilikuwa naenda pale nyumbani kwake maana dada yangu anaishi jirani.

Yeye anashikilia kuwa mimi nilionekana nyumbani kwake kwenye kochi, ni kweli kabisa ila ulitokea msiba, nikawa naogopa kukaa kwa dada yangu, ndo’ nikaenda pale nyumbani kwa yule baba kama jirani tu lakini hakuna ishu ya mapenzi, aache kuniwazia mabaya kabisa,

Nimeona nisikae tu maana linaweza kunitokea lolote, nimeenda kufungua jalada kwenye kituo cha Polisi cha Mtongani lenye namba MT\ RB\1477\2018 KUTISHIA KUUA KWA MANENO”.

Baada ya Tuhuma hizo gazeti hilo lilimsaka Mama Aisha ambaye alifunguka kuwa hajawahi kusema kuwa anataka kumwagia tindikali lakini amekiri kuwa Sasha amevunja ndoa yake.